Lusekelo (Mzee wa Upako) ana mapepo na ni Agent wa Shetani. Ataka oa mke mwingine?

kazi ya mungu ningumu sana nahasa pale unapo taka kufanya kazi ya mungu kwa jeuri yako mungu hakosi kukuumbua naipenda nyimbo moja ya mgogo anasema usipotelee mwisho
 
Imani ni nafsi ya mtu mwenyewe na Mungu wake. Kwenye kiama nasimama mwenyewe kujibu sio fulani
 
Kuoa mke zaidi ya mmoja SIO UZINZI,
Unataka kuniambia leo kati ya Lusekelo na Ibrahim (baba wa Imani) nani MZINZI?
Swali lako mwiba . Watakujibu watasema ooh lile lilikuwa agano la kale. Waulize agano la kale ni biblia au gazeti ?
 
Nafikirib hatujamwelewa mzee wa upako. Alichokuwa anafundisha na changamoto za ndoa na jinsi wake wanavyopaswa kuwatunza waume zao wakijua kuwa waume wanatafutwa. Pili tungepata mahubiri yote ndio tungetoa hukumu ya mahubiri yake sio kipande cha sekunde kadhaa tu.
 

Attachments

  • VID-20161206-WA0053.mp4
    1.5 MB · Views: 24
Nafikirib hatujamwelewa mzee wa upako. Alichokuwa anafundisha na changamoto za ndoa na jinsi wake wanavyopaswa kuwatunza waume zao wakijua kuwa waume wanatafutwa. Pili tungepata mahubiri yote ndio tungetoa hukumu ya mahubiri yake sio kipande cha sekunde kadhaa tu.

Kuwa makini wewe!
 
Vita ya wema na uovu, shetani na mwovu watu wote wako katikati ya vita hii. Aandamwe shetani na sio watu aliwanasa
 
tusidanganyane, hakuna Mwanaume anayeridhika na mke mmoja, kama yupo basi atakuwa "msenge", we are by nature polygamist!ndoa ya mke mmoja sio mpango wa Mungu, ni ubunifu tu wa watu
 
Nmejikuta wakati flan nikitafakari sana matendo ya huyu anayejiita Mchungaji na kugundua ana mapepo na ni mtumishi wa shetani kabisa.

Kitendo cha kusema anamtafuta aliyesema wakristo waoe mke mmoja amhoji tayari anaonesha kuukana ukristo na kujihalalishia uzinzi.

Mungu angetaka adam awe na wake wengi angemtengenezea na mwingine.lakini hakufanya hivyo.kusudio la Mungu lilikuwa mke moja na mume mmoja. Kuhoji uhalali wa neno hilo tayari anaonesha ni mtu aliyekengeuka.

Ndugu huyu anayefahamika kwa majivuno na kiburi kinyume na matendo ya ukristo Yesu aliposema Mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu. Yampasa ajinyenyekeze na kujishusha kama mtoto mdogo.

Lusekelo ambaye ni juz juz tu alikumbwa na kashfa ya ulevi jambo ambalo ni aibu hata kwa mchungaj kusingiziwa. Bado hakuweza kujieleza akaelweka machoni pa watu wa Mungu.

Style yake ya mafundisho imejikita zaidi katika yeye kupokea sadaka na tunaona hata kwnye ibada anavyofurahia kutuzwa pesa. Na hapa ndipo ukristo unapozidi kujidhihilisha kuhusiana na siku za mwisho kutakuwepo na manabii na wa uongo na wachungaj wa aina ya lusekelo.

Haya ni mafundisho ya kishetani kabisa. Tamaa za mwili ndizo zinazoweza mkristo akahoji jambo kama hili.

Yesu anasema mwanaume atamwacha babaye na mamaye naye ataambatana na MKEWE na si WAKEZE. Mathayo 19:3-9

Ukina Mkristo anaanza kutaman yaliyo kwa shetan ujue tayar shetan ameshamkamata. Tuendako usishangae kusikia lusekelo anaruhusu waumini wake kuoa wake zaidi ya mmoja.

Huyu ni pepo anafundisha maagizo ya mapepo
 
Jehova aliruhusu bila pingamizi lolote abraham awe na wake wawili,
jacobo awe na wake wanne,
solomoni wake elfu moja na vimada juu,
hata david nae akaoa wakati keshakua wa kutoa nje kuota jua.
Mimi naona lusekelo yuko sawa
Lilikua agano gani kwenye biblia hayo mambo yalitendeka? Je unajua tofauti ya agano la kale na agano jipya?
 
chapombe,taarifa za uhakika ni kwamba "kawaka"

na pia kajenga kajumba ambako hukaa mpaka asubuhi
 
Mzee wa Upako ni mchungaji kama walivyo wengne..!! Na ni binadamu ..na binadamu hukosea..! Kahoji wapi biblia iliandika make mmoja mnakasilika..ni vyema mmjibu kwa kuweka maandishi ya biblia
 
Lilikua agano gani kwenye biblia hayo mambo yalitendeka? Je unajua tofauti ya agano la kale na agano jipya?
utetezi wako ni dhaifu sana,
kwani Adam na ever waliumbwa kwenye agano lipi?.

Mkubali tu hii ya mke mmoja mlijitungia na si maagizo ya bible
 
Mwendawazimu huyo. Mafundisho hayo yanaonesha nyumbani kwake hapakaliki kati yake na mkewe. Shetani wa uzinzi amelala kicgwani mwake mpk anatamani dini nyingine ili ajihalalishie mke mwingine. Tamaa za mwili zinaongoza kichwa chake. Hakuna mchungaji hapo bali uozo.

Si arudi tu alikotoka akaendelee na ustaarabu wake huko! Kwani asili ya dini aliyotoka inamruhusu kuongeza na kubadili kadri atamanivyo
 
Back
Top Bottom