Duu kumbe huyu jamaa wakati mwingine aliweka kando itikadi za kisiasa huwa anaongea point.
Kasema - Mawaziri WABUNGE wakitembelea vijiji wapewe maji wanavyokunywa wanakijiji ili wajue shida ya maji vijijini.
Pia kasema CHADEMA sio adui, maadui ni watendaji wa Serikali.
Pia kaponda uchimbaji wa visima kwa gharama kubwa. Kashangaa ilikuwaje Serikali ya Nyerere iliweza kujenga mabwawa na Serikali hii imeshindwa.
Kkamalizia kwa kutounga mkono hoja
Mheshimiwa.
Salaam.
Umechangia vizuri sana leo. Umeonekana kama mheshimiwa hasa na umependeza sana kuitwa mheshimiwa leo. Siku nyingine unakuwaje?
Umechangia vizuri sana. Kwa maneno mazuri, matamu na yenye ukweli kabisa.
Umesema vizuri kuwa kana maji yakitoka mwakani wenzenu yaani Chadema bila bila shaka watasema ni kwa ajili ya kampeni. Ni kweli. Lakini kwa nini umetumia neno "wenzetu" badala ya maneno yako yale machafu ya zamani? Bila shaka umekuwa mtu mzima sana na uheshimiwa unakustahili.
Mwisho. Hivi ni kwa nini hukuogopa kusema kwa ujasiri kuwa huungi mkono hoja? Ujasiri huu umeutoa wapi? Wewe ambaye mwanzoni ulionekana kama bendera fuata upepo? Bila shaka umetambua ukweli kuwa huwi mpinzani kwa ajili ya kusema ukweli. Utakuwa mkweli hata ukiwa ni muumini wa CCM.
Kwa kweli leo umenifirahisha sana leo na mimi NAKUUNGA MKONO.
Hongera Mheshimiwa wetu. 2015 ni wetu.
Leo mchana nimebahatika kumsikia Mh, saana Job Lusinde, akichangia hoja Bungeni kuhusu swala la Maji!
Alisema kwamba swala la Maji ni swala nyeti sana na si la Kisiasa kama ambavyo inachukuliwa!
Aliendelea kusema kwamba kama Wabunge wataendelea kumbana sana Profesa na Dokta, [Nadhani alimaanisha Waziri wa Maji na Naibu wake] itakua sio sahihi!
Japo alisema swala la Maji tusifanye Siasa, hapo hapo akajisahau na kuchomekea eti kua kama swala ni Uprofesa na Udokta, mbona tunao Profesa na Dokta waliogombea Urais mara nyingi na wameshindwa!!
Point ya mwisho aliyoiongea alisema kwamba swala la Maji Waziri ahakikishe wanalishugilikia kwa ukamilifu na kwamba Serikali inaweza ikadhani Adui yake ni CHADEMA, kumbe sio ila Adui ni Matatizo yanayowakabili wananchi!
Baada ya kuongea mambo mengi sana alimalizia kwa kusema Haungi Hoja Mkono!
Huyo ndio Lusinde Mbunge Kijana na Msomi kutoka Jimbo la Mtera!!
Hujui siku hizi ukianza kuropoka kuhusu chadema bila point za msingi wanaweka kambi jimboni mwako? Kauli hii haimuepushi Lusinde na kikombe cha kuporwa jimbo wakati ukifika.
Sijui,lakini napata mashaka kama hatakuja kutengua kauli
mmmmh!! Lusinde? Basi kama ni hivyo sasa akili zimeanza ushirikiano utulie hivyo hivyo zisije zikapangaranyuka tena na siku nyingine utoe mchango mzuri zaidi..
Duu kumbe huyu jamaa wakati mwingine aliweka kando itikadi za kisiasa huwa anaongea point.
Kasema - Mawaziri WABUNGE wakitembelea vijiji wapewe maji wanavyokunywa wanakijiji ili wajue shida ya maji vijijini.
Pia kasema CHADEMA sio adui, maadui ni watendaji wa Serikali.
Pia kaponda uchimbaji wa visima kwa gharama kubwa. Kashangaa ilikuwaje Serikali ya Nyerere iliweza kujenga mabwawa na Serikali hii imeshindwa.
Kkamalizia kwa kutounga mkono hoja
Mheshimiwa.
Salaam.
Umechangia vizuri sana leo. Umeonekana kama mheshimiwa hasa na umependeza sana kuitwa mheshimiwa leo. Siku nyingine unakuwaje?
Umechangia vizuri sana. Kwa maneno mazuri, matamu na yenye ukweli kabisa.
Umesema vizuri kuwa kana maji yakitoka mwakani wenzenu yaani Chadema bila bila shaka watasema ni kwa ajili ya kampeni. Ni kweli. Lakini kwa nini umetumia neno "wenzetu" badala ya maneno yako yale machafu ya zamani? Bila shaka umekuwa mtu mzima sana na uheshimiwa unakustahili.
Mwisho. Hivi ni kwa nini hukuogopa kusema kwa ujasiri kuwa huungi mkono hoja? Ujasiri huu umeutoa wapi? Wewe ambaye mwanzoni ulionekana kama bendera fuata upepo? Bila shaka umetambua ukweli kuwa huwi mpinzani kwa ajili ya kusema ukweli. Utakuwa mkweli hata ukiwa ni muumini wa CCM.
Kwa kweli leo umenifirahisha sana leo na mimi NAKUUNGA MKONO.
Hongera Mheshimiwa wetu. 2015 ni wetu.
humu ndani kuna waswahili ww acha tu,nami nimebak nakenua meno tu,,,,
ila huenda jamaa akili zake zinarandana na muandamo wa mwezi