Gotta UTube this stuff.
wameitaja JF au?
wameitaja JF au?
Yah, Imetajwa kwenye kikao. Na baadhi ya wajumbe ambao wanaweza kumudu hii njia mpya ya mawasiliano wamepewa jukumu la kujiunga na kujibu mapigo. Kuanzia sasa angalia ID za wachangiaji wa hoja za CUF/Lwakatare nyingi zitakuwa ngeni na mpya.
Pundamilia07 said:Je, kwanini Mh Lwakatare hajisafishi katika tuhuma ambazo aliambiwa kuwa alifanya ubadhirifu wa fedha ya chama? Kukaa kimya maana tutaelewa kuwa tuhuma zilikuwa ni za kweli.
Omutwale said:Baada ya kujitambua kuwa nina extreme affection na Lwakatare sikupenda kabisa kuwa mchangiaji katika hii thread. Maana nilijua kwa ukweli kabisa kuwa siwezi kuwa neutral. Sipendi kuwabore kama yule ndg yetu ambaye akipenda mtu hataki asemwe vibaya.
Pamoja na maelezo mazuri nadhani wewe huenda ni muhusika mkuu na wa karibu sana katika hili suala la Mh Lwakatare. Na kwa kuwa tayari umeshaonesha kufahamu mengi ya ndani, basi si vibaya ukatuambia ni kwanini Mh Lwakatare hajazungumzia kwa undani au kujisafisha dhidi ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama chake?
Hili swali uliniuliza kwenye thread ya Kutoka kwa Lwakatare. Ulisema hivi:
Nikajibu hivi:
Pia ukapata majibu kwa urefu sana toka kwa Mkandara.
Sasa tena:
Labda nirejee maneno ya Prof. Lipumba. Lwakatare HANA TUHUMA YOYOTE NDANI YA CUF. Hiyo unayoikomalia kama tuhuma aliisema mwenyewe Lwakatare mbele ya Balaza akitaka viongozi watamke wazi na bayana kuhusiana na minon'gono ambayo mahasidi wake wamekuwa wakiitoa kama sababu za yeye kutoteuliwa tena. Ni sababu mbili wamekuwa wakitoa:
!. Lwakatare ni mbadhirifu (Japo bila uthibitisho wa viongozi wakuu wala si tuhuma rasmi)
2. Uwezo wa kiutendaji wa Lwakatare umepungua.
Toka hapo juu sifikiri kama inawezekana usikie minon'gono, uje nazo mbele ya Balaza kujishtaki, Balaza na viongozi waseme huna tuhuma yoyote, halafu wewe uanze kujitetea.
Labda ebu niambie Pundamilia07; nguo iliyo safi kabisa iliyonyooshwa tayari kwa kuvaliwa, huwa unairudisha laundry ifuliwe pasipo kuchafuka kwanza?
"Baada ya kuyapitia alimhoji Mwenyekiti kuwa kwa nini Jina la Wilfred M. Lwakatare halikuwemo na hasa ikizingatiwa kuwa ndiye hadi kipindi hicho alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu (Bara) alihoji iweje Juma Duni Haji apewe fursa ya kutetea nafasi yake aliyokuwa nayo lakini Wilfred Lwakatare asipewe nafasi hiyo pia.
5. Mhe. Mwenyekiti na Wah. Wajumbe wa Baraza Makamu Mwenyekiti alijibiwa na nyie wenzake wawili kuwa Lwakatare ana matatizo. Na matizo yake ni kuwa si mwaminifu katika Masuala ya fedha, ni mbadhirifu na mtumia madaraka yake vibaya kwa kulazimisha hati za malipo anazotaka zifanyiwe malipo zilipwe iwe isiwe.
Makamu Mwenyekiti alizidi kuwauliza wenzake iwapo imeshindikana kumuita Lwakatare na kumuonya kuhusu tabia hiyo na akashindwa kujirekebisha kuliko kuacha jina lake kabisa. Anasema akajibiwa kuwa tabia zote Lwakatare
anaweza kuonywa na kujirekebisha lakini kwa masuala ya fedha ni sugu hawezi kusikia cha mtu. Mwishowe uamuzi wa kulitosa jina la Lwakatare ukaridhiwa na wote watatu na huo ndio ulikuwa ukweli wa suala lenyewe.
Alimalizia Mhe. Machano Makamu Mwenyekiti wetu
Na matizo yake ni kuwa si mwaminifu katika Masuala ya fedha, ni mbadhirifu na mtumia madaraka yake vibaya kwa kulazimisha hati za malipo anazotaka zifanyiwe
malipo zilipwe iwe isiwe.
makahaba ya kisiasa!
Hayo 'matatizo kibao' ndiyo yaliyomuondoa Lwakatare CUF mara baada ya kutemwa Unaibu Katibu Mkuu. Inaonekana ile hoja ya ubadhirifu ni valid. Inawezekana Mheshimiwa alikuwa anamalizia shida zake kwenye kofia ya Unaibu Katibu Mkuu na mara baada ya kuondolewa sasa inakuwa imeshakuwa taabu, CUF haiwezi kukalika.Mhe. Mwenyekiti, nilielezea kwa kirefu wakati tukijadili agenda ya kupitia muhtasari
na yatokanayo juu ya kutoridhishwa na namna mlivyopokea na kulishughulikia
suala la Mafao yangu na Matatizo yangu. Mhe. Mwenyekiti na wahe. Wajumbe
pamoja na kuonekana nadhifu na kuendesha gari la vx nililopata kutokana na kura za wana Bukoba mwaka 2000 lakini mimi nina matatizo "kibao" kama nilivyowaambia.
Soma hapa chini:
Hivi haya maneno asingeyasema na kuyaandika Lwakatare wewe na wengine wangeyapata wapi? Unataka hayaseme kwa mtindo upi ili uridhike?! Huwezi kujiweka pingu, ukajipeleka polisi, kisha ukajiongoza kizimbani na kujishtaki ilihali ukiwa unajua unamakosa.
Ukisoma vizuri alama za nyakati, CUF imepoteza mvuto wa kitaifa na kimkoa. Mgombea mtarajiwa yeyote mwenye kupiga hesabu vizuri hata kama anao mtaji wa wapiga kura, kugombea kupitia CHADEMA ndiyo turufu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ubunge.
Omutwale,
Hizi ni siasa, kama aliamua kusema yale maneno kwa faida za kisiasa basi ajue amejiingiza mahali ambapo hawezi kutoka kwa kupiga gia ya rivasi au kama hivyo. Hapa kinachotakiwa ni kwamba kama yale maneno hayakuwa na maana yeyote basi hakuwa pia na sababu ya kuyatamka.
Kwa vile aliyatamka mwenyewe, basi hana budi kuchukua hatua muafaka za kujisafisha dhidi yake. Vinginevyo ukweli utabaki kuwa hivyo na atapata taabu kubwa pale ambapo tuhumu zikirudi kutoka upande mwingine.
Nina wasiwasi mkubwa yale maneno yana ukweli ndani yake japo kuwa wewe unataka yawe diluted.
Ni mimi ndiye napata taabu sana kukuelimisha wewe na si Lwakatare kueleweka kwa wapiga kura. Ningeweza ningeweka Mkanda wa Mkutano wake alioufanya BK trh 19 mwezi huu ili nawe ujionee na kujisikilizia.
Tunafua nguo chafu, tusafisha viatu walau hata kama vina vumbi lakini je, tunaweza kuyaosha maji yaliyo safi?
Pundamilia07, naona tunaanza kuufanya mjadala kuwa wetu. Waonaje tusi-bore na tuingie vyumba vya ndani (PM)?!