Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Oct 21, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu.

  Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.

  Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu, wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo Kristo nikimuangalia JK na makamu wake, si uoni mfumo Kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi Sheini na Sharif Hamad, siuoni mfumo Kristo nikimuangalia Chande Othman (yule jaji mkuu) na Othaman Rashid (mkurugenzi wa Usalama wa Taifa), siuoni hata nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.

  Wanaoongela mfumo Kristo hawana uthibitisho wa kutosha kuhalalisha madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana wa jua kali.

  Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.

  Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia za amani kupata suluhu.

  Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.

  1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanaoendana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa dini.

  2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya CCM kupata uhalali wa kutawala kwa kura za waislamu. Lazima tujue kuwa CCM wametutumia vya kutosha na kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya CCM wakapiga kura za kuhadaiwa lakini baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.

  3. BAKWATA imekuwa ni kama taasisi ya CCM, wanamuweka wanayetaka wao. Lazima tupiganie BAKWATA kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio CCM hii itasaidia kurejesha imani kwa BAKWATA. Napendekeza Qualification ya kuongoza BAKWATA iwe ni PhD kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu cha MUM kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa BAKWATA ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe shahada moja na kuendelea.

  4. Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya. Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.

  "Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili tumuenzi kipenzi chetu.

  *MWENYE MCHANGO WA KUJENGA USIO KUWA KEJELI AU MAUDHI AONGEZE NISIPOGUSA*

   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,135
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Well said MM.
  100% niko nawe.
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu Mohamedi Mtoi kwanza na kupongeza kwa kutoa mawazo mazito na yenye uoni wa mbali.

  Nina ugomvi na watu wengi kutokana na kuwapa ukweli mchungu kuwa tatizo la nchi yetu si udini bali ujinga, umaskini na ufisadi. Kwa ambao tunazijua taasisi za kielimu za kiislam, ni kweli hazina mfumo wa kielimu wala mpangilio. Nenda pale AlHaramain utalia. Wanaajiri walimu wa kiislam ambao wengi wao hawalipwi vizuri. Watoto wanapewa mizigo ya masomo ya dini tena kwa lazima bila kutoa motisha wa kufanya hivyo.

  Pili baada ya kukopngeza na kutoa machache, acha niongelee hili la mfumo-Kristo. Kwanza hakuna kitu kama hicho zaidi ya kuwa jinamizi linalowasumbua baadhi ya watu wanaotaka kutumia waislam kufikia malengo yao ya kisiasa. Nadhani waanzilishi wa mfumo huu ni akina profesa Kighoma Malima.

  Ni bahati mbaya kuwa vijana wengi wa kiislam walioelimika, ima hawataki au wanaogopa au hawajihangaishi kutafuta ukweli. Wengi wa wasomi wa aina ya Mohamed Said wameshikilia vita ya kutengeneza wakimlaumu marehem Mwalimu Nyerere. Hata baada ya kufa hawampi nafasi wakafikiri kama watu hai zaidi ya kufikiri kwa jazba na kuelekea nyuma. Ukiwa na wasomi kama Mohamed Said wenye kinyongo na chongo utegemee nini mwanangu?

  Mwisho kabisa ni kwamba tunapaswa kuwaelimisha watanzania kuwa tulipodai uhuru tuliudai kama watanzania na si waislam wala wakristo bali watanzania. Uislam na Ukristo vimeletwa lakini utanzania wetu hakuletwa. Isitoshe kwa umaskini tulio nao kama tutaanza kuchinjana wenyewe tutakufa kwa njaa na si matundu ya risasi wala mapanga. Je ni wangapi wanaliona hili?

  Nakupongeza tena mwanangu Mohamed Mtoi kwa kuja na fikra mbadala.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mohamed, I sincerely hope watu (wa dini zote) watasoma post yako wakiwa na fikra huru. Tatizo linalotumaliza Tanzania ni elimu. Kwanza nafasi za elimu ni chache, na ukibahatika kupata nafis elimu ni ya hovyo kupindukia. Ni rahisi sana kumyumbusha mtu ambaye hana elimu.

  Kwenye uongozi wa BAKWATA, mimi sio muislam lakini kama mtanzania nina maslahi na uislam maana sote tunaishi pamoja. Nakubaliana na wewe juu ya umuhimu wa viongozi wenye elimu dunia na dini. Na ningesema Sheikh wa msikiti wa Ijumaa lazima awe na elimu walau Diploma; Sheikh wa Wilaya -Advanced Diploma; Sheikh wa mkoa awe na walau degree moja, na Mufti definately awe na Masters. Ni isiwe elimu ya google. Wawe wamesoma kwenye recognised instututions.

