Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Kama haitachachawa profesa anapiga kelele ya nini? Kisha teka viongozi wangapi -- wale wa maana kutoka CCM au Chadema? Chama chake ni kukimbiwa tu na viongozi na anashindwa kunasa hata mmoja kutoka kwingine. Why should it be one way traffic?
 
Eeh...hawatachachawa vipi.....kwa mujibu wa mkuu Omtwale.....baadhi ya viongozi wa CUF walienda kumuona babake na Lwakatare kumwomba amsihi mtoto wake asiihame CUF.....sasa huko si kuchachawa?
 
Ama kweli ukiwa mwalimu mchumi ni bora ubakie ktk kazi unayoijua vizuri.. sasa huyu Lipumba anachojaribu kusema ni kipi hapa?..Unataka kuimarisha Chama Bukoba kisha unamwondoa mtu ambaye kafanya kazi yake vizuri kitaifa na huko Bukoba, matokeo yake chama kimemomonyoka huko Bukoba..

Ni ishara zipi za wakati wake yeye kung'atuka! Ni kina nani ambao wako responsible na Uteuzi wa nafasi zao (yeye na Maalim) ktk nyadhifa walizoshika maanake anajigonga kichizi..Uteuzi unaoliondoa jina la aliyekuwa naibu katibu hauwezi kuwepo bila sababu za msingi hasa pale anaposisitiza Lwakatare kafanya kazi yake vizuri tu na ati sababu kubwa ni kukiimarisha chama Bukoba..wamekiimarisha vipi chama kama sii kuzua ugonvi na haya yote yasingetokea kama Lwakatare angebakia ktk majina ya uteuzi na akaja shindwa ktk uchaguzi..Wajumbe ndio sikio la chama ikiwa mtu hafai wajumbe hawataweza kumpakura hata kidogo..
It seems kuwa jamaa alikuwa nakitishia kiti cha Mw'kiti, wakaamua kufanya "conditional dismissal" mapema.
 
Lwakatare ni loser tu acheni aende kwa wachovu wenzio huko Chadema. CUF walikuwepo akina Mapalala, Nyaruba, Akwilombe, Hiza, Msafiri nk wameondoka na CUF bdo ngangari.

Lwakatare ni opportunist tu na kwa uchovu wa vyama vyetu atatengezewa cheo huko chadema nako atavurunda na his final destination ni CCM

Mark my words...
ww umenena.
 
...Chama chake ni kukimbiwa tu na viongozi na anashindwa kunasa hata mmoja kutoka kwingine. Why should it be one way traffic?
ukiona hivyo ujuwe chama chake kipo imara na hakitetereki kwa kumbiwa na mwanachama yeyote, kuna vyama hapa vimekwisha kwa kukimbiwa na mwanachama mmoja tu, wangapi CUF wametoka na bado ipo ngangariii.
 
Sasa kama aliona jamaa wanamzibia njia kwa nini asiende/asihamie chama kingine? Most of us we are after green pasture in one way or another.
 
Lipumba na Maalim wamekuwepo kwenye uongozi wa CUF tokea 1994. Wamegombea mwaka 1995, 2000, 2005. Wakubali tu wao ni vign'ang'anizi kama wengine. Wenzetu wengine ukishindwa chaguzi moja tu basi mtu unajiuzulu kwenye uongozi na mtu kupewa ugombea hata mara mbili ni kazi kweli. Sasa watu wapo kwenye madaraka ya chama kwa miaka 15 anasema siyo ving'ang'anizi? Wakubali tu wanataka hayo madaraka.
waingie bungeni kama kweli wanapenda nchi waachane na uraisi kwani bado safari ndefu inaonekana.waingie bungeni tuone mapamabano yao .sio kubwabwaja tu kila siku majukwaani wakitoka hapo wanaenda kunywa chai na RA LOL.
 
Sasa kama aliona jamaa wanamzibia njia kwa nini asiende/asihamie chama kingine? Most of us we are after green pasture in one way or another.

in politics WE DON'T NEED PEOPLE OF YOUR CHARACTER,consider the bolded part please!

We need someone clean,someone a saint,we need the new nyerere!watu wa mlengo wako napenda kuwashauri waachane na siasa!waende kariakoo pale na mitaji yao wataendesha tu ESCALAT
 
CUF wamefanya technical mistake ya kisiasa. Ukimuuliza mkuu wa Kaya atakuambia wamepata ajali ya kisiasa. Kama kweli Lwakatare alikuwa mchapakazi na amekisaidia chama chake kukua kiasi hicho, kwanini wanamuondoa kwa kikao cha watu wachache (wasiozidi 3)? Kitendo cha wao kumtoa katika orodha ya wagombea bila sababu za msingi na pia kusambaza taarifa kuwa anapenda pesa (kisa kudai pesa anazostahili kutoka kwenye chama) ni udhalilishaji ambao si rahisi kwa mtu wa kawaida kuuvumilia.

Hatima ya mwanasiasa yeyote iko kwenye chaguzi huru na za haki. Lakini pia, iko juu yake binafsi. Haiwezi kuwa kosa kwa mwanasiasa kutoka kwenye chama ambacho ameona hakimtendei haki, eti kwasababu akifanya hivyo ataonekana ana njaa. Njaa kubwa kwa binadamu mwenye hekima na ustaarabu ni kulinda heshima na haki yake na jamii yake. Lwakatare anayo kila sababu ya kuamua kubaki au kuhama chama kwani hiyo ni haki yake na uhuru wake mwenyewe.

