Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Ni kawaida wapinzani kuhangaika wala hakuna cha ajabu kwani hana jipya atakalolifanya

wasiwasi wangu na hawa wanasiasa wa 'kisasa' ni kwamba wamekaa kimaslahi zaidi.akiona tu amekosa kanafasi kakula mailage basi anakuwa MBOGO,anaanza kubomoa hoja

Ndiyo yaliyomkuta mate wangu mwita!ukweli mwita hakusoma alama za nyakati!
 
Hivi Tanzania vyama vyetu vina sera mama? Ni vyama vipi ni vya mlengo wa kushoto na vipi kulia? Sijawahi kusikia wakibishana kuhusu sera bali zaidi ni utendaji ( mikataba ya ulaji, takrima n.k.). Naona Zito ameuliza maswali ya msingi lakini kinachokazaniwa ni neno 'ovyo ovyo'! Hakuna mwenye ubavu wa kutueleza ni sera gani zitakazo tutoa hapa tulipo! Ndiyo maana mimi ninavyoona kuna sera mbili tuu; utawala na upinzani. Kwa hali hiyo hakuna tofauti ya msingi kati ya Chadema na CUF kumfanya Lwakatare aonekane msaliti. Wote hawa sera yao ni upinzani; mmoja amejikita kwenye kutetea maslahi ya watu wa bara na mwingine Pemba.

Kama kweli amehama, namtakia kila la kheri huko alikoenda.

Amandla..........
 
Yeyote anahaki na uhuru wa kuhamia chama chochote anachopendezewa nacho. Hata wewe huenda ukahamia chama kingine anytime. Let say upo CCM sasa (ni kwasababu unaridhika na yale inayoyafanya au sababu nyingine). So, sababu hizo zikitoweka utahamia chama kingine.

Mtu anayesema atabakia chama hichohicho hata mambo yaweje huyo anamatatizo ktk mfumo wake wa kutafakari na kutoa maamuzi.
Hiyo siyo kweli Nziku mimi naamini wale wanao hama hama ni watu wenye tamaa na uroho wa madaraka na kujiona wao ni miungu watu never Nziku lazima ukubaliane na maamuzi ya walio wengi
 
Hivi Tanzania vyama vyetu vina sera mama? Ni vyama vipi ni vya mlengo wa kushoto na vipi kulia? Sijawahi kusikia wakibishana kuhusu sera bali zaidi ni utendaji ( mikataba ya ulaji, takrima n.k.). Naona Zito ameuliza maswali ya msingi lakini kinachokazaniwa ni neno 'ovyo ovyo'! Hakuna mwenye ubavu wa kutueleza ni sera gani zitakazo tutoa hapa tulipo! Ndiyo maana mimi ninavyoona kuna sera mbili tuu; utawala na upinzani. Kwa hali hiyo hakuna tofauti ya msingi kati ya Chadema na CUF kumfanya Lwakatare aonekane msaliti. Wote hawa sera yao ni upinzani; mmoja amejikita kwenye kutetea maslahi ya watu wa bara na mwingine Pemba.

Kama kweli amehama, namtakia kila la kheri huko alikoenda.

Amandla..........
Zito kila kitu Zito hana hoja za msingi zaidi ya ubishi usiokuwa na maana na kuta sifa mimi binafsi sijaona hoja anazotoa huyo Zito wenu
 
Hiyo siyo kweli Nziku mimi naamini wale wanao hama hama ni watu wenye tamaa na uroho wa madaraka na kujiona wao ni miungu watu never Nziku lazima ukubaliane na maamuzi ya walio wengi

Mkuu Ipole. Sio kila wakati walio wengi wako sahihi! Wajerumani walimchagua Hitler, chama chake cha National Socialists na sera zake lakini hawakuwa sahihi. Panatakiwa watu wenye ujasiri wa kuweza kusimama kidete kutetea principle zake bila kujali wangapi wako upande wake! Si wote wanaohama wana tamaa, uroho wa madaraka na kujiona mungu mtu kama unavyodhani. Wako lakini si wote.

Amandla........
 
zitto NJAA zimemuandama,alilidhihirisha hili kwenye sakata la dowans
 
Zito kila kitu Zito hana hoja za msingi zaidi ya ubishi usiokuwa na maana na kuta sifa mimi binafsi sijaona hoja anazotoa huyo Zito wenu

Utaonaje ana hoja wakati umeisha mhukumu kuwa ni mbishi tu? Usiangalie mtu bali angalia anachosema na matendo yake. Kutofautiana kisiasa hakina maana ya uadui kiasi kila afanyacho mwenzio unaona kinyaa! Leo Obama anawasifia marais Lincoln na Reagan ambao walikuwa republicans. Wewe unaona tatizo gani kuziangalia kwa undani zaidi hoja za Zitto Kabwe? Au unaogopa kugeuka mlingoti wa chumvi?

