Mke wangu wa ndoa kapewa Mimba na mtu mwingine

trigger

Member
Nov 30, 2011
95
25
Wana jamvi naomba msaada wenu katika jambo hili;Mimi mwaka 2009 nilifunga ndoa na binti mmoja ambae nilikutana nae kazin na baada ya kama miez kadhaa tuliamua kufunga ndoa kanisani lakin wakati nafunga nae ndoa yeye alikuwa tayar kaacha kaz katika shirika tulilokutana so baada ya kufunga ndoa maisha yaliendelea lakin mie nikikaa mkoan yeye akikaa Dar kutokana na majukumu ya kikazi mie nafanya mkoan yeye Dar kwan alipata kaz nae baada ya kukaa mtaan muda flan.
Mahusiano yaliendelea vizur tu lakin nikaja gundua ya kwamba anachat na mtu ambae tuliwah ishi nae mkoan na nilipoamua kumtafuata akasema binti alimwambia hajaolewa,akakubali kuacha kuchat nae.Vitimbi vikawa vingi sana hatak kuja tena mkoan kuniona mpaka mie niende Dar na kwa bahat mbaya mie nilikosa likizo kwa miaka 3 mfululizo na nikawa kama kuja Dar ni training ya cku mbil mpaka tatu nikawa nakutana na vituko sana mara ninuniwe mara kahama nyumba wakati yy yupo pale pale,stand kuja kunipokea hatak na wakat tuna gar la kutumia nyumban.
Mahusiano yakawa yanaenda kwa mazoea tu mwaka jana kuna mtu akanipigia cm kunipongeza kwa ujauzito wa mke na nilipata shock ukitegemea nina mwaka cjaonana nae kimwili kwan nikienda training fup mara nyingi anasema yupo period,nikazima so kwa kukubali ile hongera nikaanza upelelezi na wakati huo alikuwa anaweza akakaa hata wiki asipokee simu yangu na akipokea da sio dharau hizo kwamba anitak.Kupitia dada ake mmoja akakubali kuniambia ukwel wa jambo hilo kwamba ana mimba na wao wamejua co yangu kumuuliza hawaezi nikawa na uhakika na jambo hilo nikaamua kumwambia tuweke sawa kwan naamin kateleza na tuendelee na maisha kama kawaida akasema hatak na niendelee na maisha yangu kama kawaida japo nilimbembeleza sana
Mwez wa kwanza nikaamua kwenda Dar kwan nilipata ruhusa kama ya siku 9,ndugu zangu wakasema niende nikahakikishe kwa macho yangu na kwa msaaada wa yule dada alinicholea mchoro muda ambao yupo nikaenda nilimkuta na yy ndio alinifungulia mlango kwanza aliponiona kidogo asifungue mlango ila akaamua baada ya dk kama tano akafungua nikawa na aman sana kumwona na ile hali japo yeye alikosa raha kabisa nikajaribu kumsocialise asijione mkosaji nikapiga stori baada ya dk kumi nikaaga kuondoka kwan cku iliyofuata nilikuwa narud mkoan japo nilimwambia ntaenda kesho yake na ndio nikathibitisha ya kwamba ana mimba
Baada ya kurud mkoan akawa amerudisha sana mapenz kama mwanzo simu za mara kwa mara na msg sasa mie nami kuogopa acjepata matatizo wakat wa uzaz nikawa namjal kama mie ndio mwenye mimba na akawa na aman kila ktu akawa ananiambia kuhusu mimba hyo,Juz Mungu kasaidia kajifungua mtoto wa kike nikaambiwa na mpaka sasa kila ktu maambiwa mtoto anasumbua hik mara kile kwa kifup kaona kama mtoto wangu
Picha ya cku ya harus aliitoa sebulen muda sana lakin sasa nimeambiwa kaiweka sebulen tena na anaonesha kukumbuka kuna mtu alimpenda,sasa wana jamvi mie naomba ushauri wenu nafanyaje ktk suala hilo,mimba sio yangu na je kama nikiamua kuwa na mtu mwingine je ntafunga nae ndoa kwan mie ni mkristo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Km una uakika mimba si yako ushauri wng achana naye babu ata kumiza kichwa angalia maisha yako km wanawake wapo wengi, na kwa nn arudishe mapenz ghafla kwako labda aliye mtia mimba kachomoa mpaka kafika hatua kabeba mimba bora ungesikia labda kacheat kitu cha kawaida ungemsamehe maisha yange endelea. Ni mtazamo tu.
 
