Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Uamuzi wa mtu fulani kuhama chama cha siasa ni haki yake ya msingi na ipo ndani ya katiba,lkn sikubaliani na repercussion ambayo inatolewa na wanasiasa wengi nyumbani tz eti ndiyo sababu iliyomsukuma kuhama chama fulani!
Lwakatare umesema tu kuwa CUF walikuwa wanakulipa laki 3 lkn hujaeleza maombi yako wewe ndani ya CUF kimshahara ilikuwa unataka kulipwa bei gani?Wala hujasema CHADEMA wamekuambia watakulipa bei gani?Typical no sense claim from one of highly regarded and respected opposition icon in tz.
Anyways,ni wakati sasa mzuri kwa CUF kuwaeleza watz wataziba vipi pengo la kisiasa kule Bukoba!
 
Huyu Lwakatare atakuja kuwaletea shida sana CHADEMA, mark my words.
Mkuu Bluray,
Ungesoma maelezo vizuri ya Omtwale unaweza kubaini style ya uongozi wa CUF ni watu 3.Ukija upande wa CHADEMA maamuzi yao ni shirikishi,yaani viongozi wa juu hawana ukiritimba wanapenda maamuzi ya pamoja.Dhana hii ya uongozi ndiyo iliyomvutia Lwakatale kujiunga,ili aweze kutumia kipawa chake sawasawa kujenga jamii ya Kitanzania ambayo itajiamini na kushiriki kikamilifu katika kuliendeleza Taifa letu katika maendeleo endelevu.
Kule CUF wenye maamuzi ni Seif,Duni na Lipumba,wengine wanatakiwa kufuata maelekezo sahihi ya vinara hao!Kule CHADEMA hoja sahihi ndiyo kitu cha msingi sio nafasi aliyonayo mtoa hoja.
 
kuna mwingine alikuwapo kwenye mkutano atujuze kama 300,000 ndiyo sababu ya msingi??
 
Uamuzi wa mtu fulani kuhama chama cha siasa ni haki yake ya msingi na ipo ndani ya katiba,lkn sikubaliani na repercussion ambayo inatolewa na wanasiasa wengi nyumbani tz eti ndiyo sababu iliyomsukuma kuhama chama fulani!
Lwakatare umesema tu kuwa CUF walikuwa wanakulipa laki 3 lkn hujaeleza maombi yako wewe ndani ya CUF kimshahara ilikuwa unataka kulipwa bei gani?Wala hujasema CHADEMA wamekuambia watakulipa bei gani?Typical no sense claim from one of highly regarded and respected opposition icon in tz.
Anyways,ni wakati sasa mzuri kwa CUF kuwaeleza watz wataziba vipi pengo la kisiasa kule Bukoba!

Unataka kutueleza kwamba CUF haina kiwango cha nafasi aliyokuwa nayo Lwakatare ilipwe kiasi gani? Kwa maani hiyo anatakayeziba pengo lake ajichagulie mshiko wake.

Basi msiwapigie kelele wabunge wa sasa kudai mishiko ya millioni kumi kwa sababu wa zamani hawakuipata kama Lwakatare alivyokosa mshoki CUF.

Mzee, tuletee hoja hapa umejibu "hovyohovyo"!
 
kuna mwingine alikuwapo kwenye mkutano atujuze kama 300,000 ndiyo sababu ya msingi??
Yeah, mleta mada naye huenda alipokuwa anapitapita (kama alivyojieleza) maybe alikuta anazungumzia salary. Na pengine mleta mada hakuendelea kukaa kwenye mkutano kwa sababu zake za kikazi (kama alivyojieleza as well).
 
Uamuzi wa mtu fulani kuhama chama cha siasa ni haki yake ya msingi na ipo ndani ya katiba,lkn sikubaliani na repercussion ambayo inatolewa na wanasiasa wengi nyumbani tz eti ndiyo sababu iliyomsukuma kuhama chama fulani!
Lwakatare umesema tu kuwa CUF walikuwa wanakulipa laki 3 lkn hujaeleza maombi yako wewe ndani ya CUF kimshahara ilikuwa unataka kulipwa bei gani?Wala hujasema CHADEMA wamekuambia watakulipa bei gani?Typical no sense claim from one of highly regarded and respected opposition icon in tz.
Anyways,ni wakati sasa mzuri kwa CUF kuwaeleza watz wataziba vipi pengo la kisiasa kule Bukoba!

