Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,907
- 1,080
Mkuu Kingwele,
Hicho chama huwa sikitamki mara kwa mara. Na wala sina mahusiano nacho hata chembe. Si kwa sababu ya chuki binafsi bali utofauti katika mitizamo. Ukisema Omutwale ni mfuasi mwadilifu wa Lwakatare na watu fulani hapa JF utakuwa una hoja. Maskini ya Mungu, wala huyo Lwakatare hajawahi na wala hajanikatia kwenye kale ka "Opportunity Cost Tranfer Fee" alikopewa, bali ni ile "extreme affection" niliyowahi kujieleza kuwa nayo kwake mwanzoni kabisa mwa sakata hili. Na huu ni mfano hai kuwaonyesha WaTZ, umaarufu wa Lwakatare si wa chama bali wa kwake yeye kama Lwakatare.
Mkuu Kingwele, nikuandalie Rubisi au utatumia Mramba? Karibu Uhuru platform!
Mkulu, Niko safarini nakwenda Bukoba kwa ajili ya tukio la leo.
Tutakutana Uhuru platform.
Wengi wanashangaa kwa nini kuna shamra shamra za Chadema Bukoba. Lakini wajaribu kuulizia Tambwe alipokelewaje alipokwenda Sisi Maf...... Mi sijali wanasema nini lakini nimelipa nauli ili nikashuhudie nililotamani miaka mingi. Kwamba tunabaki na chama kimoja chenye nguvu cha upinzani Tz.
Kwa taarifa tu kwa wale wasioelewa, kumekuwa na uhusiano mzuri kati ya Lwakatare na Chadema hata alipokuwa bado kafu.
Miaka nenda miaka rudi, ni Chadema hawa hawa huwa wanakuja kumpigia kampeni wakati wa uchaguzi. Nimeshuhudia kwa macho yangu kwa miaka mingi sasa.