  Hii kwanza itaondoa hii migogoro ya kugombea misikiti lakini pia itasaidia sana kuweka misingi bora ya namna kuinua taasis zilizo chini ya waislam. Ni ajabu unakuta msikiti uko mahali kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna hata nursery school! Sasa unawaambia watoto wenu wanasoma wapi? Lakini utakuta sheikh na wazee wenziwe hawana habari hata kidogo.

  Mambo yameachwa kwa muda mrefu lakini sasa hakuna ujanja.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,788
  Likes Received: 83,160
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana MM michango yako mie inanivutia sana. Ulichoandika ni ukweli mtupu.
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,135
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu waislam ni kua hatutaki kubadilika. Sitegemei Mufti wa darasa la Saba aweze kuja na vision + mission ya kuipeleka Bakwata mbali kama afanyavyo Doctor Alex Malasusa.

  Mi nimesoma A-Level Islamic Seminary, yaani ni bora ukwepe darasa unaweza kupona kuliko kukwepa sala. Watu wanajengwa kiimani zaidi kuliko kidunia, no balances.

  Pia kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa taasisi zetu tofauti na wenzetu. Tukijiuliza Mufti wetu anawajibika kwa nani nje ya nchi, jibu hakuna. So akiboronga hakuna wa kumsimamia maana ye ndio Top. But wenzetu mfano Waroma, wao wanawajibika Vatican, hivyo no ujinga ujinga wa kiuongozi.

  Sambamba na hilo, hao wakubwa zao wa nje wanawapa musaada mbalimbali, ndio maana kila siku vigango, parokia, usharika n.k. vinafungulia na kuanzishwa. Sisi wakubwa zetu wa kutupa misaada wako wapi? Ni kina nani?

  Pia utakuta hata sera ni tofauti. Wenzetu wanatafuta pori a.k.a msitu, wanafyeka na kuweka mission hapo. Hapo zitapatikana shule, hospitality, other economical activities e.t.c, sisi hatuna akili hiyo.

  Mimi ukiacha A-level, shule zingine zote nimesoma na hawa ndugu zangu, yaani Waislamu wenzangu nafanya kuwahesabu, wako wapi wengine?? Hawakuchaguliwa? Au hawakuomba? Wali-qualify? Why?

  Hivi kuna sababu zozote za kisayansi zinazofanya mtoto awe/asiwe na akili just because of dini yake?? Nikichora graph ya waislamu nlioanza nao primary walioacha shule mpaka nimemaliza shahada ya pili, pyramid ni Kali sana? Where are others??

  Fanya research fupi tu;
  Pitia kituo cha daladala anza kuuliza jina wale mateja wa pale, utaambiwa Dullah, Muddy, Ally, Ramso and the like. Toka hapo upitie mahakama za chini ambazo kesi mbalimbali kama za wizi wa kuku, kutukanana, kupigana, n.k. zinahukumiwa, majina ni hayohayo.

  Tumeshakosea, tufanyeje sasa??
  Real inahitajika debate then utekelezaji on this issue.
   
 7. s

  salmar JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Since 1961 mpaka miaka miwili nyuma ndio anapatikana jaji mkuu muislamu bakwata na sheehena wao mufulis simba waondoshwe na hao vibaraka wa bakwata washtakiwe kwa kuufilisi mali ya waislamu
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,135
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Upande mmoja tunaweza kuwalaumu waliowachagua hao majaji wakuu. But tujiulize huyo mchaguzi (Rais) alikua ana wigo gani wa kuchagua??

  Kama kila akipepesa macho, haoni muislam basi angefanyaje? Kunaweza kukawepo na njama za kutukandamiza waislam, but njama hizo zinafanikiwa kutokana na udhaifu wetu wenyewe.
   
 9. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  siasa inapochanganywa na din inakua hatar mno.suala la mfumo kristo halipo ilo embu fanya research ndogo t angalia hao wanaolalamika wana elimu gan alafu utaguxmua ni kit gan kinaendele
   
 10. c

  chama JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 11. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Yap!!! Hujambo baba!! Hadi natamani tuonane tusalimiane!!! Ahsante kwa hoja zenye mantiki, busara na mang'amuzi. Natamani kungekuwa na Waislamu 10 tu wenye muono huu!! Ubarikiwe sana!!!!!
   
