Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Inaonekana wewe ndio uliomuandikia hizo barua zake zina makosa mengi ya kiswahili.

It goes without saying that my swahili is mgogoro?

Taratibu wasikusikie wenyewe walio pata kijana msomi na machachari
 
Kyaruzi said:

Kyaruzi,

Mbona unakuwa kama kyaruzi wa kuchongwa??! Umesahau kuwa uwezo wetu Watalwe ni Ngeli ya UK na Kihaya! Wewe Bwana vp, what are you wondering here? Utani tu Mkuu....

Anyway, lengo ilikuwa ujumbe uliyomo kwenye hayo maandishi. Maadamu ujumbe umefika na watu wameuelewa basi lengo limetimia.
 
Yaliyojiri leo hii BK mjini:

Hadi kufikia jioni vitambaa vya kaki imekuwa bidhaa adimu madukani. Toka jana mafundi wamekuwa busy kushona magwanda ya wafuasi wa chama chenye mvuto mpya-BK; ambacho tayari kimeteka mjini

Kadi za chama hicho (..) zimekwisha ofisi kuu-BK. Wajasiriamali wamechangamkia fursa na kuomba vyeo vya ghafla kisha kutumia vyeo hivyo kuchukua kadi nyingi. Wakati ofisi kuu kadi ilikuwa inauzwa kwa TShs. 600, Wajasiriamali mtaani wanaiuza TShs. 1,000/= Duru zetu za kikachero hazijathibitisha kuwepo kwa mkono wa Kagasheki wala SISIm katika kununua kadi hizi.

Wajumbe wa Kaskazini wamewekewa ngumu kukodi ndege ya Any Time Cancelled Co. Ltd ambayo walikwisha i-book kwa safari ya kesho. Hivyo Wajumbe wa Kaskazini watatumia ndege za kawaida ambapo Prof. Mwesiga Baregu atatangulia asubuhi akiongozana na Dr. Slaa Kisha Mzee Ndessa Pesa na vigogo wengine watafuata.

Wale wenye msimamo mkali wa kidini (mimi simo) wameanzisha uvumi kuwa Maaskofu ndiyo waliomshauri Lwakatare atoke CUF na kwenda CHADEMA kwa ahadi ya kumpigia debe 2010. (Hii nitaelezea siku zijazo kampeni ya namna hii zinaweza kula kwa nani na kwa sababu gani)

Mwisho natoa salamu za pole kwa Mpambanaji na familia yake. Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja siku zote katika sala.

Nawakilisha.
 
Hiyo siyo kweli Nziku mimi naamini wale wanao hama hama ni watu wenye tamaa na uroho wa madaraka na kujiona wao ni miungu watu never Nziku lazima ukubaliane na maamuzi ya walio wengi

Ipole, nina maswali kadhaa kwako.
1. Hivi nini hasa ni uroho wa madaraka.
(a) Mwenye uroho wa madaraka ni yule ambaye tayari ana madaraka na hayuko tayari kuachia ama yule ambaye ndiyo anatafuta madaraka ?
(b) Mroho ni yule aliyehodhi madaraka yote na kwa wakati wote zote ama ni yule ambaye baada ya kutoridhika na utawala uliopo anapigania na yeye apate nafasi ya madaraka ?

2.Tuseme wewe ni mwanachama wa CCM
:-
(a) Ukikuta hukubaliani na matendo fulani fulani ndani ya chama na juhudi zako za kuleta mabadiliko ndani ya chama zikakwama ama kukwamishwa, je utahama ama utabaki humo humo ?
(b) Ukiamua kubaki humo je hautakuwa mshiriki hata katika kupitisha maamuzi ambayo nafsi yako inapingana nayo ?
(c) Je chama kikijiingiza kwenye matendo machafu na kuchafuka, utakuwa na haki yoyote ya kusimama kando na kudai eti wewe ni msafi ?

