Lusekelo (Mzee wa Upako) ana mapepo na ni Agent wa Shetani. Ataka oa mke mwingine?

Nmejikuta wakati flan nikitafakari sana matendo ya huyu anayejiita Mchungaji na kugundua ana mapepo na ni mtumishi wa shetani kabisa.

Kitendo cha kusema anamtafuta aliyesema wakristo waoe mke mmoja amhoji tayari anaonesha kuukana ukristo na kujihalalishia uzinzi.

Mungu angetaka adam awe na wake wengi angemtengenezea na mwingine.lakini hakufanya hivyo.kusudio la Mungu lilikuwa mke moja na mume mmoja. Kuhoji uhalali wa neno hilo tayari anaonesha ni mtu aliyekengeuka.

Ndugu huyu anayefahamika kwa majivuno na kiburi kinyume na matendo ya ukristo Yesu aliposema Mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu. Yampasa ajinyenyekeze na kujishusha kama mtoto mdogo.

Lusekelo ambaye ni juz juz tu alikumbwa na kashfa ya ulevi jambo ambalo ni aibu hata kwa mchungaj kusingiziwa. Bado hakuweza kujieleza akaelweka machoni pa watu wa Mungu.

Style yake ya mafundisho imejikita zaidi katika yeye kupokea sadaka na tunaona hata kwnye ibada anavyofurahia kutuzwa pesa. Na hapa ndipo ukristo unapozidi kujidhihilisha kuhusiana na siku za mwisho kutakuwepo na manabii na wa uongo na wachungaj wa aina ya lusekelo.

Haya ni mafundisho ya kishetani kabisa. Tamaa za mwili ndizo zinazoweza mkristo akahoji jambo kama hili.

Yesu anasema mwanaume atamwacha babaye na mamaye naye ataambatana na MKEWE na si WAKEZE. Mathayo 19:3-9

Ukina Mkristo anaanza kutaman yaliyo kwa shetan ujue tayar shetan ameshamkamata. Tuendako usishangae kusikia lusekelo anaruhusu waumini wake kuoa wake zaidi ya mmoja.

Ukiona hivyo pia ujue alishapiga KONYAGI. Maana hizo ni mada za walevi.
 
Sheria ya kuoa mke mmoja sio Sheria ya Mungu, Bali ni Sheria ya kanisa. Kama Mungu aliweka hiyo Sheria ilikuwaje akawabariki kina , Jakobo, Ayubu wakati walikuwa na mke zaidi ya mmoja.
Kanisa liliweka hiyo Sheria sababu wakijua binadamu ni dhaifu, akiwa na mke zaidi ya mmoja ataiweza kuwapenda sawasawa na hapo itazuka chuki Kati yake, wake zake na vizazi vyake.
Wengine wanasoma biblia na kukariri bila kuitafakari.
 
Maandiko yanasema "...mke na mume wataungana na kuwa mwili mmoja..."
Haijasema "...wake na mume..."
Utata unakuja utakapojua kua Musa alioa wake wawili na jibu hua linakua "Lile ni agano la kale".

Mchungaji atatenda upuuzi akiulizwa anajibu " Fuata maneno na si matendo" kwenye biblia tunaambiwa matendo ndiyo yatakupeleka unapotaka, hata Baba wa Taifa alisema hiki kitu.
Yesu hakuja kutengua TORATI, ...BALI KUIKAMILISHA!
... HAKUNA SHERIA YA KUOA MKE MMOJA KATIKA BIBLIA!
 
Back
Top Bottom