TANZIA Luteni Jenerali Mstaafu, Balozi Martin Mwakalindile afariki dunia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
images (22).jpeg
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Nkunda ametangaza Kifo cha Luteni Jenerali Mstaafu Balozi Martin Mwakalindile kilichoteka Januari 28, 2024 nchini India alikokuwa akitibiwa.

20240130_194424.jpg
20240130_194427.jpg
 
Poleni sana Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki.



Muumba awaangazie katika kipindi hichi kigumu.

Again, Poleni sana.

R.I.P Luteni Jenerali M.Mwakalindile.
 
Wanyakyusa wapo vzr upstairs wamejaa kwnye nyadhifa nyeti...
RIP...sir
Hapana siyo hivyo. Inategemea nani alikuwa sehemu ya maamuzi ya nani awe nani enzi za Mwalimu na kuendelea. Mfano, watu wa Mbeya walijulikana kwa ukabila na tangu enzi hizo apson etc alihakikisha wanyakyusa wanashika hatamu (siyo kuwa na akili). Same kwa makabila mengine yenye mrengo wa kupendeleana kama wachaga, waluguru, wapogoro etc. Hivyo usiseme kabisa eti wana akili bali ni nepotism ndiyo iliwabeba. Ni sawa na watu wa musoma kuwa na wanajeshi wengi ni hivyo hivyo
 
Hata hivyo umri wake ulishakua mkubwa, mm nikiwa form 1Secondary school 1986, yeye alishakuwa Meja General wakati huo walikua 13 na akina Warden, Mayunga, Makame Rashid, Lupogo, Luhanga nk
Gen Warden alikuwa mwenyekiti wa Board Iyunga Tech Secondary

Enzi hizo shule ni fujo fujo ,Mwamba alikuwa akiitwa anatukana matusi vibaya mno na kutishia kuwafyatua bastola watukutu


Ni mjerumani full mikwara pale Sekondari Iyunga Tech Mbeya

Alishafariki lakini

Jamaa alikuwa anapiga mkwara mpaka wanafunzi wanataka kukimbia akiitwa Iyunga Tech kama wanafunzi wanafanya fujo au kudharau walimu

Kuna wakati alikuwa anaenda na Bastola kiunoni enzi hizo alishastaafu jeshi kitambo


Kuna siku kaitwa,Akaomba list ya watukutu wapite mbele akiwa na hasira full kufura ,Akaangalia jina moja akakutana na Sir name la rafiki yake walikuwa wote jeshi na jamaa alikuwa kiburi sana Jeshi

Akamuangalia yule mwamba akasema wewe dogo ni laana maana hata Baba yako alikuwa anaambiwa kuna siku atazaa mtoto kiburi kama yeye hivyo kosa sio lako nampigia simu Baba yako kumkumbusha tabia zake za hovyo na yeye ndie atakuhamishe uondoke hapa shule kabla sijakufukuza
 
Back
Top Bottom