3. Kwa kuwa mtu hujiunga na chama kwa hiari yake mwenyewe :-
(a) Kitu gani kinakuzuia usihame kwa hiari yako mwenyewe kama hufurahishwi na utendaji ndani ya chama ?
(b) Kama ikitokea kuwa kwa kupinga matendo maovu ndani ya chama, unachukuliwa hatua yoyote ile kama kushushwa wadhifa ama kuvuliwa madaraka, je ukijitoa humo umefanya kosa ?
Chama hakiwezi kufanya uchafu kikabaki kisafi.
Mwanachama hawezi kushiriki katika uchafu akadai ni msafi
No,
one cant eat one's cake and have it !!
 
Mag3,
Ningekushauri uachane na Ipole. Akiona uongo anaita ukweli. Ukimpa ukweli anakwambia kwa heri.
 
Yaliyojiri leo hii BK mjini:

Hadi kufikia jioni vitambaa vya kaki imekuwa bidhaa adimu madukani. Toka jana mafundi wamekuwa busy kushona magwanda ya wafuasi wa chama chenye mvuto mpya-BK; ambacho tayari kimeteka mjini

Kadi za chama hicho (..) zimekwisha ofisi kuu-BK. Wajasiriamali wamechangamkia fursa na kuomba vyeo vya ghafla kisha kutumia vyeo hivyo kuchukua kadi nyingi. Wakati ofisi kuu kadi ilikuwa inauzwa kwa TShs. 600, Wajasiriamali mtaani wanaiuza TShs. 1,000/= Duru zetu za kikachero hazijathibitisha kuwepo kwa mkono wa Kagasheki wala SISIm katika kununua kadi hizi.

Wajumbe wa Kaskazini wamewekewa ngumu kukodi ndege ya Any Time Cancelled Co. Ltd ambayo walikwisha i-book kwa safari ya kesho. Hivyo Wajumbe wa Kaskazini watatumia ndege za kawaida ambapo Prof. Mwesiga Baregu atatangulia asubuhi akiongozana na Dr. Slaa Kisha Mzee Ndessa Pesa na vigogo wengine watafuata.

Wale wenye msimamo mkali wa kidini (mimi simo) wameanzisha uvumi kuwa Maaskofu ndiyo waliomshauri Lwakatare atoke CUF na kwenda CHADEMA kwa ahadi ya kumpigia debe 2010. (Hii nitaelezea siku zijazo kampeni ya namna hii zinaweza kula kwa nani na kwa sababu gani)

Mwisho natoa salamu za pole kwa Mpambanaji na familia yake. Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja siku zote katika sala.

Nawakilisha.

Wewe nawe acha kutufunga kamba hapa hata hao wenye Chadema yao TanzaniaDaima hawajafikia ushabiki huu.

Let me tell you my friend, you are up for the biggest dissapointment na Cha-chechemea wako
 
uJUMBE KWA MAALIM SEIF,LIPUMBA NA JUMA DUNI
ni wazi kwamba CUF Inapotea mwelekeo na ushawishi kule TZ baada ya kuondokewa na Luwakatare, ni chama kinachoyeyka kama nyasi zinvyoyakua katika moto mkali. nadhani imefika hatua haraka kwa Pr Lipumba, maalim seif, jusa, Duni, Machano, Dimani na wengine kujipanga upya. njia pekee ni kushirikiana na CHADEMA Katika siasa na sio kuwakumbatia mahututi wengine kama vile NCCR mageuzi, TLP au SAU katika siasa za TZ, tumieni elimu yenu kusoma mchezo wa siasa za tz kwani kama mtaungana na chadema katika saiasa ni wazi CUF iinaweza kucheza karata yake vyenginevyo Cuf itapotea tz bara kama vile ilivyopotea NCCR MAGEUZI. anagalieni Chadema ilivyoungana na nyinyi katia 95, 2000 katika siasa malengo yao yalikuwa kuijweka nyuma yenu kwani mlikuwa na nguvu, lkn sasa waomndio wapo juu kwahivyo hakuan budi na nyinyi kujificha kwenye kivuli chao
 
Yawezekana Lwakatare ni tumaini la Chadema kuelekea 2010?
Hukuna Lwakatale kusadia chochote mimi naamini atashindwa ameshindwa CUF ni chama cha udini lakini hiyo ni siri yake hawezi kusema anaenda chademe ni chama cha wachaga ashindwa pia chama ni CCM tu.
 
oh! now i know kumbe fix zako zote sababu ni 'chama ni CCM tu' lol. Mkuu fungua macho kidogo tu uone miaka kadhaa ijayo, watu wanabadilika kwa kasi sana. Ni kweli kwamba CCM ni chama chenye nguvu lakini haimaanishi ndo chama pekee. Mzarau mwibw mguu huota tende....
 