Achana naye huyo co mwanamke mwema.vilevile hyo ni skendo mme mwenzako kuja kukuzalia mtoto ndan ya familia yako as if we hauwez.kuhusu suala la ukristo na ndoa hyo tayari iko kinyume na maagano ya din,ndoa ni kiapo cha wawili sasa kama mwenzako kazin nje tayari hyo imeharbika kwa wote.piga chin tafuta dem mwngn
 
Hakuna mke hapo,ila uamzi wa mwisho unao wewe....dah!ndoa hizi
 
kama unampenda endelea nae kama kawaida isipokuwa lazima uishi nae venginevo utalea mtoto mwengine, huyo mtoto ukimlea Mungu atakulipa kwa ulezi wala usiwe na shida
 
Una moyo mgumu sana wewe! Mimi changamoto hii mbona siiwezi! Kweli tunatofautiana!
 
Hakuna mke hapo,ila uamzi wa mwisho unao wewe....dah!ndoa hizi

hii sio ndoa. Mwanamke anagoma kukufuata, na hamuwezi kuonana, umo tuuu!. Na anahama haujui kahamia wapi. Still unaita mke? Miujiza ya dunia ya tatu?
Huyu hata matumizi kwa mkewe alikuwa hatoi. Ukimpa matumizi mwanamke na kuangalia affairs zake hata akikucheat anacheat kwa.woga!

mtoa mada, hivi hata kodi ya nyumba ulikuwa unajua inapotokea? Manake ukute mimba ni ya mfadhili?
 
Dah mpaka inafikia hatua hiyo, nahisi kuna vitu vingi umekosea wewe kama mume. Pia nahisi kuna vitu unatuficha hapa. There is more than what meet the eye.
Ushauri wa haraka, kaa pembeni jipime wewe kwanza
 
pole sana kwa mkasa.
Actually ulikuwa na mke jina tu. Kuanzia jinsi mlivyobebana, then kukaa mwaka bila kuonana, etc. hapakuwa na ndoa ya kweli hapo, zaidi ya cheti cha ndoa. Suala la wewe kugundua 'mkeo' kapewa mimba na mtu mwingine ni CHACHANDU tu ya tatizo, sio tatizo lenyewe.
ujumbe kwa vijana wote: NDOA SI KUSIMAMA MBELE YA KASISI, au kukalia mkeka, au kusaini cheti. NDOA NI TAASISI.
 
eeh pole sana...mimi naona huyo dada hakufai, utazidi kupata presha bure...yaani dharau zote leo abadilike ghafla?amekuona zoba..!!
Hadi ndugu zake wanajua mwana si wako, mmh! Hapo ndoa imebaki jina. rudisha heshima yako kama mwanaume!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
King'asti nachoomba ushauri je naweza oa kwa ndoa tena kwa hyo scenario


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hahaha, mi namshauri wakafanye sup ya mafundisho ya ndoa. Mweeh, tembea ujionee. Bushoke ana nafuu aisee.

sikujua kama kuwa mzazi ni taabu kiasi hiki....!


hivi mtu anaweza kutamka kwamba bado ana mke na kuna ndoa?

halafu mwanamume gani unakaa mwaka mzima bila kuonana na mkeo? Hiyo ni kazi gani na wanalipa dola ngapi mbazo ni zaidi ya mkeo?
 
Nilitaka nikushauri upime mwenyewe na uamue mwenyewe, Lakini baada ya kusoma kile kipengele kuwa alishawahi kukutamkia kwamba hakutaki, nimebadili mawazo, huna mke hapo bro sepa kivyako, msimamo wa mwanamke ni kwamba hakutaki hiyo hali ya sasa hivi ni geresha tu ili uwe una toa pesa kulea mtoto wa jamaa.
 
Back
Top Bottom