mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 543
- 1,828
Wakuu,
Baada ya kukaa likizo bongo kwa wiki tatu nilifanya vipimo vya Corona na kulipia ada ya malipo ya Tsh. 230,000 siku ya Jumatano tarehe 4 ili nijiandae na safari yangu iliyokuwa jana siku ya Ijumaa tarehe 6.
Cha ajabu mpaka ilipofikia lisaa limoja kabla ya muda wangu wa safari bado majibu yangu hayakuwa yametoka, hali iliyosababisha nianze kufuatilia na kufanikiwa kupata namba za simu za emergency desk ya MAABARA ya TAIFA.
Nilipopiga na kumueleza shida yangu kwamba mpaka sasa sijapata certificate yangu ya majibu alianza kupaniki na kunifokea bila sababu za msingi huku akiniambia nisipotulia sitoipata.
Jambo hili lilisababisha niamue kufanya rapid test na kutoa pesa nyingine ya ziada tsh 60,000.
Mpaka sasa niko njiani nikisubiri kuunganisha usafiri mwingine kuelekea mwisho wa safari yangu na nikiangalia email naona sijatumiwa hayo majibu bado.
Sina la kusema zaidi ya kuwachukia watumishi wote wa MAABARA ya TAIFA.