Hukuna Lwakatale kusadia chochote mimi naamini atashindwa ameshindwa CUF ni chama cha udini lakini hiyo ni siri yake hawezi kusema anaenda chademe ni chama cha wachaga ashindwa pia chama ni CCM tu.

SIZITAKI MBICHI HIZI.........

omarilyas
 
Yaliyojiri leo hii BK mjini:

Hadi kufikia jioni vitambaa vya kaki imekuwa bidhaa adimu madukani. Toka jana mafundi wamekuwa busy kushona magwanda ya wafuasi wa chama chenye mvuto mpya-BK; ambacho tayari kimeteka mjini

Kadi za chama hicho (..) zimekwisha ofisi kuu-BK. Wajasiriamali wamechangamkia fursa na kuomba vyeo vya ghafla kisha kutumia vyeo hivyo kuchukua kadi nyingi. Wakati ofisi kuu kadi ilikuwa inauzwa kwa TShs. 600, Wajasiriamali mtaani wanaiuza TShs. 1,000/= Duru zetu za kikachero hazijathibitisha kuwepo kwa mkono wa Kagasheki wala SISIm katika kununua kadi hizi.

Wajumbe wa Kaskazini wamewekewa ngumu kukodi ndege ya Any Time Cancelled Co. Ltd ambayo walikwisha i-book kwa safari ya kesho. Hivyo Wajumbe wa Kaskazini watatumia ndege za kawaida ambapo Prof. Mwesiga Baregu atatangulia asubuhi akiongozana na Dr. Slaa Kisha Mzee Ndessa Pesa na vigogo wengine watafuata.

Wale wenye msimamo mkali wa kidini (mimi simo) wameanzisha uvumi kuwa Maaskofu ndiyo waliomshauri Lwakatare atoke CUF na kwenda CHADEMA kwa ahadi ya kumpigia debe 2010. (Hii nitaelezea siku zijazo kampeni ya namna hii zinaweza kula kwa nani na kwa sababu gani)

Mwisho natoa salamu za pole kwa Mpambanaji na familia yake. Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja siku zote katika sala.

Nawakilisha.

Omutwale nimekuaminia ndugu yangu, kumbe data zote za Lwakatare zimelala kwako, asante kutujuvya, nimeshangaa yote ulo yaandika hapa, ndo haya hapa kutoka nipashe, kumbe hukuongeza chumvi.

Lwakatare ajiunga rasmi Chadema

Bw. Wilfred Lwakatare.