 12. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kiukweli huu ndo ukweli japo kuna watu wenye sababu zao ukweli huu kwao hauonekani, nakupongeza sana ndg yangu Mohammed, umeeleza kwa lugha rahisi na umeeleweka sana, nataka kusema kitu hapa.

  Kwa kutumia vigezo vyovyote vile ili kujua idadi ya waislamu na wakristo hapa Tanzania lazima jibu litakuwa wakristo ni wengi kuliko waislamu, miaka yote hata kabla ya uhuru tumeishi pamoja kwa upendo na amani na kama elimu kweli ndo msingi wa mafanikio basi wakristo kwakuwa ni wengi kwa idadi na walijenga shule zao nyingi basi ni dhahiri walio wengi wamefanikiwa zaidi kielimu, sasa tofauti hii ya mafanikio katika elimu kwa maoni yangu nayo ni sababu inayowafanya waislamu waonekane wanyonge, kuhisi walionewa na wanazidi kuonewa, lakini kiukweli alichokisema MOHAMMED hapo juu ndo ufumbuzi wenyewe, waislamu muache kulalama na kujiona wanyonge kila wakati,nyie ni watu mnaomjua Mungu!

  Leo hii iko wazi kabisa kwamba "ADUI WA WAKRISTO NI SHETANI LAKINI ADUI WA WAISLAMU NI UKRISTO" Hii hapana ndg zangu hebu tuwe na subira, kuna mambo yalivyo sasa kama ingekuwa ni nyie sijui ingekuwaje hebu fikiria kama ingekuwa Rais ni mkristo, makamu wa rais ni mkristo, mkuu wa polisi ni mkristo,Jaji mkuu ni mkristo,mkuu wa usalama mkristo....kutaja wachache tu hao, je hali ingekuwaje? Wakristo muda wote wamekuwa watulivu!

  Hebu tusidanganyike tuishi kama zamani changamoto za maisha tuzijadili pamoja kwa hali ya amani na utulivu! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
   
 13. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo lipo; Bwana Mohamed ameliainisha na ametoa ushauri ni nini kifanyike. Baadala ya kulalamika hebu na wewe toa ushauri wako tuone!!!
   
 14. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mohamedi Mtoi,

  Nimekusoma mkuu… Napenda niongeze Kwa mtazamo wangu "Uadui" mkubwa wa Uislamu Tanzania ni haya pia…

  Lugha ya Kiarabu katika Mafundisho

  Lugha ya kiarabu inayotumika kufikisha ujumbe uliopo kakika kitabu kitukufu cha Kiislam. Ni wazi kuwa njia kubwa ya kupata mafundisho ya Mwenyezi Mungu ni kwa kupitia Msahafu ambao una mafunzo mbali mbali ya njia na namna mbali mbali ya kuishi… Na bahati mbaya ama nzuri msahafu ni kitu takatifu kwetu, hauguswi ovyo bali uwe na udhu na kujipanga kwa kutaka kusoma na kuelewa sio kwa mzaha...

  Dini ya Kiislam ni dini ya kistaarabu, iliyojaa mafunzo yaliyojaa wema na upendo ikiwa na hadithi lukuki ya namna ya kuishi katika jamii bila kumkwaza Mwenyezi Mungu na wale waliokuzunguka. Katika dini yetu ya Ki Islam kuna hadi hadithi ya dhambi ambayo inaweza pata kwa kutema mate ovyo na mbele ya hadhara… LAKINI bahati mbaya sana mengi ya yaliyo mafundisho ni mengi ambayo viongozi wetu wengi wa Ki-Islam hufundisha yale ambayo wanaona yanatakiwa..

  kuna baadhi ya misikiti mwaka mzima mawaidha yale yale, umuhimu wa sadaka, usizini, usiibe, n.k Mawaidha ambayo baadhi ya Viongozi wetu hawazingatii wala kufuatilia… Hilo sio tatizo sana kama ilivyo tatizo la waumini wengi ambavyo tunaingia mkumbo na kukubali mengi ya tushawishiwayo/ambiwa hata kama havihusiani na dini vitahusishwa kwa njia moja ama nyingine… Kama ilivyokuwa swala la sensa.