Mkuu Malafyale,
Huyo mleta mada amechagua kipengele kimoja tu alichozungumza Lwakatale.Mimi ninachoelewa alikuwa anatoa maelezo ya uongozi ni kujitolea na ndio maana alikuwa anapokea mshahara wa Sh.300,000/= kwa mwezi.Naomaba watanzania msimuwekee mawazo yenu akilini kwake.Mimi nimefarijika kuwa bado huyu mtu yuko upinzani amebadilisha timu tu.Malengo yake na yale ya CUF kuitoa CCM ambayo ndiyo ya msingi yapo palepale.Mbona tukio hili siyo mara ya kwanza kutokea kuna kipindi msaidizi wa Mbatia,Bw. Nyambabe aligombea kule Serengeti kwa tiketi ya CUF mbona NCCR-Mageuzi hawakupiga kelele?Mwingine ni Akwilombe alihamia CHADEMA akitokea CUF,sikusikia kelele kwa nini hii ya Lwakatale inaleta zogo?
 
Mkuu Bluray,
Ungesoma maelezo vizuri ya Omtwale unaweza kubaini style ya uongozi wa CUF ni watu 3.Ukija upande wa CHADEMA maamuzi yao ni shirikishi,yaani viongozi wa juu hawana ukiritimba wanapenda maamuzi ya pamoja.Dhana hii ya uongozi ndiyo iliyomvutia Lwakatale kujiunga,ili aweze kutumia kipawa chake sawasawa kujenga jamii ya Kitanzania ambayo itajiamini na kushiriki kikamilifu katika kuliendeleza Taifa letu katika maendeleo endelevu.
Kule CUF wenye maamuzi ni Seif,Duni na Lipumba,wengine wanatakiwa kufuata maelekezo sahihi ya vinara hao!Kule CHADEMA hoja sahihi ndiyo kitu cha msingi sio nafasi aliyonayo mtoa hoja.

Kwa mfumo huo hakuna haja ya kuwa na kiongozi maana hata mnapoelekea vitani basi anetakiwa kufuatwa amri zake ni platuni kamanda ,sasa kama maamuzi yanatakiwa yawe shirikishi kutapatikana vurugu mechi ndipo pale tulipoona Slaa kasema tusinunue Zito kasema tununue ,au umesahau ule mshike mshike wa generator za umeme.
 
Mkuu Malafyale,
Huyo mleta mada amechagua kipengele kimoja tu alichozungumza Lwakatale.Mimi ninachoelewa alikuwa anatoa maelezo ya uongozi ni kujitolea na ndio maana alikuwa anapokea mshahara wa Sh.300,000/= kwa mwezi.Naomaba watanzania msimuwekee mawazo yenu akilini kwake.
Kama angekuwa na lengo la kutaka kuonyesha kuwa alikuwa anajitolea, asingelinganisha hizo laki 3 na laki 8 anazozipata hivi sasa kwa kuuza maparachichi
 
Kama ameingia Chadema na halipwi hata hiyo laki tatu bali anafanya kwa kujitolea akitegemea hiyo laki nane ya maparachichi ni sawa na mtu ambaye anatengeneza mamilioni kwenye biashara yake na bado anataka kuingia CCM ili apate mamilioni zaidi? Na ni nani ndani ya CCM katika ngazi za juu ambaye anafanya shughuli zake kwa kujitolea?

As a matter of fact, ukifikiria sana utaona kuwa kama tatizo lake lilikuwa ni fedha, Chadema is the wrong party to join. He had more to gain with CCM than with Chadema. Think about it.
 
Cha Msingi hapa ni Kubaki Upinzani na Siyo CCM!! Awe analipwa milioni 3 au Shilingi 50 elfu au Laki 3 siyo sababu ni Upinzania wa maana katika Taifa maana ukiwa na Vyama Legelege na Serikali pia huwa na maamuzi dhaifu sana katika mambo ya mSingi, Kwa hiyo kulipwa kiduchi siyo shida sana
 
Kaka Yangu Mzee Mwanakijji, Kama amekwenda huko kwa ajili ya pesa basi atakuja kuondoka au kwenda CCM, maana ukitazama huyu mwandishi kiini cha kuandika ni kusema kuwa Lwakatare ameamua kwenda CHADEMA kwasababu CUF alikuwa anapewa Pesa Kiduchu sana, Hapa ni lazima tusubiri maana inawezekana akasosa ubunge na Kurudi CCM kabisa
 
kumbuka hiyo ndiyo tafsiri ya aliyetundika hii habari; siyo maneno ya Lwakatare mwenyewe. Tumsubiri Lwakatare mwenyewe aseme ni kwanini amejiunga na Chadema na kama malipo kidogo toka CUF ni sababu.
 