[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatimaye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara, Wilfred Lwakatare, ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lwakatare ambaye ni mmoja wa waasisi wa CUF, mwenye kadi namba 149, alitangaza uamuzi wake huo alipozungumza na Nipashe jana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema amefikia uamuzi huo, baada ya kupata baraka zote za wanachama 284 wa tawi la CUF lililopo kijijini kwake, Kibeta, wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lwakatare alisema kabla ya wanachama hao kutoa baraka hizo, zaidi ya wananchi 7,000 waliohudhuria mkutano wake wa hadhara, uliofanyika hivi karibuni mjini Bukoba, kwa kauli moja walimshauri ajiunge na Chadema isipokuwa wananchi wawili ndio waliopiga kura kumshauri ajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, alisema hawezi kurudisha kadi ya CUF kwa vile hakuna kifungu chochote cha katiba ya chama hicho kilichoweka utaratibu kwa mwanachama kurudisha kadi pindi anapoamua kukihama chama, hivyo, akasema ataitunza kadi hiyo kwenye hazina yake ya kumbukumbu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema amejitoa CUF baada ya kubaini kuwa imepoteza mwelekeo na haina programu nzuri, badala yake imekuwa chama kinachoendekeza fitina, chuki, majungu, kula njama za kukomoana na kwamba, imekuwa haitaki kupokea ushauri anaoutoa kupitia vikao halali vya chama ili kurekebisha hali hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema hali hiyo imesababisha chama kufanya vibaya kwenye chaguzi ndogo za hivi karibuni zilizofanyika kwa nyakati tofauti katika majimbo ya Mbeya Vijijini, Busanda na Magogoni, ambako alisema licha ya kutumia fedha nyingi, kiliishia kuambulia aibu.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Kupitia kikao cha Baraza Kuu, niliomba marekebisho ya matatizo hayo, lakini wenzangu hawakunielewa. Badala yake, wakaanza kunikejeli eti nataka Unaibu Katibu Mkuu. Mimi Sitaki Unaibu Katibu Mkuu, nataka CUF iendelee. Nikaona kumbe hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu….Bado kuna haja ya kuangalia niliyoyasema kwenye kikao cha Baraza Kuu, ili wanihukumu kwa yale niliyoyasema na siyo kunitungia uzushi," alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, alisema licha ya kufikia uamuzi huo, bado anaipenda CUF na kwamba, yuko tayari kuisaidia kwa vile anaamini katika ushirikiano baina ya vyama vya siasa.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata kama katika Uchaguzi Mkuu mwakani CUF kama wataweka mgombea anayekubalika katika Jimbo la Bukoba Mjini, nitasaidia katika kampeni. Mimi ni muumini wa ushirikiano wa vyama vya siasa," alisema Lwakatare.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbali na Unaibu Katibu Mkuu, Lwakatare amewahi pia, kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini (CUF), Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Baraza Kuu la Uongozi, Mkutano Mkuu na Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama CUF Taifa. Alijiuzulu nafasi hizo wiki chache zilizopita kupitia kikao cha Baraza Kuu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lwakatare alibwagwa na mbunge wa sasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ikiwa atajitosa katika kinyang'anyiro hicho mwakani atachuana na Balozi Kagasheki kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitamteua. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo huo, Chadema kinatarajia kumpokea Lwakatare mjini Bukoba kwa ndege ya kukodi kutoka jijini Dar es Salaam.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lwakatare anapokelewa na Chadema baada ya juzi kutangaza rasmi kukihama CUF na kujiunga na chama hicho.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mapokezi hayo yatafanyika kesho ambapo ndege maalum itakodiwa kutoka jijini Dar es Salaam na kuwapitia wabunge wa Chadema mjini Dodoma na kisha kuelekea mjini Bukoba.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana kutokea mjini Dodoma, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, alithibitisha Lwakatare kujiunga na chama chake na kwamba wamekubali kumpokea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Ni kweli ninayo taarifa kuhusu Lwakatare kujiunga na chama chetu," aliema Dk. Slaa.[/FONT]
 
Yaliyojiri leo hii BK mjini:

Hadi kufikia jioni vitambaa vya kaki imekuwa bidhaa adimu madukani. Toka jana mafundi wamekuwa busy kushona magwanda ya wafuasi wa chama chenye mvuto mpya-BK; ambacho tayari kimeteka mjini

Kadi za chama hicho (..) zimekwisha ofisi kuu-BK. Wajasiriamali wamechangamkia fursa na kuomba vyeo vya ghafla kisha kutumia vyeo hivyo kuchukua kadi nyingi. Wakati ofisi kuu kadi ilikuwa inauzwa kwa TShs. 600, Wajasiriamali mtaani wanaiuza TShs. 1,000/= Duru zetu za kikachero hazijathibitisha kuwepo kwa mkono wa Kagasheki wala SISIm katika kununua kadi hizi.

Wajumbe wa Kaskazini wamewekewa ngumu kukodi ndege ya Any Time Cancelled Co. Ltd ambayo walikwisha i-book kwa safari ya kesho. Hivyo Wajumbe wa Kaskazini watatumia ndege za kawaida ambapo Prof. Mwesiga Baregu atatangulia asubuhi akiongozana na Dr. Slaa Kisha Mzee Ndessa Pesa na vigogo wengine watafuata.

