Lusinde: Serikali isifikirie adui ni CHADEMA, ni watendaji!

Lusinde: Serikali isifikirie adui ni CHADEMA, ni watendaji!

alipokuwa anaongea nilitaka kurecord lakini kwa kuwa walikuwa wanapewa dakika5 tu nikashindwa wakati na hangaika kutafuta jinsi ya kurecord naona ccm maji yako shingoni kwa sasa msimamo ulioonekana bunge 2015 ccm itakuwa na kazi sana. Ndio maana mama makinda kaamua wakutane ccm wote naona kuzima makali wa wabunge wa ccm kabla ya kupitisha budget ya maji nje ya hapo itakula kwa Pro. maghembe
 
Mhh! Siku zote alikua wapi huyu mdudu? Kaona dalili sio nzuri! Na bado
 
kweli shetani mbaya sana ..homework yako ni kuchangia namna hii na uyaishi haya maneno then we can trust.. sawa L?
 
Mheshimiwa.

Salaam.

Umechangia vizuri sana leo. Umeonekana kama mheshimiwa hasa na umependeza sana kuitwa mheshimiwa leo. Siku nyingine unakuwaje?

Umechangia vizuri sana. Kwa maneno mazuri, matamu na yenye ukweli kabisa.

Umesema vizuri kuwa kana maji yakitoka mwakani wenzenu yaani Chadema bila bila shaka watasema ni kwa ajili ya kampeni. Ni kweli. Lakini kwa nini umetumia neno "wenzetu" badala ya maneno yako yale machafu ya zamani? Bila shaka umekuwa mtu mzima sana na uheshimiwa unakustahili.

Mwisho. Hivi ni kwa nini hukuogopa kusema kwa ujasiri kuwa huungi mkono hoja? Ujasiri huu umeutoa wapi? Wewe ambaye mwanzoni ulionekana kama bendera fuata upepo? Bila shaka umetambua ukweli kuwa huwi mpinzani kwa ajili ya kusema ukweli. Utakuwa mkweli hata ukiwa ni muumini wa CCM.

Kwa kweli leo umenifirahisha sana leo na mimi NAKUUNGA MKONO.

Hongera Mheshimiwa wetu. 2015 ni wetu.

Tabia ya kiumbe 'panya'huwa anang'ata na kupuliza mpaka uje umstukie keshamaliza kidole.
 
leo kaongea point tangu nilipomjua. ameanza kuepukana na ujuha. unajua mjinga akisemwa sema huwa ana pata akili kwa njia mnunurisho
 
Kuvilaumu vyama vya siasa ilihali havina vyanzo vya fedha kuleta maendeleo ni kosa kubwa sana.

Na kukilaumu chama tawala ilihali hakina ofisi kwenye serikali kuu nalo ni kosa kubwa sana.

Wa kulaumiwa ni watendaji walioaminiwa na kuteuliwa na jamhuri na wao kwa ridhaa yao uwatunuku ndugu zao,jamaa zao na wazazi wao kwenye nafasi nyeti ilihali hawana sifa na uwezo wowote kiutendaji,ni wababaishaji,wabishi,wenye vibuli na dhalau kwa kuzani kuwa wao ndio serikali.

Watumishi wa namna hii hawafai na ndio hao hao wanaokwamisha mipango mingi ya maendeleo ya ujumla kwa watu.

Ni wajibu wetu kuwabaini na ikiwezekana tuiombe serikali ifanye haraka operation maalum ya kuhakiki watumishi wake

kuanzia taaluma zao,uwezo wao wa kuzalisha/tija na uwajibikaji wao kwa wananchi.

Wengi wa watumishi wa umma wanafurahi sana pindi lawama zao zinapotupwa ndani ya chama tawala na mbaya zaidi ndani ya chama tawala hicho mwenye mamlaka juu yao ni Rais pekee (Mteuzi mkuu wa nafasi nyeti za nchi).

Katika hili ni vema tukabadili fikra juu ya nani alaumiwe kwani si chama kinachopelekewa fedha za maendeleo bali watendaji wa serikali ambao hawatekelezi wajibu wao ipasavyo na muda mwingi wao ni kuwaza kula,kunywa na kuvaa vizuri tu.

Kama mnabisha jaribuni kutembelea walau ofisi za chama tawala za matawi muone walivyo choka na wengi wao maisha yao ni ya kuungaunga na kuombaomba kwenye ofisi za umma/serikali.
 
Lusinde huyu huyu bingwa wa matusi?kwani leo alitumia dawa gani kupiga mswaki?
 
Lusinde ni Mnafiki, na msiomjua huyu aligombea ubunge cdm jimbo la mtera 2005 na akaachia njiani hata kabla ya kumaliza kampeni ; mara tukashitukia kapewa ukatibu wa shishiemu Tarime!!!!!!!!!!!!! Fungukeni msimshabikie mzee wa mitusi huyo. Ukiona hivyo ujue mamluki wake wa mtera wamempigia simu na kumjulisha wananchi wamekuchoka ndio anajidai anaigeuka serikali ya mashishiemu. Too late men!!!!!!!!!!!:bounce::bounce:
 
Leo Lusinde anasema bungeni kuwa wabunge na mawaziri waende vijijini kunywa maji ya huko vijijini,anakataa kuunga mkono hoja ya bajeti ya maji. Lusinde ni Mnafiki, na msiomjua huyu aligombea ubunge cdm jimbo la mtera 2005 na akaachia njiani hata kabla ya kumaliza kampeni ; mara tukashitukia kapewa ukatibu wa shishiemu Tarime!!!!!!!!!!!!! Fungukeni msimshabikie mzee wa mitusi huyo. Ukiona hivyo ujue mamluki wake wa mtera wamempigia simu na kumjulisha wananchi wamekuchoka ndio anajidai anaigeuka serikali ya mashishiemu. Too late men!!!!!!!!!!!:rockon:
 
Achaneni na "Bipolar' huyo...labda pengine daktari wake amembadilishia dozi baada ya kuona ile dozi aliyokuwa anatumia mgonjwa wake hapo mwanzo ilikuwa inamsababishia madhara (side effects) mgonjwa wake🙂 teh teh

Hebu wana JF na tumpe siku 90 tuone maendeleo ya hiyo dozi mpya🙂

Angalizo: Nilipoanza kusoma kichwa cha habari nilifikiri alikuwa Job Lusinde (the rtd ambassador) kuuuumbee ni yule kada (Cha Utusi) wa kile Chama ambacho kuwa kwamba.....hapo 2015🙂
 
Siku zote ukiamini akili zako na kuzitumia ipasavyo utafanya vizuri kuliko kuwa mbayuwayu
 
angeunga mkono ungesema hajar amekataa unaleta majungu binadam,yesu alifunga siku arobaini bila kula mkasema hali anapepo alipofungua akala mkasema ni mlafi.kazi kwel2
 
Ukweli wanaujua ni basi tu wanalalia masikio, taratibu wote watanyooka.
 
"Kunguru hafugiki" na "Asili haachi asili yake kamwe". Tumpe muda kama atafuta kauli tu mwenyewe coz hapa anahisi ndo ameongea pumba. Yale ya zamani ndo poit kwake ila nampongeza kwani amejitahidi
 
Tupa kule. Mnafiki sana huyu, jembe aliyebaki ccm ni deo filikunjombe peke yake wengine ni mavuvuzela tu.
 
Back
Top Bottom