  Kujivua Uislam kwa Waumini wa Waislam

  Wale ambao kwa kiasi kikubwa wangekuwa wakombozi katika kuendeleza na kukuza Uislam na kurudishia heshima yake stahili katika jamii yetu hujivua Uislamu, wapo waislamu wengi wasomi, sikubaliana na hoja kuwa Waislamu wasomi hawapo… Ama kuwa waliosoma ni wachache… Hiyo sio kweli, mana tupo katika wakati ambao nchi ina viongozi wa Ki-Islam ngazi za juu, kati na chini kuliko wakati wowote ule katika historia ya Uongozi wa nchi.

  Hata ni ajabu kuwa kuna lawama kubwa sana za ukandamizaji na hali viongozi wa juu wengi ni Waislam katika taifa ambalo sio la kiislamu bali la wanachi wenye imani mbali mbali. Ninaposema kujivua Uislam nina maana wale ambao ni Waislam katika jamii hasa ambao wamejichanganya katika jamii badala ya kuji acknowledge kuwa wao ni Waislam hujifanya kana kwamba wapo huko bahati mbaya… Hao ndio walikuwa njia ya kuelewesha umma, iwe waislam ama sio waislam kuwa sio yote yale ambayo huwakilishwa huwa ni sawa na sahihi… Swala ambalo linazidi udidimiza Uislamu.

  Mafunzo ya Vitisho katika Dini

  Katika dini yetu ya Kiislam mafunzo ya dini huambatanishwa sana na vitisho… Na mara nyingi elimu akhera hupewa wakati tukiwa watoto… Unafundishwa kwa njia ya vitisho kwa namna moja ama nyingine. Ukifundishwa kuwa kitu Fulani ni kosa adhabu yake unapewa ‘imagination' ya kuogofya na kutisha. Kwa mtoto hadi pale unapokuwa kama hujabahatika kuisha maisha ya kueleweshwa kwa njia zaidi ya elimu unapowa unaweza kuwa rigid sana katika imani hata kwa yale ambayo sio msingi kuwa rigid. Naamini kuwa ni DHAMBI kubwa sana kushika msahafu huna udhu, sembuse kuukojolea?

  Mimi kama muumini nikiwa karibu nastahili kumuelwesha yeyote asielewa (hasa ambaye ni dini tofauti) kuwa haruhusiwi hata kuugusa let alone kuukojolea. Haya mafunzo ndio sasa kwa namna moja ama nyingi umepelekea tatizo kubwa lililo zaa matatizo katika jamii nzima. Haya mafunzo ya vitisho ndio yalifanya Yule kijana Muislam katika lile alilomwambia mwenzie na kupelekea mwenzie kutaka kufanya majaribio kama ni kweli… Ndio maana kwa kiasi kikubwa namlaumu sana aliye tulia tuliiii akisubiri mwenzie akojolee kuona kama atageuka nyani... Kwa mtazamo wangu katenda dhambi kubwa! Karuhusu na kushawishi kwa nguvu zote kitabu kitakatifu kichezewe.. Kwa kweli inasikitisha...

  Kukosekana kwa ustaarabu

  Ustaarabu, sijajua kuwa tulikwamia wapi hasa… Katika jamii ya watu waliochanganyikana hatuwezi wote kuwa sawa, hatuwezi wote tukaamini kitu kimoja. Na kawaida kila kundi lina namna yake ya kutamka na kuita kundi ambalo hawawakubali… Kuna maneno kama "Kafiri" na "wagalatia". Kutumia maneno kama hayo kwa kumuita mtu hivyo moja kwa moja hujenga chuki kubwa sana… Sasa hapa nashindwa kuelewa kuwa dhambi inapimwa pale ambapo muumini anatataka? Mradi anawakilisha dini yake ana ruhusa ya kutenda dhambi zingine? Huwezi hata siku moja kumbadilisha mtu Imani, msimamo ama mawazo yake kwa kukashifu, kumkejeli ama kumdharau!

  Ni lazima umuingilie kwa kumuelewesha… Ni lazima umweleze kwa nini hapo alipo sio sahihi na kwa nini huko unakotaka aende kuna manufaa juu yake! Kuna mambo mengi wanadamu hufikiria ama kujisemea moyoni kuhusu watu mbali mbali, lakini tunajua fika kuwa kutamka haitakiwi… Sio sababu huwezi, sio sababu wamuogopa, wala sio sababu labda atakuadhibu… Ila tu kwa sababu kubwa kuwa inakuwa SIO ustaarabu kutamka lile ufikirialo juu yake! Tulichotofautiana na Wakristo katika "name calling" katika waliomini katika dini ni kwamba Waislam tuliowengi tunakutamkia kuwa wewe ni "Kafiri" na Mkristo anakufikiria ila atatamka akiwa na waumini wenzie (huo mfano hauingii kwa majority ya JF members walio na ushabiki wa matusi yasio na tija wala kujenga).

