M23 vs FARDC (DRC CONGO) Mapigano yaanza upya

M23 vs FARDC (DRC CONGO) Mapigano yaanza upya

mi najiuliza tu hivi makommando wetu kwa nini wasipewe fursa wakadungua mmojawapo wa hawa rebel leaders? Yaani sniper wao ameua Komando wetu roho inaniuma sana...inabidi kulipiza kisasi kwa kudungua high profile wao mmoja.

mwongozo wa kivita tafadhali Moshe Dayan
 
Last edited by a moderator:
Wakifanya hivyo mkuu watakuwa hawana akili timamu, maana nchi zote za SADC itabidi zimwage troops za kutosha CONGO DR na UN itawawekea vikwazo vikali vya kiuchumi, Hivyo hiyo ni ndoto ya alinacha. Hawawezi kujiingiza vita hivi moja kwa moja mkuu.

kwanza wanatuhofia sana Tanzania, hata kujaribu hawawezi, kelele za chura tu lakini ni vyema tuzidi kujipanga
 
Vita vya Congo ni biashara ya Museveni na Kagame, wananufaika na uporaji wa rasilimali za Congo mashariki. Ndio sababu wanaichukia sana nchi yetu kupeleka majeshi Congo

Inatakiwa ujue hii vita wanufaika ni wengi kwa mgawanyo tofauti
1. Museven na Kagame wananufaika kwa kupora Rasilimali(Madini) za DRC
2. Tanzania tunanufaika kwa Viongozi wachache kujinufaisha kujimegea fedha zinazolipwa na UN mfano zile fedha za Commoro. na ndio maana unaona tunapenda sana kushiriki na kuwa kimbelembele katika hivyo vita.
 
Napendekeza waende mpaka Nairobi wakawafurushe Alshabab.

Unazungumzia Al Shababu kikundi hiki kiliingia nchini na hakuna aliowakamata na kwa taarifa ya Mwakyembe wanamahusiano na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali.

Soma hapa chini.

Jeshi la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua. Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.

Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili “kuwapumbaza Watanzania wote” baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.

Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe

“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.

“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.

“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.

“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).

“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

"Usalama wa Taifa, Polisi wataka kuniua" - Mwakyembe - wavuti.com

Na kuna uwezekano wa FDRL wakapewa mafunzo ili warudi kuipindua Serikali ya Kagame.
Huyu Kagame nafikiri ni mjinga na ame msicalculate vibaya sana.
Alipokuwa anamtukana Rais wetu Kikwete, hakujua kuwa katika muda wa miezi sita tu atakuwa anafikiria for his own survival strategies.
Nmependa hii ya Tanzania kufanya mabo kimya kimya , kama wajinga vile, lakini Kagame sasa ameelewa , inabidi atubu tu.
 
Baada ya kuungwa mkono na hao raia Wa DRC wewe kama Mtanzania utakuwa umenufaika na nini? wakati nchi imepoteza Askari mwenye utaalam wa juu na amesomeshwa kwa gharama kubwa ambazo hao Wa DRC hawakuchangia chochote zaidi kilichotumika ni kodi zetu Watanzania.
Hiyo nukuu ya Nyrere chini ya post yako inakusuta. Mwanajeshi anasomea ujuzi wa kupigana ili aweze kuutumia katika vita. Siyo kupata vyeti vya kupamba ukutani. Hao waliokufa walikuwa wanatimiza majukumu yao kama wapiganaji. Kufa katika vita kwa mwanajeshi si jambo la ajabu. Ndiyo mkataba alioingia. Anyaway, kila mtu ana siku yake ya kufa ni swala la muda tu.
 
Unajua maana ya JWTZ? ukijua maana yake utaelewa nazungumzia nini kufa kwa mwanajeshi sio kitu cha ajabu lakini tujiulize kafa akitetea mipaka ya tanzania na raia wa Tanzania au kafa akitetea Mipaka ya nchi nyingine na wananchi wa nchi nyingine?
Tumeshuhudia kwenye Taarifa ya Habari kwenye TV ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu lakini badala ya waziri nahoza kuwafariji wafiwa yeye anakuja na hoja kuwa wanajeshi wetu hawatakata tamaa na wataendelea kupigana ili kuwasaidia wananchi wanyonge wa DRC bila kuzungumza hao ndugu waliokuwa wakimtegemea huyo marehemu watasaidiwa vipi ili maisha yao yaendelee kwani pia ameacha mtoto mmoja.
 
kama ndo hivyo basi pendekeza Tanzania ijitoe UN na UN isiwepo kabisa duniani.
 
hayahaya jirani yake navamiwa na majambazi hatakutoa msaada wa kupiga sim polisi au kamajirani wengine haliwezi,dume zima unalikuta limejificha chini ya uvnngu,watu eanadhani kwammba sisi hatuathiriki na vita ya CONGO,tunaathiriwa sana tu,fikiria hayo majambazi huko KG na kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika yanatoka wapi kama sio hawa waasi,kingine kuwa hifadhi wakimbizi nigharama kubwa sana kwetu,M23 lazima waiache Congo ijiendeshe sasa
Mkuu juzi tu Rais wetu amefungua Tender ya Wawekezaji watakaotaka kuwekeza katika VITALU vya Gasi katika Ziwa Tanganyika, hivi hao Rwanda wangekuwa nao Ziwani si ingekuwa balaa.
Jirani hata kama ni maskini asaidiwe huwezi jua MUNGU atakulipa nini au hilo LIADUI LINALOTAKA KUTAWALA MAZIWA MAKUU huwezi jua tamaa zake linaweza kutuvamiaYaani
hao watu hawafai kabisa kuwa nao SHARE /PARTINER watakuzunguka tu. Tusubiri EAC
 