CUF na vyama vingi vingine hudhani kuwa kila wanapokosea na wananchama wao kukimbia, wanakuwa wamefanyiwa hila. Hila moja kubwa wameifanya wao wenyewe. Siasa inahitaji umakini wa kusoma alama za nyakati. Kiongozi akiweka ubinafsi kwenye siasa, na maamuzi ya kiuongozi, lazima ataharibu tu. Hilo ndilo linalowatokea CUF sasa. Wanaanza kuhofu kupoteza wanachama wake wachache waliobaki.
 
waingie bungeni kama kweli wanapenda nchi waachane na uraisi kwani bado safari ndefu inaonekana.waingie bungeni tuone mapamabano yao .sio kubwabwaja tu kila siku majukwaani wakitoka hapo wanaenda kunywa chai na RA LOL.

Mkuu you are right. Nafasi ya kushinda uraisi hawa ni mdogo tukatae tukubali that is reality. Wagombee ubunge waka pambane nao from the inside. Wabunge wachache tu wamelete mabadiliko makubwa kama skendo mbali mbali kuibuliwa nk. Siyo lazima wang'an'gane uraisi tu.
 
Mtaji wa mwanasiasa yeyote makini ni jukwaa la kufanya siasa. Unapomnyang'anya mwanasiasa jukwaa ni sawa na kumnyang'anya askari silaha akiwa vitani. Walichofanya CUF ni kumnyang'anya Lwakatare jukwaa ili asifanye siasa; asingekubali. Watajilaumu milele kwa uamuzi wao huo.

Halafu kumfananisha Lwakatare na Hiza au Akwilombe ni makosa. Lwakatare alikuwa na faida mbili kubwa kwa CUF. Mosi, alikuwa anaisimika CUF huko Bukoba. Ukiongea na watu wengi wa Bukoba wanasema wazi kuwa anayependwa kule ni Lwakatare, sio CUF. Ndio kusema kuondoka kwa Lwakatare CUF ni kuiondoa CUF Bukoba. Pili, Lwakatare ndiye aliyekuwa anawasaidia CUF kuua dhana ya kuwa ni chama cha udini. Kuondoka kwake kunaihuisha na kuiimarisha dhana hii. Hizi ni sifa ambazo Akwilombe na Hiza hawakuwa nazo. Kwa hiyo kulinganisha kuondoka kwa Lwakatare na akina Hiza ni njia nzuri kujiridhisha kisiasa, lakini ukweli ni kwamba athari zao kwa CUF hazifanani hata kidogo. Tusubiri tuone.

Ni matumaini yangu kuwa CUF walipiga mahesabu yao vizuri na wakaona kutoka kwa Lwakatare hakungeleta madhara makubwa kisiasa. Vinginevyo, wajue huu ndio mwanzo wa mwisho wa chama chao bara. By the way, kwa muda mrefu tumelilia kubaki na vyama viwili tu, sasa coincidentally ndiyo hivyo tuna vyama viwili rasmi, tushindwe sisi!
 
Ohooo...Kitila...ulikuwa wapi? Maana tumekutafuta weeee.....lakini wapi....
 
Kitila, tunakusubiri kule kwenye complains kuhusu topic ya kuwa ulimkamua house girl wako.

Kabla hujaleta blah blah za CUF na udini uje utuweke sawa kule kuhusu tuhuma zinazokuhusu mkuu.
 
Kitila, tunakusubiri kule kwenye complains kuhusu topic ya kuwa ulimkamua house girl wako.

Kabla hujaleta blah blah za CUF na udini uje utuweke sawa kule kuhusu tuhuma zinazokuhusu mkuu.

Tayari keshasepa....harudi tena
 
Lwakatare ni loser tu acheni aende kwa wachovu wenzio huko Chadema. CUF walikuwepo akina Mapalala, Nyaruba, Akwilombe, Hiza, Msafiri nk wameondoka na CUF bdo ngangari.

Lwakatare ni opportunist tu na kwa uchovu wa vyama vyetu atatengezewa cheo huko chadema nako atavurunda na his final destination ni CCM

Mark my words...

Mkuu uishi kucheua pumba?
 
ukiona hivyo ujuwe chama chake kipo imara na hakitetereki kwa kumbiwa na mwanachama yeyote, kuna vyama hapa vimekwisha kwa kukimbiwa na mwanachama mmoja tu, wangapi CUF wametoka na bado ipo ngangariii.

Siku nimekuja na breaking news za wananchi wa Bukoba kumtaka ahame kafu, wewe ndiye ulinisakama kuwa mi ni mwongo😀
Leo kwa sababu hii habari kaisema mwenyekiti wako Lipumba, unakuja kutuletea old stories!
Mwaka huu kafu mtaumia sana maana yuko na kiongozi mwengine yuko njiani kuwakimbia pia. Huyo simtaji. Time will tell😀
Sasa kama si maumivu kwenu wewe na Lipumba mbona mnaonyesha ku panic?
Mmeshapigwa bao bwana😀tena la kisigino😀
Kwangu mi sintajali anakwenda chama kipi cha upinzani. Ila ni hamu yangu kuona kafu inakufa mikononi mwa Lipumba na Seif😀
Hata hivyo kwa kuwa wadau wengi wanatamani kuona nchi inakuwa na chama kimoja chenye nguvu cha upinzani, naona ndoto zao zinaelekea kutimia maana kitabaki Chadema. Kafu tlp nccr kwishney😀
Alafu mwambie Lipumba kuwa Bukoba kafu kwishney. Kama ilivyo Pemba kafu bila Seif si kafu ndivyo ilivyo Bukoba kafu bila Lwakat.... si kafu😀
 
Back
Top Bottom