  Umimi wetu Waislamu

  Inawezekana kweli serkali kwa njia moja ama nyingine imeweka mazingira ya kuupendelea ukristo, labda sio kwa nia hiyo ila ilitokea tu ama kwa makusudi. Hata hivyo kulitazama hilo swala linatokana na vile sisi twajitazama vipi... Kama tungejitazama kuwa tuna haki na hii nchi kama mtu yeyete yule iwe Mkristo ama sio mkristo ina mana tungeweza piganaia kuweka na kutengeneza mazingira ya kuhakikisha kuwa na sisi tunakuwa na kupata hilo ambalo tunaona tunapunjwa badala ya kulalamika..

  Umimi umekuwa mkubwa saana kwa waislamu walio wengi... In the sense kuwa mimi ni muislamu basi kila kitu hadi nchi iendeshwe Kiislamu... HAPO nauliza kwa misingi ipi? kwa nini? na wa imani nyingine iwe vipi? Ama haihusu sababu sio Waislamu? Na kama haihusu - ni vigezo vipi vya fikra vinatumika kufikiri hili kwa kina?

  Inakuwa mimi, mimi mimi... Mimi kama Muislam nina haki hii…. Mimi Muislamu matatizo yangu yanasababishwa na huyu… Mimi nakandamizwa… Mimi ndio nastahili sio Yule (hata kama muislamu mwenzio). Dini inafundisha tumheshimu kiongozi wetu, sasa hiyo ruhusa ya kumdarau kiongozi wako kwa ushabiki sio hoja unatoka wapi? Haya basi wewe ni Muislamu unakandamizwa; umejiuliza Waislamu wengine walifika hapo unapopataka wamefikaje? (Kiongozi anakuja na hoja aliyefiika hapa ni msaliti sio muislamu kamili – Huyo kiongozi ni Mungu??) Unapolalamika unakandamizwa ni haki kulalamika LAKINI Je upo tayari kwa mabadiliko? Upo tayari a wewe kucheza nafasi yako ama unasaburi uletewe hayo mabadiliko katika sahani? Kama yote hayo ni kweli hatutakomboka kwa kulalamika ama kwa vitendo vya hasira bali kwa vitendo vya kujenga na kuweka misingi bora ya UISLAMU mbeleni ndani ya taifa letu!

  Waislam… Bado tupo nyuma.. Bado tuna safari ndeeefu, nab ado tunahitaji kujikomboa kabla ya kukombolewa. Dunia ya leo kila mmoja ana maslahi yake binafsi... Inatakiwa kutulia, kutafakari, kujuwa hasa ni nini UNATAKA, nini haki na sawa na kipi ambacho hata Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mtume Mohammad (S.A.W) atakubali kuwa ni haki ufanye. Maisha yamebadilika…. Dunia imebadilika.. Nyakati zimebadilika. Inatakiwa tusibadilike Uislamu wetu ila tubadilike yale ambayo sio lazima yafafanuliwe kwa Uislam kwa maslahi ya wachache wenye niya na malengo ya kutumia Uislam na Waumini wa Waislam vibaya! Tufanye mambo kwa kujipanga, kutafakari na ustaarabu huku tukimhusisha Allah kumuomba kutupa hekima katika matendo yetu.

  BTW, Nakubaliana na swala la BAKWATA, Hicho chombo inabidi kivunjwe kwa manufaa ya wengi sababu ni asilimia kubwa ya Waislam tunapingana nacho na kuona kuwa hakifai.

  Huo ni mtazamo wangu, kama kuna mahala nimeonesha kutoelewa swala kwa ukina kwa namna ya maelezo, nakaribisha kuelezwa/eleweshwa.

  Wabillah Tawfiq.

  Pamoja Saana AshaDii.
   
 15. K

  KIRUMO JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli mtupu.

