Hayo 'matatizo kibao' ndiyo yaliyomuondoa Lwakatare CUF mara baada ya kutemwa Unaibu Katibu Mkuu. Inaonekana ile hoja ya ubadhirifu ni valid. Inawezekana Mheshimiwa alikuwa anamalizia shida zake kwenye kofia ya Unaibu Katibu Mkuu na mara baada ya kuondolewa sasa inakuwa imeshakuwa taabu, CUF haiwezi kukalika.
Mheshimiwa ameonesha kuwa yeye ni kiongozi mbinafsi wa hali ya juu kabisa hasa pale anapoitaka CUF iweke sera maalum za kuwaenzi 'wastaafu' baada ya yeye kutemwa katika safu ya uongozi wa juu. Ni kwanini hakupigania hili wakati akiwa kiongozi kwa ajili ya wale ambao tayari si viongozi tena? Au aliona kuwa yeye yuko mbali na ukweli siku moja naye hatakuwa kiongozi wa juu?
Pili, inaonekana kuwa Mheshimiwa pamoja na kuwa na juhudi nyingi lakini hakuwa na vision na hili linadhihirika pale baada ya muda mfupi kutolewa katika madaraka ya juu analalamika jinsi ambavyo CUF imekosa mwelekeo katika siasa za bara na hata kudiriki kusema CUF inatia aibu. Hapa Mheshimiwa anasahau kuwa yeye ndiye aliyekuwa namba tatu na pia akiwa na jukumu la pekee la kusimamia shughuli za chama kwa upande wa bara?
Mheshimiwa Lwakatare, nadhani hana jipya zaidi ya kusaka kiti cha Bukoba Mjini. Kwa mtazamo wangu Lwakatare angekuwa radhi kwenda CCM ili mradi tu kama angehakikishiwa kuwa atapendelewa ateuliwe kugombea kiti cha ubunge cha Bukoba Mjini. Lakini kwa utaratibu ambao CCM wameamua kuuchukua si rahisi kwa mtu kama Lwakatare aweze kupenya na kufikia jina lake kuwekwa kama mgombea wa CCM. Safari yake ya kwenda CHADEMA ameiona kuwa inaweza kumnufaisha kwa vile chama hicho kwa sasa kinaangalia sura ya mtu na jinsi anavyoweza kuwapatia ushindi hata kama anamushkeli.
Kwa kweli, pamoja na matatizo yote ya Lwakatare, hayo yanayoitwa matumizi mabaya ya fedha hayapo, maana Lipumba aliulizwa swali na kujibu, "hatumdai wala hatuna kashfa yoyote dhidi yake" na hiyo ni kauli ya uhakika, maana hakukuwa na tuhuma zozote zilizojadiliwa katika vikao vyote kabla na baada ya Lwakatare kuondolewa katika Unaibu Katibu Mkuu.
Lakini, tujue suala moja hapa kwamba, hakuna mtu anayeingia katika siasa kuwa mtumishi tu wa wengine, wote wana matarajio ya kupanda ngazi.
Aliwahi kusema Dr. Gharib Bilali, kwamba, "mimi ni mwanasiasa, nimeshakuwa Waziri Kiongozi, kwa hiyo lazima niangalie juu zaidi, kuanzia urais wa Zanzibar hata wa Jamhuri ya Muungano". kwa hiyo kama mwanasiasa anaona maslahi yake kisiasa yanahatarishwa katika chama husika, na kwa kuwa ni mwana mageuzi, chaguo la kwanza ni kwenda katika chama ambacho anaona kimeshika chati katika eneo husika, na kwa sasa Chadema ndicho chama cha upinzani chenye nguvu bara. Chaguzi ndogo za hivi karibuni zimedhihirisha.
Lakini jambo lingine lililo wazi ni kuhusu CUF kuanza kupoteza kuungwa mkono kwa wao kuamua kwenda "kivyao vyao" wakati wananchi na wanasiasa wenzao wakiwamo wa CCM wamebadili mbinu na kwenda kwa wananchi na kufuata wananchi wanavyotaka. Kwa sasa hata hao munaowaita mafisadi, wanahutubia na kusema "wanapambana na ufisadi" na hiyo ndiyo turufu ya sasa. Sasa Lwakatare anaangalia alama za nyakati.
Pamoja na kuwa sipendi, si vibaya kwake kwenda hata CCM ikiwa CHADEMA watamkataa (miujiza) kwani siasa ni popote, inategemea na mkakati wa mtu mmoja mmoja. Naamini Lwakatare hayuko sawa na kina Akwilombe na Tambwe Hiza, kwa kuwa amewahi kuwa Mbunge na Kiongozi wa Upinzani. Ana wafuasi na imedhihirishwa na mikutano yake. Mwanasiasa ni watu.
Suala la mwisho, ni kwamba kwa muda mrefu sana Lwakatare amekuwa na msimamo wa kuwa na ushirikiano na vyama, na wenzake walikuwa hawataki mahusiano na CHADEMA na ndio maana amekuwa akituhumiwa kutoa "siri" kwa CHADEMA. Naamini hakukuwa na siri zozote bali ni mambo ya uninafsi tu, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha na mikataba feki. Kuna mambo mengi ya ovyo ikiwa ni pamoja na aibu ambayo ikipasuka itakiabisha chama cha CUF, ikiwa ni pamoja na kuwapo taarifa za mizigo yake kukamatwa mpakani ikitumika kukwepa kodi na mfanyabiashara ambaye ameingia mikataba ya ovyo na viongozi. Wao wenyewe ndani wanalalamika, lakini Lwakatare aliwatetea na leo hii hata waandishi wakimuuliza anagoma kutoa hiyo siri ikiwa ni pamoja na kukataa kutoa siri ya RA na CUF.
Mwacheni Lwakatare aamue pa kwenda hata ikiwa ni CHADEMA ama CCM