Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Kwa maneno yako Masatu! baada ya wanasiasa wetu kuzunguka koooote huko at lastlazima warudi CCM siyo? kwa maana hiyo hakuna haja ya kuzunguka saana ni bora kubaki tu CCm au?
 
Nakumbuka msaji wa kwanza wa vyama vya siasa Bw. George Liundi, aliwahi kunukuliwa akisema aliwajua fika wanasiasa waliopandikizwa katika vyama vya upinzani kwa maksudi ya kuvivuruga. Nafikiri ndo akina hawa Lwaks na wenzake watafuatia tu, ngojeni.
 
unamaanisha chama cha kaskazini na kile cha majambazi?
 
Siku nimekuja na breaking news za wananchi wa Bukoba kumtaka ahame kafu, wewe ndiye ulinisakama kuwa mi ni mwongo😀
Leo kwa sababu hii habari kaisema mwenyekiti wako Lipumba, unakuja kutuletea old stories!
Mwaka huu kafu mtaumia sana maana yuko na kiongozi mwengine yuko njiani kuwakimbia pia. Huyo simtaji. Time will tell😀
Sasa kama si maumivu kwenu wewe na Lipumba mbona mnaonyesha ku panic?
Mmeshapigwa bao bwana😀tena la kisigino😀
Kwangu mi sintajali anakwenda chama kipi cha upinzani. Ila ni hamu yangu kuona kafu inakufa mikononi mwa Lipumba na Seif😀
Hata hivyo kwa kuwa wadau wengi wanatamani kuona nchi inakuwa na chama kimoja chenye nguvu cha upinzani, naona ndoto zao zinaelekea kutimia maana kitabaki Chadema. Kafu tlp nccr kwishney😀
Alafu mwambie Lipumba kuwa Bukoba kafu kwishney. Kama ilivyo Pemba kafu bila Seif si kafu ndivyo ilivyo Bukoba kafu bila Lwakat.... si kafu😀
kwani ww ni wa kaskazi au ni wale walio wengi mjengoni?Mbona ueleweki?
 
unamaanisha chama cha kaskazini na kile cha majambazi?

Amosam na wengine wote,

Naomba mupokee angalizo hili; nilipotumia "Wajumbe wa Kaskazini" sikumaanisha eneo katika nchi ya Tanzania wala kabila. Nilitaka kutumia fasihi ya Kusadikika. Kama umewahi kusoma hiki kitabu utakuwa umenielewa au kama bado nikumegee kidogo, watakaokuja kuleta chama BK wanakuja kwa staili ya Mjumbe wa Kaskazini ndani ya Kusadikika
 
In reality CUF wanapita katika moja ya vipindi vigumu mno tokea kuanzishwa kwao kwenye miaka ya 90 mwanzoni.....

Nakumbuka zama zakuondolowa Mapalala mmoja kati ya waanzilishi wa mwanzo mwanzo kabisa wa CUF.... nakumbuka nusura pachimbike maana influence ya jamaa na uasisi wake kiasi vilileta mtikisiko kenye kambi ya CUF. Lakini what happened kila mtu anajuwa waliweza ku recover sana na hatimaye kujijenga.

Namkumbuka sana Maiko Nyaruba..jamaa alikuwa muongeaji hana mfano na naamini ali wa influence watu wengi mno kujiunga na CUF lakini yakamkuta yaliyomkuta.

Then ustadhi wangu Salim Msabbah yule aliyekuwa mbunge wa jimbo la mtendeni...very influential..na bright mno....nae aliondoka......Naila Jidawi, Akwilombe, e.t.c

The list is endless... ila waliweza kurecover huko nyuma.... Wilfred Lwakatare mmoja kati ya vijana tena wasomi mno ambao uwepo kwake CUF ulikuwa ni muhimu mno..angeweza kuvutia vijana wenzake na wasomi wenzake kujiunga na CUF.

CUF inavyoenekana haina mvuto na vijana wasomi unlike CHADEMA.. sababu hazijulikani whether hawaoewi nafasi za uongozi au vipi.... Nimeipenda mno approach ya CHADEMA ya kuwapa vijana nafasi za uongozi na mamuzi katka chama. Mwenyekiti wao ni kijana, then kina Kabwe and his co.

Naamini CUF bado ina hazina ya wanachama wengi mno Tanzania...na I will eat my words wanaweza wasipate mmbunge bara..lakini overall mgombea wa uraisi akawa next to wa CCM. Sababu nadhani wengi wa wanachama wao have something in common between them.

Kingwele.
 
Kama CUF haichachawi kwa nini anayasema haya yote? asingeyasema haya yote basi ndio tujue CUF haichachawi; ila debe tupu halikosi kuvuma; ngoja tuone mwisho wake maana mwanzo wa ngoma ni lele
 
Give me a break! hayo mambo ya ku bandwagon kampeni za CCM. Kwa hiyo Chadema nayo ni ya wachaga? Mbona hiyo nafasi ya Lwakatare kaingia somebody Joram i hope sio muislam!