  Wakati tunapata uhuru shule nyingi zilikuwa ni za Wakristo. Wamisionari wao walihakikisha kuwa popote penye Kanisa panakuwa na shule pamoja na hospitali. Waislamu walikuwa na shule chache sana. Haijalishi kuwa nia ya wakoloni wale ilikuwa watupe elimu ya kuweza kuwatumikia tu, lakini ilileta mwangaza kwa walioipata. Mwalimu Nyerere kwa kuliona hilo akaona kuwa wakristo wanaendelea kuanzisha shule mpya na waislamu hawana mpango. Akaona maono ya mbali kuwa taifa litakuwa na wasomi wakristo wenye nuru na waislamu wengi walioko gizani na akafanya maamuzi magumu ya kutaifisha shule zote za wakristo ilo na waislamu nao wasome.

  Hata siku za karibuni waislamu walipodai kuwa shule zilizotaifishwa zirudishwe, Kikwete alisema kuwa hilo haliwezekani kwa kuwa itanufaisha makanisa zaidi kwani karibu asilimia 80 ya shule zote zilizotaifishwa zilikuwa zao.

  Inanishangaza kuona waislamu wakimwona Nyerere kwa mmoja wa maadui zao wakuu. Hulka ya wakristo ni ukarimu. Hawakumbishia Nyere bali waliona nia yake njema kwa ndugu zetu waislamu na hakuna Kanisa hata moja lililowahi kumlaani mwalimu kwa kutaafisha shule na hospitali zake. Walionufaika ndio wanaomlaani.

  Angalia tu mfano wa vyuo vikuu. Baada ya kuruhusiwa tena kujenga mashule na Vyuo vya binafsi, Makanisa yameanzisha mashule mengi sana tena ya viwango. Wameanzisha vyuo vikuu vingi katika kila kanda ya nchi yetu kama si kila mkoa. Waislamu wanafanya nini? Kwa kadri wanavyolalamika kuwa huo ni mfuma Kristo ndio wanavyopoteza muda na huku wakristo wakiendalea mbele. Na elimu ndio ufunguo wa maisha.

  Waislamu amkeni. Acheni kutoa sababu za kufikirika na kusadikika tu zisizo na uhalisia. Vurugu hizi ni taswira ya kukosa elimu.
   
 16. K

  Kigano JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikupenda kuongeza neno, lakini Nimeumia sana kuona "Chama" bado anabisha ukweli huu !
   
 17. K

  Kigano JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda ungebainisha hayo matatizo unayosema, maana mwenzio amebainisha, ameenda mbali zaidi, akatoa mifano, ukisoma uchambuzi wake unapata nafasi ya kutafakari. kipimo kingine unachoweza kuangalia kwa haraka ni pale ambapo zaidi ya 99% ya wachangiaji wameunga mkono hoja yake, haiwezekani wote hao waunge mkono hoja ambayo haina mashiko ! Lets be objective !
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mohamedi Mtoi

  Umefungua chapter mpya sijui kwa mashinikizo au umeamua jiangalia upande wa pili. Siwezi ku criticize kama nilivyofanya ktk thread ya maggid kwa vile kule mlikuwa kwa kujijua au kutojijua mlikuwa mkiwalinda waislam wapenda vurugu na chuki kwa kuwaapooza waathirika. This time around unafanya wengi walichopenda na kushauri kuwa anza kueleimisha nyumba yako ili wasitoke nje kwa aibu.

  Nawajibika kusupport si kwa vile upo ktk fikra kama zangu 100% ila kwa vile umeanza mwanzo mpya ingawa ni mgumu. Ni wazi kuna waislam wengi watakuona msaliti na umelewa dunia au kurubuniwa na makafir. Ukweli utabaki palepale kuwa wamekuwa programmed na mihadhara, cassete za video na sauti kw amiaka mingi, na wamepotoshwa sana na watu waliowaamini kama viongozi wao wa kiroho na kimwili. Utakuta sizable population ya vijana wasomi wa Kiislam ambao wamechanganyiwa elimu ya kaina Malcolm-X na ukoloni, mapinduzi ya mtu mweusi na uislam na bila jijua wakafanya kazi ya mkoloni mwenye kujitambulisha kama muislam Muarabu.

  Hawa vijana wana nguvu zinazoambatana na kwenda na wakati kwa kiasi fulani. Basi ni rahisi sana kukuvunja moyo au hata kusema kiholela tuu kuwa hujui usemalo, na blah blah nyingine kuwa wametembea dunia na wamona watu wakiingia ktk uislam kwa fujo. Ukiwauliza kaina nani watakupa majibu mepesi sana, mengine ni watu ambao hata hawajabadili na hawana mpango wa kubadili zaidi ya kutokea katk event moja mbiliza waislam. Sasa haya yote yanawafanya waislam waishi kwa ndoto na hisia huku wakiskilia kauli za kuwapa hasira na moyo.

