Wakuu FM na Mwanawasu Masatu wala msitoane macho.
Pamoja na uwezo, nguvu,umaarufu, uhodari, au sifa yoyote utakayoweza kumpa Lwakatare lakini bado ukweli unasimama kwamba CUF itaendelea kuwepo, kwa suala la kuwa imara kama zamani sina uhakika. Na kwa kuzungumzia bukoba watakuwa wamepoteza wanachama na wafuasi wengi sana, watakaomfuata lwakatare kama ataamua kuhama chama.
Hata hivyo huyo aliyevaa viatu vya Lwakatare sio mtu wa kuwa na mashaka nae. Ni mtu mwenye msimamao thabiti haswaaa.Nilimuona na kumsikiliza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2005 akigombea jimbo la Mikumi na kushindwa na Clement wa ccm, lakini ukweli jamaa anajua kuzungumza, anajua kujenga hoja na kiukweli naamini jamaa anaweza. Joram Bashange aliwahi kuwa katibu wa TPAWU(tawi la kilombero sugar-sasahivi ILLOVO) wakati kiwanda hicho kinabinafsishwa kwa makaburu(ingawa kuna maneno ya chini chini kwamba makaburu walipewa K1 na mzee chenkapa & ze sumaye wakajigawia K2(samahani mzindakaya najua hupendi kuona huyu mzee akitajwa).Huyu bwana Bashange ameacha historia ya kukumbukwa kilombero sugar hadi kesho ukienda utasimuliwa, jinsi alivyokuwa imara kutetea haki za wafanyakazi wa kiwanda kile wakati wa ubinafsishwaji wake. Alipambana na uongozi wa wilaya, mkoa, na polisi kwa hoja kwenye vikao mbalimbali vilivyoitishwa kwa ajili ya kuweka mambo sawa na akawashinda.Inatajwa kuwa sababu mojawapo iliyopelekea Lukuvi kula shavu la uwaziri enzi za chenkapa ni baada ya kumtonya mzee mkapa madudu yaliyokuwa yamefanywa na watendaji kadhaa katika kushughulikia kadhia hiyo akiwemo waziri wa kilimo kipindi hicho mzee kimiti. Matokeo yake kimiti akapotezezewa baada ya uchaguzi mkuu wa 2000.Kumbuka tu kwamba vuguvugu la kubinafsisha kampuni ya kilombero sugar ilikuwa kati ya 1998 hadi 2000.
Nimalizie kwa kusema tu kwamba tumpe muda bw.Bashange tuone ataifanyia nini CUF, BTW bw.Bashange nae ni mtani wangu, dugu moja na Lwakatare (wote ni BK boys).Sasa sijui hapa Lipumba aliendeleza ukabila???!!!!anyway natania tu , turudi kwenye mada.