Mimi naijua full story ya lwakatare.Alikuwa mpiga debe wa hali ya juu CUF,mwaka 2000 lipumba akamteua kuwa naibu katibu mkuu bara na baraza kuu la uongozi la chama chake likampitisha,then baada ya uchaguzi wa ndani ya chama wa CUF wa mwaka 2004 Lipumba aliposhinda alimteua kuwa naibu katibu mkuu tena.
Mwaka 2005 nyote mnakumbuka Chama chake kilipigana naye bukoba mjini lakini wakashindwa kwa balozi kagasheki(kagasheki alimshinda lwakatare kwa kura 130 tu)Baada ya kushindwa alifungua kesi ya kupinga matokeo hayo,yeye lwakatare ndiye aliyeongoza chama chake CUF katika chaguzi ndogo kadhaa za tunduru,mbeya vijijini na kwingineko(isipokuwa busanda).
Mwaka jana 2008 alikuwa kwenye mgogoro mkubwa na viongozi wake wa juu baada ya kutumia tshs 30,000,000(milioni thelathini) vibaya (alipewa pesa hizo akasimamie zoezi la daftari la wapiga kura kwa muda wa mwezi mzima) lakini akawashangaza wakubwa pale aliporudi baada ya wiki moja na kudai pesa zote zimekwisha huku ushahidi wa maafisa wa ngazi za chini alioenda nao ukionesha pesa zilizotumika kwa hiyo wiki moja hazizidi hata 5,000,000(milioni tano).Hiyo haikuwa mara ya kwanza,inasemekana huko nyuma alikuwa na rekodi chafu ya matumizi ya pesa ndani ya chama chake.
Inasemekana wakubwa walitaka kumuondoa mara moja lakini wakaona itaharibu sura ya chama chao,wakalimezea suala hilo na kukaa kimya kwani walijua bado miezi sita tu uchaguzi mkuu mwingine wa ndani ya chama ufanyike na walikuwa wakimtegea hapo.Uchaguzi mkuu wa chama cha CUF uliofanyika mwezi march mwaka huu ndio uliwaleta tena madarakani lipumba,machano na seif sharif na ndipo wakamtema lwakatare.
Inasemekana katika mkutano huo mkuu wa chama lwakatare alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza kuu la uongozi la taifa la chama hicho na tena alikuwa ana matumaini makubwa kwamba lazima atateuliwa kuwa naibu katibu mkuu kwani inasemekana aliwahi hata kutamka kwamba bila yeye tanzania bara chama hakipo.Siku ya uteuzi wa wakurugenzi na manaibu katibu wakuu wa zanzibar na tanzania bara ilikuwa siku moja baada ya mkutano mkuu wa chama.
Wajumbe wapya wa baraza walikutana ili kupokea uteuzi na kuukataa au kuukubali na mmoja wa wajumbe hawa alikuwa lwakatare huku akiwa anaamini kwa asilimia 100 kwamba lazima atateuliwa kuwa naibu katibu mkuu.Inasemekana alipata mshtuko mkubwa pale ambapo yalitajwa majina mawili kwa upande wa bara huku lake likiwa halimo na ndipo wajumbe wa baraza wote wakampigia kura JORAM BASHANGE.
Kutokana na mshtuko alioupata lwakatare palepale hakuchelewa alisimama na kutamka kikaoni hapo kwamba yeye anapinga uteuzi wa JORAM BASHANGE,alipoulizwa sababu ya kupinga akawa hana,na ndio kutokea hapo ikawa haieleweki;akaanza kuwaponda CUF na LIPUMBA na wengineo kwamba hawafai na wamekipeleka chama hicho kubaya.
Ikumbukwe kwamba lwakatare alikuwa anaongoza mambo yote ya utendaji wa chama na mikakati upande wa bara,na amekuwa katika kuongoza utendaji wa chama chake kwa miaka 10,iweje leo hii asipewe nafasi ya juu ndo anaanza kusema chama kimepoteza mwelekeo?
Nashauri ma-thinker wote walitizame suala hili vizuri bila ushabiki,iweje mtu anyimwe nafasi ya juu ndo anaona chama kibaya na waliomo hawafai?
Hivi tuseme leo hi lwakatare angekuwa ameendelea kuachiwa nafasi ya naibu katibu mkuu angetangaza kukihama chama chake?
Hivi leo hii mtu akinyimwa nafasi mahali ndio anahama? Viongozi wa namna hii sio wazuri hata kidogo.
Mimi nadhani ni yeye ndiye anajimaliza,ninamaanisha lwakatare anajimaliza mwenyewe- sote tunachojua ni kwamba anahitaji kulirudisha jimbo la bukoba vijijini mikononi mwake tena anakiri kwamba jimbo lile ni lake kwani alinyang'anywa na ccm mwaka 2005,if that is the case alihitaji kutulia ndani ya cuf na kuimarisha mtandao wake ili apate madaraka aliyokuwa anayahitaji.
Kwa kuhama kutoka cuf it means anaanza upya na chadema na najua ha taweza kuondoka na hata nusu ya wafuasi wa cuf bukoba mjini na hiyo itam-cost kwenye uchaguzi ujao kwani atamrahisishia kazi kagasheki iwapo cuf watamsimamisha mgombea mwingine anayekubalika.
Lakini pia napata bad news sasa hivi kwamba imebainika baadhi ya wabunge wetu wa CHADEMA wanachangishana ili kumuongezea nguvu lwakatare huko na tena jana usiku kulikuwa na kikao kati ya madiwani wa CUF walioko bukoba vs Lwakatare na viongozi wa chadema na madiwani wale wameahidiwa kupewa pesa za kampeni za uchaguzi mkuu ujao iwapo watang'oka CUF na kujiunga CHADEMA.
Habari hizi ni za uhakika na hivi ndio vyama vyetu vya upinzani.