#COVID19 Maabara ya Taifa (COVID-19), wateja wakiulizia majibu au kuomba msaada sio uhalifu

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Kama kichwa cha habari hapo juu. Kwanza niwapongeze hapo maabara kwa kuweka namba za simu yaani customer care au kwa kizungu call center. Ili mwenye malalamiko au maswali apate Majibu.

Sasa basi hapa ndio kuna tatizo. Hawa watu wa kupokea simu kutuona sisi wateja kama wahalifu au tunapoteza muda.

Sisi ni wateja tuna haki ya kupiga simu na kuuliza chochote mradi hatuvunji sheria. Pia tuna haki ya kuomba na kusikilizwa. Maana utakuta mtu wa simu anakujibu AHIRISHA SAFARI. Mpaka mtu unajiuliza hivi huyu anafahamu mimi naenda wapi na naenda kufanya nini na je anafahamu madhara au hasara ya kuahitisha safari. Maana huwezi kusafiri bila kuwa na cheti cha Majibu ya covid.

Nawaomba tena muhusika wa hii idara awaeleimishe hawa wahusika wa kuongea na wateja.
 
Usiamini call centre kwenye ofisi ya umma, bora utumie matairi ulopewa na mungu kufika kwa ofisi😃

Kwenda kwenye digital globe ni wamelazimishwa ila mioyoni mwao wako kwenye barbaric system
 
Unapiga simu katika muda sahihi kuulizia Majibu yako. Yaani kuulizia huduma ambayo umeilipia. Customer anakujibu rahisi tu kuwa Majibu leo yamechelewa na hapo hakuna lugha ya kuomba msamaha yaani samahani yaani utadhani wewe mteja ni omba omba. . Unamuuliza sasa nitapata Majibu saa ngapi maana nasafiri na ndege ya muda fulani. Anakujibu kuwa Majibu yataanza kutoka muda fulani. Mfano baada ya masaa mawili. Kweli ule muda unafika na unasikilizia kwa muda wa saa moja. Unapiga tena simu Anakujibu muda si mrefu yanatoka. Unamwambia hapa nimebakiza dakika chache ndege itaniacha. Ndio anakujibu fuata maelekezo yangu au ahirisha safari. Hapo hajui kama hiyo safari unayoenda ina umuhimu gani. Na unaenda wapi. Hajui ticket ya ndege isiposafiri ina expire au inabidi ulipie tena. Hajui kuwa huko unapokwenda ulishafanya booking ya hotel na ulishalipia. Nashauri serikali I train hawa watu wa Call center ili waweze kufahamu ni kwanini wapo pale na pia wafahamu wanahudumia nini na wanahudumia watu wa aina gani.

Sent from my SM-A605G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom