Monsignor
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 523
- 13
Ranmarwa,
Mkuu hii inaonekana kama hadithi simulizi zaidi ya Ukweli maanake kila naposoma kuna majungu, visokorokwinyo na kadhalika..
Hawa viongozi wa CUF kama kweli Lwakatare alipewa millioni30/ na akatumia Millioni 5 tu iweje washindwe kumuuliza/kumwajibisha ila wammezee ati wamsubiri ktk uchaguzi!.. hao viongozi wa CUF walitegemea kuwaeleza nini wananchi ikiwa millioni 30 zimetumika vibaya na sii fedha toka mifukoni mwao..hizo millioni 25 pungufu zimehesabika vipi ktk vitabu vya chama ikiwa Lwakatare ataondoka chama kabla ya kutakiwa kujieleza..
Kisha unasema ati Lwakatare aliulizwa sababu ya kupinga jina la Joram akashindwa kujibu.. Mkuu tafadhali, Lwakatare alikuwa naibu Katibu mkuu iweje ashindwe kujibu ikiwa jina lake limeenguliwa wakati viongozi wengine wote majina yao yalirudi! Na wala sioni sababu ya kuulizwa swali hilo ikiwa hao viongozi wa CUF wameliondoa jina la Lwakatare bila kumweleza yeye sababu.. Kwa nini wao watake kujua sababu ya kupinga ikiwa kahupewa sababu ya kutolewa...maamuzi yao hayakuwa na maelezo..
Kifupi ni hivi CUF wamechoka Lwakatare na sababu zipo nje kabisa ya matumizi mabaya ya fedha kwani kama ingekuwa hivyo basi wanachama wa CUF wangeisha pewa hesabu hizo na matumizi hayo mabaya.. Na nakuhakikishia sii Lipumba wala Seif wanaweza ku raise hii issue kwa sababu hawa wote ni Opportunist nina hakika wametumia fedha vibaya kuliko huyo Lwakatare..Opportunist mwninge..
Kifupi wanasiasa wengi Bongo kama sii wote ni Opportunist, hawakuingia siasa bila kutegemea malipo bora na ujanja ujanja laa sivyo wangekuwa wakiachia nafasi hizo baada ya awamu mbili za kushindwa ama kuweka ushindani wa kweli within vyama hivyo.
Mara zote utakuta nafasi ya Mwenyekiti wanagombea Lipumba vs Mkandara asiyejulikana kabisa wala uanachama wake.
Makamu mwenyekiti, Sief against Mkandara!
sijui kiti cha nini Duni against Mkandara..basi ili mradi kurudi kwao madarakani ni LAZIMA..
Mkandara,
Jamaa mwenyewe alishasema hii ni story japo akasema full story lakini inabaki ni story vilevile. Hapo kaongea kikurya angaongea kiswahili angesema "hadithi." Labda tumwulize kama Sara Dumba aalivyokuwa akiwauliza watoto wa kipindi cha mama na mwana RTD enzi zileeeeee. "Hadithi hiyo alikufundisha nani na inamaanisha nini?"