Pamoja na kwamba sioni sababu ya ku-question nia yake ambayo ameitimiza kwa kuhamia chama kingine, naona haikuwa vyema kwake kusema alikuwa akilipwa kiasi gani na CUF. Masuala ya mshahara ni makubaliano yake na chama alichokuwepo. Na ni masualaya kibinafsi sana. Kinachotakiwa ni sababu za kuhama, na kuhamia CHADEMA, nia ya kuendeleza upinzani wa kidemokrasia na mikakati aliyonayo ya kisiasa baada ya kuondoka CUF.

Kuweza kupata wanachama wa CUF wenye nia ya kuhama nae ni hatua muhimu sana pia. Kwani anaingiza mtaji mpya kwenye chama chake kipya. Ila anatakiwa kuahidi kushirikiana na chama chake kipya na kujifunza imani zao, malengo yao na kupania kukiimarisha zaidi kwa kushirikiana na wenzake aliowakuta huko.

Siasa za upinzani Tanzania ni ngumu sana. Inabidi tumuelewe tu ndugu yetu huyo kwamba amebidi kuhama na zaidi ametumia haki yake kufanya hivyo. Tuheshimu maamuzi hayo, kwani kufanya hivyo ni kumtendea haki. Hakuna haja ya mtu kubaki sehemu moja ambayo una uhakika kuwa hutaweza kutoa mchango wowote kwa haki, na uhuru. Hasa baada ya kutokea yaliyotokea.

Kila binadamu hupenda challenges. Bila challenges maisha yanakuwa boring. Hivyo kuhama kwa Lwakatare inaweza kuwa ni challenge kwake, ni kwa manufaa yake kabla hayajawa manufaa kwa mwingine yeyote.
 
Kwa mfumo huo hakuna haja ya kuwa na kiongozi maana hata mnapoelekea vitani basi anetakiwa kufuatwa amri zake ni platuni kamanda ,sasa kama maamuzi yanatakiwa yawe shirikishi kutapatikana vurugu mechi ndipo pale tulipoona Slaa kasema tusinunue Zito kasema tununue ,au umesahau ule mshike mshike wa generator za umeme.

Mkuu hapa tunaongelea shujaa kuhamisha viwanja, hayo yagenereta yana nafasi yake!

Tangiapo kuwa chama kimoja haina maana kila mtu hana ubongo wake wa kufikiria na kutoa maoni yake! Na kuwa kiongozi haina maana wewe ni
SI unitT ya unao waongoza, lazima uwasikilize maoni yao ndo gurudumu litasonga, huwezi ukawa good leader kwa mtindo wa 'one man show', and for CUF's case 3 man show, never!'
 
Wakuu na wadau hapa naanza kuwasukumia picha na maelezo mengine kuhusu mkutano nitawatumia baadaye. Nimejitahidi nitume picha nyingi ili wadau muamue kwa kuzisoma na kuona nini kimejili Bukoba.
Kwanza kitu kilichonishangaza ni umati huo mkubwa kukaa kwa uvumilivu uwanjani kwa masaa kama matano bila kuchoka wala kukata tamaa.

IMGP2132 i.jpg

IMGP2133 i.jpg
Kulia Ni Mh. Lwakatare, katika Dr Slaa, Kushoto Professor Baregu.

IMGP2136 i.jpg
Wananchi wakisikiliza hotuba mbali mbali za viongozi wa vyama vya siasa Kagera.

IMGP2137 i.jpg

IMGP2138 i.jpg
Mmoja wa viongozi wa CUF Bukoba akitoa hotuba.

IMGP2139 i.jpg
Ndugu Lwakatare akiwa anakwenda jukwaani na Viongozi wengine wa Chadema taifa. Aliyetangulia ni mmoja wa waanzilishi wa Chadema Kagera David Kalikawe(aliyevaa kofia)

IMGP2140 i.jpg
Lwakatare akisalia umati wa wapenzi wake wakati akielekea jukwaani.

IMGP2141 i.jpg
Lwakatale akihutubia wananchi.

IMGP2142 i.jpg

IMGP2143 i.jpg
Umati wa watu ukimsikiliza Lwakatare akitoa hotuba.
 
Kama yuko mwandishi wa gazeti anazihitaji picha kwa ajili ya gazeti anaweza kuni PM nimpe ruhusa ya kuzitumia gazetini.

Bado natayarisha nyingine na nitawasukumia punde.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, nimeelewa kuwa alikuwa anafanya kazi kubwa ambayo haikuwa inalingana na mshahara aliokuwa akipata. Pamoja na hayo ukirejea katika maelezo ya Lwakatare mbele wanachama na viongozi wa CUF wakati akibwaga manyanga, alidai kuwa kulikuwa na watu ambao walikuwa wana kikorosho naye. Na still hawaku-appreciate kazi aliyokuwa anafanya kwa ajili ya chama cha CUF.