Amandla.......
 
zitto NJAA zimemuandama,alilidhihirisha hili kwenye sakata la dowans

Kwa hiyo kwa sababu aliteleza mara moja basi kila asemacho kimekuwa ovyo? Si mnamtupa mtoto na maji mliomuogeshea!

Amandla......
 
Upinzani bado ni mchanga hivyo lazima kuwe na harakati nyinge tena nyingine tata kuuimarisha. I think it's a right move.
 
Kwa hiyo kwa sababu aliteleza mara moja basi kila asemacho kimekuwa ovyo? Si mnamtupa mtoto na maji mliomuogeshea!

Amandla......

kwa level aliyofikia kisiasa,na kwa namna watanzania wengi walivyoweka imani kwake...............!kwahili moja unaloita 'kuteleza',zitto namshauri AACHANE NA SIASA.

amepoteza ladha!the guy is tasteless men!and so does mwita!,lwakatare,and the likes.they have that spirit of SELFISHNESS,an enterpreneuer character.

Kuna wakati huwa namkubali sana NAPE!hakutetereka
 
hao madogo ni wachumia tumbo tu a.k.a waganga njaa na sio wanasiasa.
 
kwa level aliyofikia kisiasa,na kwa namna watanzania wengi walivyoweka imani kwake...............!kwahili moja unaloita 'kuteleza',zitto namshauri AACHANE NA SIASA.

amepoteza ladha!the guy is tasteless men!and so does mwita!,lwakatare,and the likes.they have that spirit of SELFISHNESS,an enterpreneuer character.

Kuna wakati huwa namkubali sana NAPE!hakutetereka

Kwa hiyo unaona entrepreneurship ni dhambi? Kwa mtaji huu hatutafika kokote!

Amandla.........
 
Haya bwana Lwakatare tunakutakia kila la heri. Hili tulishaliona kabisa linakuja. Sasa zile barua za CUF walizosambaza mawilayani kumkataza asifanye mkutano kwa jina la chama.....
 
Huyo Kitila "kachanganyikiwa" na masuala ya Housegirl wake sasa anamwaga utumbo tu
Yego Masatu,
Simple minds zako zinajadili watu badala ya hoja.
Mkuu unajushushia hadhi hapa, pamoja na heshima kubwa tunayokupatia.
Ungelikuwa unasoma hoja usingekuja na old fasion issue maana alishaitolea majibu yanayoeleweka. Njoo na hoja hapa.
 
Huyu Lwakatare ni narcissist kumshinda Mrema, we utaona tu.
 
kwa level aliyofikia kisiasa,na kwa namna watanzania wengi walivyoweka imani kwake...............!kwahili moja unaloita 'kuteleza',zitto namshauri AACHANE NA SIASA.

amepoteza ladha!the guy is tasteless men!and so does mwita!,lwakatare,and the likes.they have that spirit of SELFISHNESS,an enterpreneuer character.

Kuna wakati huwa namkubali sana NAPE!hakutetereka

Ukimnyooshea mwenzio kidole kimoja, vinne vinakugeukia wewe, Si afadhai hata huyo Zitto kathubutu? wewe je? nyuma ya keyboard?

Bravo Zitto, songa mbele wala usirudi nyuma!
 
Kwa hiyo unaona entrepreneurship ni dhambi? Kwa mtaji huu hatutafika kokote!

Amandla.........

sio dhambi,lakini isichanganywe na 'siasa'!ikulu,au bungeni HAKUNA BIASHARA!ukileta tamaa za fedha utamisuse hela ya walipa kodi.impact ya tamaa na mtizamo wa kujilimbikizia fedha ndio uliozaa kashfa zote ambazo kila mwanaharakati analia nazo sasa

we need 'a new nyerere'
we need a leader
we need 'a new mandela'
we need a leader
 
Nakumbuka msaji wa kwanza wa vyama vya siasa Bw. George Liundi, aliwahi kunukuliwa akisema aliwajua fika wanasiasa waliopandikizwa katika vyama vya upinzani kwa maksudi ya kuvivuruga. Nafikiri ndo akina hawa Lwaks na wenzake watafuatia tu, ngojeni.
Hapa mtasema mengi amabayo hayakuwahi kutoka midomoni mwenu, lakini Lwaks huyooooooooooooooo chadema. Mnayodhani kuwa yatakuwa maafa kumbe itakuwa baraka.
 
Back
Top Bottom