  NI kipindi waislam wajue kuwa Mungu wa kweli ana mahusiano binafsi na viumbe wake na ana majukumu vinafsi ambayo huwa ndiyo anayotumia mhukumu mtu binafsi na si Mob. Wakifikia kumchukua Mungu km mahusiano binafsi naye watu watatii sheria, wanaheshimu haki za wengine,watajitahidi jiuliza maswali binafsi kabl aya kufanya maafa kwa wengine kabla ya kufuata mkumbo.

  Mtoi unahitaji pewa moyo, na pia kukumbushwa hatari yake ,sadaka unayohitaji itoa, na pia kutojisahau na kuja kuwa taasisi inayotumika kuwanyonya waislam wenzio. Sijui kwanini hukuliona hili ila ukwei ni kwamba waislam ndio wanaowanyonya sana waislam wenzao, ndio wanaowageuza waislam wenzao farasi ya kula maisha huku wakiwapa marejesho ya chuki, na vitu vidogo vidogo km futari, na michango ya hija. Hawataki waislam wajifunze vua samaki ili wakajilishe wenyewe kwa kadiri wanavyoweza vua. Wanataka kila mara waislam wapange foleni wapewe kipande cha samaki huku wakishukuru kwa kuokolewa toka ktk dhiki (inayosingiziwa kuwa ni mfumo kristu kw avile wakristu hawaingii huko ktk nyumba za ibada).

  Ni kipindi waislam wakafikiri tena kuwa badala ya kufikiri kutawala baraza la mitihani ili watoto wafaulu ni bora wakajifunza jenga taasis imara, huku wakiwapa watoto wao mioyo ya kupambana ktk haki na kazi huku wakitafuta hekima. Kwani hilo litawasaidia kufaulu kwa haki na hata watakaoshindwa kielimu watakuwa na mengi ya kushinda ktk maisha. Mahubiri wawapayo vijana wao yanawavunja moyo na kuwapa excuse tuu ya kushindwa. Na hili litaonekana kwa wanafuzi wa kiiaslam wanaosoma ktk shule za serikali au za kikikrsitu watu wanafaulu kwa juhudi zao kwa vile hakuna huuu uhamasishaji wa kufelishwa.

  Nakumbuka shule ya msingi niliposoma tulikuwa na wanafunzi wazito sana darasani.Ila nilishangaa wakati wa mitihani ya darasa la saba kijijini enzi hizo. Wazazi wa hawa watoto walikuwa wakila viapo kabisa kuwa kama hawatakata mitihani watoto wao watafaulu. Na matokeo yalipotoka walikuwa wamefail (na hakika si kutochaguliwa kwani hawa watoto walikuwa wagumu hata kuigilizia). Hawa hawakuwa watoto wa kiislam pekee ila hata wa makabila na dini nyingine. Lengo langu hapa ni kuonyesha jinsi gani waislam wanavyoteswa na kurudishwa nyuma na mazinginra waliyoyajenga kuwazunguka.

  Vijana wengi wa kiislam waliokuwa wakiipend adini yao bila kusikiliza mihadhara ya chuki, walikuwa watu wazuri sana ktk dunia na watu wengine hadi pale walipofanikiwa na kurudi kwa hawa masheikh wa design ya kutoka Tabora, Kondoa, Zenj, Ujiji n.k ili waweze mrudia Mungu na kumshukuru kwa mafanikio n
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Chama soma hoja badala ya kuleta uzushi. Naona umeanza kuthibitisha aliyosema Mtoi. Maana badala ya kuangalia nini kimeongelewa unaanza shutuma na jazba.
   
 20. c

  chama JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nadhani hujamuelewa Mtoi; amedai haoni tatizo liliopo liwe ni mfumo kristo kama unavyodaiwa au mfumo wa ukandamizaji; cha kushangaza amekuja mawazo ya kurekebisha mfumo ambao hauna tatizo; yeye haoni tatizo la mfumo mzima kwa sababu lengo lake kuu ni kutaka kuishutumu CCM; ushauri ni serikali kuvunja MoU na taasisi zote za kidini hapo ni pa kuanzia tu.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...