Wale wenye msimamo mkali wa kidini (mimi simo) wameanzisha uvumi kuwa Maaskofu ndiyo waliomshauri Lwakatare atoke CUF na kwenda CHADEMA kwa ahadi ya kumpigia debe 2010. (Hii nitaelezea siku zijazo kampeni ya namna hii zinaweza kula kwa nani na kwa sababu gani)

Mwisho natoa salamu za pole kwa Mpambanaji na familia yake. Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja siku zote katika sala.

Nawakilisha.

I love CHADEMA..... wanakwenda kisasa zaidi. Kuweza kuajiri watu 24/7 kushinda mtandaoni na kufanya spinning.. is not a joke!

Omutwale hongera amakweli unakula kwa jasho lako, maana kwa propaganda! utadhani ulipitia pale Kivukoni?
 
sema wewe shekhe mie mwenyewe nshagive up hawa jamaa ni kama mchwa vile duh!
 
Rwabugiri said:
Omutwale nimekuaminia ndugu yangu, kumbe data zote za Lwakatare zimelala kwako, asante kutujuvya, nimeshangaa yote ulo yaandika hapa, ndo haya hapa kutoka nipashe, kumbe hukuongeza chumvi.

Wakole waitu,
Asante Mkuu,
Thank you Sir,
 
I love CHADEMA..... wanakwenda kisasa zaidi. Kuweza kuajiri watu 24/7 kushinda mtandaoni na kufanya spinning.. is not a joke!

Omutwale hongera amakweli unakula kwa jasho lako, maana kwa propaganda! utadhani ulipitia pale Kivukoni?

Mkuu Kingwele,

Hicho chama huwa sikitamki mara kwa mara. Na wala sina mahusiano nacho hata chembe. Si kwa sababu ya chuki binafsi bali utofauti katika mitizamo. Ukisema Omutwale ni mfuasi mwadilifu wa Lwakatare na watu fulani hapa JF utakuwa una hoja. Maskini ya Mungu, wala huyo Lwakatare hajawahi na wala hajanikatia kwenye kale ka "Opportunity Cost Tranfer Fee" alikopewa, bali ni ile "extreme affection" niliyowahi kujieleza kuwa nayo kwake mwanzoni kabisa mwa sakata hili. Na huu ni mfano hai kuwaonyesha WaTZ, umaarufu wa Lwakatare si wa chama bali wa kwake yeye kama Lwakatare.

Mkuu Kingwele, nikuandalie Rubisi au utatumia Mramba? Karibu Uhuru platform!
 
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lwakatare anapokelewa na Chadema baada ya juzi kutangaza rasmi kukihama CUF na kujiunga na chama hicho.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mapokezi hayo yatafanyika kesho ambapo ndege maalum itakodiwa kutoka jijini Dar es Salaam na kuwapitia wabunge wa Chadema mjini Dodoma na kisha kuelekea mjini Bukoba.[/FONT]

Mimi hapa ndipo ninapokata tamaa na siasa zetu. Huyu jamaa si kajiunga kama mwanachama mwingine? Si akachukuwe kadi yake kwenye tawi linalomhusu bila hayo mapambio ya ndege, ujumbe mzito n.k. n.k.! Au ameahidiwa kuwa hatakuwa mwanachama wa kawaida huko anakokwenda? Hiyo gharama wanayoingia kwenda kumpokea si heri wangechima visima au kupeleka sola kijijini kwake ( au kitu kigine cha maendeleo) ? Naamini wote hao wazito watalipiwa nauli na kupewa Per. Diem!

Kweli safari ni ndefu.

Amandla...........
 
mag3.
Haya maneno yako ni hoja za nguvu sana. Nitayakumbuka daima.

Chama hakiwezi kufanya uchafu kikabaki kisafi.
Mwanachama hawezi kushiriki katika uchafu akadai ni msafi
No, one can eat one's cake and have it !!
 
Back
Top Bottom