Hata hivyo Bw. Lipumba alikuja kutoa appreciation kupitia magazeti kuhusu utendaji wa Bw. Lwakatare.
Kwa msingi huo sidhani kama Lwakatare kahamia CHADEMA kupata mshiko zaidi ila kutoa mchango wake kwa CHADEMA. Na kwa uungwana CHADEMA watakuwa responsible kumlipa kama wakimpa ajira, unless Lwakatare mwenyewe akatae kulipwa mshahara. Si lazima uwe zaidi ya Tsh. 300,000, unaweza ukawa chini ya hapo as long as kuna makubaliano ikiwa ni pamoja na appreciation kutoka kwa chama pamoja na wanachama kuhusu utendaji wa Bw. Lwakatare katika chama.
 
Mkuu hapa tunaongelea shujaa kuhamisha viwanja, hayo yagenereta yana nafasi yake!

Tangiapo kuwa chama kimoja haina maana kila mtu hana ubongo wake wa kufikiria na kutoa maoni yake! Na kuwa kiongozi haina maana wewe ni
SI unitT ya unao waongoza, lazima uwasikilize maoni yao ndo gurudumu litasonga, huwezi ukawa good leader kwa mtindo wa 'one man show', and for CUF's case 3 man show, never!'

Hamna cha kuhamisha viwanja CUF haiongozwi na watu watatu kama unavyotaka tuamini,kile ni Chama Cha Wananchi ,wao ndio wadau ,sasa kama kulikuwa na wafuasi wa Lwakatare ndio hao umeona wamemfuata ila kama kulikuwa na wapambanaji wanaokiunga mkono Chama Chao wao watabakia na kuendeleza mapambano hadi kieleweke,hawatobabaika na kiongozi kuhama Chama ,hata Seifu au Lipumba wakibwaga manyanga basi wapo watakaozuka na kusimamisha bendera ya CUF ,maana Lwakatare huwezi kumpambanisha na Shaibu Akwilombe kwa wanaomfahamu ameondoka CUF kumezuka wepya.
Hata hivyo CUF kama Chama haina nafasi na wanaotetereka ambao utendaji wao unawalakin kama huyo Lwakatale ,na zaidi ni kwa wananchi wa upande wa bara (Tanganyika) msimamo wao unaeleweka vizuri sana na WaZanzibari wanawaelewa wenzao wa Tanganyika ,kwa hivyo nataka unielewe kuwa msimamo wa wananchi wa Zanzibar si kwa viongozi bali ni kuikataa CCM ,kama huelewi wananchi waZanzibar wanawaelewa viongozi wao na wanawafuatilia ,inawezekana huelewi kinachoendelea ,kwa kukukatiza tu kuna viongozi wengi wa CUF upande wa Pemba (Wawakilishi na wabunge)wameshanunuliwa na habari zimeshafika makao makuu na zinafanyiwa kazi,haina haja ya kumwaga mtama hapa .dont play with CUF security ni hatari sana,kuna yule muwakilishi wa Magogoni ,kesi yake sijui kama uliisikia ,yule aliitwa na Karume Ikulu ,aliporudi tu akelezwa yote aliyopatana ,ila CUF wanajua kuplay political games international wakamuachia kwani lengo lao sio kushinda kile kiti bali walitazama mbele zaidi ya kitakachojiri ambacho kimewaangusha CCM japo hilo jimbo walishinda.Na hivyo kilichomuondoa Lwakatare kinajulikana na kosa alilolifanya linajulikana na yeye mwenyewe analijua ,sasa huko Chadema ndio amekwenda na ameondoka na wengine pamoja na wafuasi,unaweza kuona kama CUF imepata hasara lakini kwa interest za Chama hakuna hasara ila ni faida katika kukijenga Chama ,sasa nakupa mtihani katafute Lwakatare alifanya nini na ni kipi kilichomuangusha katika siasa za CUF.
Na pia uelewe kuwa CUF bado ni Chama kichanga ambacho kimo katika kujijenga na CCM wanakielewa sana ,na zaidi CCM wanaitolea salute security ya CUF na wanaiogopa sana,usalama wa Taifa umegonga mwamba katika kuifuatilia Core system ya security ya CUF.Hivyo usishangilie sana ,mambo ya siasa hayataki papo kwa papo,weka masikio wazi baada ya miezi sita,kwa kukumegea tu Pemba inatutoka ?
 
Back
Top Bottom