Unajua maana ya JWTZ? ukijua maana yake utaelewa nazungumzia nini kufa kwa mwanajeshi sio kitu cha ajabu lakini tujiulize kafa akitetea mipaka ya tanzania na raia wa Tanzania au kafa akitetea Mipaka ya nchi nyingine na wananchi wa nchi nyingine?
Tumeshuhudia kwenye Taarifa ya Habari kwenye TV ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu lakini badala ya waziri nahoza kuwafariji wafiwa yeye anakuja na hoja kuwa wanajeshi wetu hawatakata tamaa na wataendelea kupigana ili kuwasaidia wananchi wanyonge wa DRC bila kuzungumza hao ndugu waliokuwa wakimtegemea huyo marehemu watasaidiwa vipi ili maisha yao yaendelee kwani pia ameacha mtoto mmoja.

1. JWTZ maana yake ni Jeshi la wananchi Tanzania. Wapi imeandikwa kuwa wako limited to protecting our borders only? kulinda borders zetu ni mojawapo tu ya kazi za jeshi hili, usipotoshe mambo hakuna dhambi yoyote kisheria wala kimaadili inayozuia jeshi letu kutumika nje ya nchi kwa shughuli za amani. Hivi wewe ungekuwa Nyerere usingeruhusu jeshi letu kupigania uhuru wa afrika kusini, msumbiji, angola n.k?
2. Kuhusu wafiwa ofcourse taratibu zote za kijeshi zinazopaswa kufanywa zitafanywa. Uanajeshi ni kazi kama zingine kuna mishahara, kuna mafao n.k.
3. Naomba nikuulize umefurahi kupigwa kwa M23 au umechukia?
 
Inatakiwa ujue hakuna anaependa Vurugu na vita sehemu yeyote hapa duniani, kupigwa kwa M23 napenda kutoa pongezi kwa Vikosi vya jeshi vya DRC kwa kuwaondoa hawa waasi kama Taarifa zinavyoeleza kwamba ni wao ndio waliowapiga hawa M23 cha ajabu kinachonishangaza ni pale wanaopigana ni jeshi la DRC lakini wanakufa wanajeshi wetu kulikoni?. maana hakuna taarifa inayotanabaisha kuwa M23 wamepigwa na majeshi ya UN kwa nini wanaficha?
 
UN wanasaidia majeshi ya serkali.. Aim yao kwa pamoja ni kuwamaliza M23. Cha msingi ni kuhakikisha Congo pako safi ili biashara na mambo mengi ya kiuchumi yanaendelea, that country is resourcefull and as Sitta said.. watakuwa good partners kuliko the coalition of the willing..
 
Napendekeza waende mpaka Nairobi wakawafurushe Alshabab.

Usijaribu ukali wa panga kwa shingo,huwezi kupigana na watu wasio na uwanja wa vita ama mapigano.WATAKUJA KIMYAKIMYA HAPA WALETE BALAA.hao upelelezi ndo unawafaa
 
hawa jamaa aisee wamesababisha madhara sana eastern congo. ICC iwashugulikie asap
 
Baada ya kuungwa mkono na hao raia Wa DRC wewe kama Mtanzania utakuwa umenufaika na nini? wakati nchi imepoteza Askari mwenye utaalam wa juu na amesomeshwa kwa gharama kubwa ambazo hao Wa DRC hawakuchangia chochote zaidi kilichotumika ni kodi zetu Watanzania.

Marekani imepoteza askari elfu ngapi Iraq na Afghanistani?

Unadhani wao ni wajinga?
 
Inatakiwa ujue hakuna anaependa Vurugu na vita sehemu yeyote hapa duniani, kupigwa kwa M23 napenda kutoa pongezi kwa Vikosi vya jeshi vya DRC kwa kuwaondoa hawa waasi kama Taarifa zinavyoeleza kwamba ni wao ndio waliowapiga hawa M23 cha ajabu kinachonishangaza ni pale wanaopigana ni jeshi la DRC lakini wanakufa wanajeshi wetu kulikoni?. maana hakuna taarifa inayotanabaisha kuwa M23 wamepigwa na majeshi ya UN kwa nini wanaficha?

Wanajeshi wetu wako kulinda amani hivyo ingawa hawapigani lakini wanasindikiza FARDC wao wakiwa wanalinda raia. Hata huyu askari wetu alikufa akiwa analinda raia wasipigwe risasi na M23.
 
Wanajeshi wetu wako kulinda amani hivyo ingawa hawapigani lakini wanasindikiza FARDC wao wakiwa wanalinda raia. Hata huyu askari wetu alikufa akiwa analinda raia wasipigwe risasi na M23.

Acheni kuandikiana habari za kijinga humu hivi M23 adui yao alikuwa na Raia na kama raia ni adui zao mbona maeneo waliyokuwa wanayashiria yalikuwa na Raia wengi tena sana mbona hawakuwaua? Msitake kuleta habari za UDAKU wanajeshi wetu wapo mstari wa mbele wa mapambano na ndio wanaoongoaza vita dhidi ya M23 na ndio maana wanauawa, mbona sijasikia wanajeshi wa Malawi au South Africa wameuawa?
 
Back
Top Bottom