Huyo Kitila "kachanganyikiwa" na masuala ya Housegirl wake sasa anamwaga utumbo tu

Masatu, unaelewa lakini maana ya neno dhana? Au unataka kutuambia kuwa hakuna wenye imani hizo za CUF kuwa chama cha waislamu na Chadema cha wachaga? Au unadhani kukataa kuziona ndiyo zitapotea? Sasa mbona una-hope Joram sio muislamu?

Amandla..........
 
Kwa maneno yako Masatu! baada ya wanasiasa wetu kuzunguka koooote huko at lastlazima warudi CCM siyo? kwa maana hiyo hakuna haja ya kuzunguka saana ni bora kubaki tu CCm au?

Yap yap yap! ebwana we!!
 
Masatu, unaelewa lakini maana ya neno dhana? Au unataka kutuambia kuwa hakuna wenye imani hizo za CUF kuwa chama cha waislamu na Chadema cha wachaga? Au unadhani kukataa kuziona ndiyo zitapotea? Sasa mbona una-hope Joram sio muislamu?

Amandla..........

Fundi,

Ungerudi nyuma kidogo mjadala ulipo anza. Hoja yako imejikita kwenye kichwa cha habari cha thread. Ndio nikasema una bandwagon wimbo wa CCM kwani kama issue ni kuondolewa Lwakatare maybe ni udini aliechukua nafasi yake ni wa dini hiyo hiyo.
 
Masatu,
Ungenisoma vizuri ungejua nilikuwa naunga mkono hoja ya pili ya Kitila Mkumbo. Kwa vile mpaka sasa sijasikia Kitila kuhamia CCm basi pengine ungenishutumu kwa kudandia tela lake na sio la CCM.

Vile vile, ninachozungumzia ni dhana. Kumuondoa mkristu maarufu na mwenye mvuto kama Lwakatare na kumbadilisha na mtu mkristu mwingine ambae hana umaarufu wowote kunawaongezea ammunition wasioitakia mema CUF. Hoja itakuwa ni hatakiwi mmisheni mwenye msimamo kwenye nafasi za juu hata kama pengine huyo Joram ni bora kuliko Wilfred! CUF walitakiwa kuwa makini zaidi katika uamuzi wao.

Hata hivyo, it is all good. Hakuna kilichoharibika.

Amandla.......
 
Fundi,

Kama ungenisoma vizuri utagundua nami nilikuwa najadili hoja hiyo hiyo ya Kitila. Na katika majibu yangu ndio likaja hilo suala la madai ya CCM na udini.

Huo mvuto wa Lwakatare hakuja nao CUF bali aliupata CUF. Simjui huyo Joram na uwezo wake lakini mpaka kufikia kupewa wadhifa hao hao waliompa wameona unwezo wake ikiwa pamoja na "mvuto"
 
Fundi,

Kama ungenisoma vizuri utagundua nami nilikuwa najadili hoja hiyo hiyo ya Kitila. Na katika majibu yangu ndio likaja hilo suala la madai ya CCM na udini.

Huo mvuto wa Lwakatare hakuja nao CUF bali aliupata CUF. Simjui huyo Joram na uwezo wake lakini mpaka kufikia kupewa wadhifa hao hao waliompa wameona unwezo wake ikiwa pamoja na "mvuto"

Masatu Mkuu. Hizo hisia za udini zipo bila hata CCM kuhusika. Alichokifanya Kitila ni ku-caution kuwa CUF wawe waangalifu katika maamuzi yao.

Walichokifanya CUF kwa Lwakatare ni kumpa platform ambayo aliitumia vizuri. Si wote wenye uwezo huo. Ingelikuwa hivyo basi huko CUF tungewasikia wengi kuliko Lipumba na Maalim. Mimi binafsi namtakia kila la kheri huyo Joram maana tunahitaji watu wenye msimamo na mvuto katika vyama vya upinzani. Ana kazi nzito mbele yake.

Amandla....
 
Masatu Mkuu. Hizo hisia za udini zipo bila hata CCM kuhusika. Alichokifanya Kitila ni ku-caution kuwa CUF wawe waangalifu katika maamuzi yao.

Walichokifanya CUF kwa Lwakatare ni kumpa platform ambayo aliitumia vizuri. Si wote wenye uwezo huo. Ingelikuwa hivyo basi huko CUF tungewasikia wengi kuliko Lipumba na Maalim. Mimi binafsi namtakia kila la kheri huyo Joram maana tunahitaji watu wenye msimamo na mvuto katika vyama vya upinzani. Ana kazi nzito mbele yake.

Amandla....

Wakuu FM na Mwanawasu Masatu wala msitoane macho.
Pamoja na uwezo, nguvu,umaarufu, uhodari, au sifa yoyote utakayoweza kumpa Lwakatare lakini bado ukweli unasimama kwamba CUF itaendelea kuwepo, kwa suala la kuwa imara kama zamani sina uhakika. Na kwa kuzungumzia bukoba watakuwa wamepoteza wanachama na wafuasi wengi sana, watakaomfuata lwakatare kama ataamua kuhama chama.
Hata hivyo huyo aliyevaa viatu vya Lwakatare sio mtu wa kuwa na mashaka nae. Ni mtu mwenye msimamao thabiti haswaaa.Nilimuona na kumsikiliza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2005 akigombea jimbo la Mikumi na kushindwa na Clement wa ccm, lakini ukweli jamaa anajua kuzungumza, anajua kujenga hoja na kiukweli naamini jamaa anaweza. Joram Bashange aliwahi kuwa katibu wa TPAWU(tawi la kilombero sugar-sasahivi ILLOVO) wakati kiwanda hicho kinabinafsishwa kwa makaburu(ingawa kuna maneno ya chini chini kwamba makaburu walipewa K1 na mzee chenkapa & ze sumaye wakajigawia K2(samahani mzindakaya najua hupendi kuona huyu mzee akitajwa).Huyu bwana Bashange ameacha historia ya kukumbukwa kilombero sugar hadi kesho ukienda utasimuliwa, jinsi alivyokuwa imara kutetea haki za wafanyakazi wa kiwanda kile wakati wa ubinafsishwaji wake. Alipambana na uongozi wa wilaya, mkoa, na polisi kwa hoja kwenye vikao mbalimbali vilivyoitishwa kwa ajili ya kuweka mambo sawa na akawashinda.Inatajwa kuwa sababu mojawapo iliyopelekea Lukuvi kula shavu la uwaziri enzi za chenkapa ni baada ya kumtonya mzee mkapa madudu yaliyokuwa yamefanywa na watendaji kadhaa katika kushughulikia kadhia hiyo akiwemo waziri wa kilimo kipindi hicho mzee kimiti. Matokeo yake kimiti akapotezezewa baada ya uchaguzi mkuu wa 2000.Kumbuka tu kwamba vuguvugu la kubinafsisha kampuni ya kilombero sugar ilikuwa kati ya 1998 hadi 2000.
Nimalizie kwa kusema tu kwamba tumpe muda bw.Bashange tuone ataifanyia nini CUF, BTW bw.Bashange nae ni mtani wangu, dugu moja na Lwakatare (wote ni BK boys).Sasa sijui hapa Lipumba aliendeleza ukabila???!!!!anyway natania tu , turudi kwenye mada.
 
Naamini mimi na Masatu ni watu wazima na tunaweza (kama tunavyofanya) kutofautiana bila kutoana macho. Mbona ishu hii tunajadiliana kwa kuheshimiana tu? Asante kwa taarifa na maelezo yako juu ya Joram. Kama nilivyosema awali, namtakia kila la kheri.

Amandla........
 
Napenda sana unvyosema na kupangilia hoja zako Kaka yangu Kitila. Hivyo ndio ukweli kuwa CUF wanajimaliza mwenyewe, maana nakumbuka kipindi fulani Prof Lipumba alisema CUF hakuna udini na kutaja majina ya Lwakatare, labda waseme kuwa wana ajenda nyingine
 
KWA MUJIBU WA GAZETI LA NIPASHE LA TAR 24/JUNE/2009

Zile tetesi zilizokuwa zikijadiliwa sana hapa jamvini juu ya naibu katibu wa CUF bwana Lwakatare kuhamia CHADEMA zimekuwa si tetesi tena,baada ya mwanasiasa huyo kutua rasmi CHADEMA,na hadi muda huu ni kwamba 'mwanazuoni' huyu yupo biharamulo akikipa nguvu chama chake kipya katika kampeni
 
KWA MUJIBU WA GAZETI LA NIPASHE LA TAR 24/JUNE/2009

Zile tetesi zilizokuwa zikijadiliwa sana hapa jamvini juu ya naibu katibu wa CUF bwana Lwakatare kuhamia CHADEMA zimekuwa si tetesi tena,baada ya mwanasiasa huyo kutua rasmi CHADEMA,na hadi muda huu ni kwamba 'mwanazuoni' huyu yupo biharamulo akikipa nguvu chama chake kipya katika kampeni
Ni kawaida wapinzani kuhangaika wala hakuna cha ajabu kwani hana jipya atakalolifanya
 
Yeyote anahaki na uhuru wa kuhamia chama chochote anachopendezewa nacho. Hata wewe huenda ukahamia chama kingine anytime. Let say upo CCM sasa (ni kwasababu unaridhika na yale inayoyafanya au sababu nyingine). So, sababu hizo zikitoweka utahamia chama kingine.

Mtu anayesema atabakia chama hichohicho hata mambo yaweje huyo anamatatizo ktk mfumo wake wa kutafakari na kutoa maamuzi.
 
Back
Top Bottom