Lulu ana zaidi ya miaka 18 - Jamhuri!

Kwa upande wangu kauli si kigezo cha kusema ati ana zaidi ya miaka 18, ila kwa suala la kuomba passport na driving license hasa passport ambayo lazima uambatanishe birth certificate naweza sema hivyo ndo vielelezo sahihi, ila ki ukweli Lulu ni above 18 wala hajadanganya ila kasema hivyo vya under 18 baada ya kupata hili tatizo.
 
Maskini Lulu, aliutafuta kubwa mapema sasa unamtokea puani, majuto huja baada ya kutenda, pole yake

Kama kwenye fomu ya polisi alisema 18 hakuna haja ya kupepesa macho,,,,,,aliongea akiwa na akili timamu,,,,iaminike hivyo,,,,,haina haja ya kwenda clouds wala wapi
 
Hii nchi kila kitu ni ubabaishaji! Kama kweli hii nchi inafuata sheria yakutoa vyeti vya kuzaliwa na kuzingatia umri wa mtu mbona hawalizingatii hili ambalo wameliweka kwenye chupa za bia kwakuandika kua HAIUZWI CHINI YA UMRI WA MIAKA 18?
Laga.JPG
 
Tatizo serikali yetu ya Jamhuri ni DHAIFU.
Kwa mtu kuwa na vyeti viwili vya kuzaliwa (Nyaraka za Jamhuri) na kuziwakilisha Mahakamani,Hilo tu ni kosa tosha la kughushi Nyaraka za Jamhuri. Ilitakiwa apewe takribani miaka 5 kwa hilo tu,ili wananchi tujifunze kuwa na adabu ya sheria za Jamhuri na Mahakama.

Kama ana leseni ya gari na pasi ya kusafiria (Nyaraka za Jamhuri) na zote akiwa ametia sahihi yake na vidole vyake kukiri kwamba yeye ana umri zaidi ya miaka 18,Nafikiri ni vyema na haki kwa Sheria ya Jamhuri kumchukulia kama hivyo. Hii itatufundisha wale wote tuliozoea magumashi...siku ikitokea bahati mbaya ndio utajua maharage sio mboga ni kiungo cha makande tu.
Tafakari!
 
Bob G mbona umeongea kwa Lugha ya ukali hivyo.anyway hii iwe fundisho kwa wengine hasa sisi wazazi tuwalee watoto katika maadili yawapasayo na sio kumwacha afanye anachotaka.Mimi naona Lulu atafungwa kwa uwongo na si vinginevyo na sasa naona utata hata kwenye kifo cha kanumba(RIP) asiposaidiwa atafungwa kwa uwongo
 
Let's face it ... hili suala linaonyesha udhaifu kwa serikali yetu pia. Kwanini ulazimike kuchunguza umri wa mtu kwa kupitia maombi yake ya passport ya kusafiria na driver's license. Vipi kuhusu cheti chake cha kuzaliwa? Kwani hakuna record yake ya kuzaliwa? Alizaliwa wapi na ilirekodiwa vipi? This case is getting ridiculous!

Nakuhakikishia huyu mtoto alidanganya umri ili aweze kula bata na kwa kuwa marehemu alishamwahidi atamuoa hivyo ni bora adanganye. Pia nilisikia katika kipindi cha mkasi kuwa amefurahi kufika 18 ili aweze kusaini mikataba!!! Ila kitakacho msaidia kuwe na makaratasi tu ya kile cheti cha clinic na tangazo la kuzaliwa ambavyo vinatumika kupata cheti cha kuzaliwa kwa wale ambao wamezaliwa miaka ambayo vyeti vya kuzaliw vilikuwa si issue sana kama ilivyo miaka hii. Kwa mantiki hiyo ili wazazi wake washinde ni vyema tangazo la mtoto na kadi ya clinic itawasaidia sana. Kila la heri. But du ni fundisho kwa mastaa wetu na wazazi tujitahidi kuwa karibu na watoto wetu kwa maadili mema.
 
Hana miaka kumi na nane, ni mtoto mdogo. Wakati anasema hivyo hakujua kama haya yatatokea na alifanya hivyo ili aweze kupata mambo fulani kama, leseni ya udereva kwa sababu ili aweze kupata leseni lazima awe na miaka isiyopungua kumi nanane, vile vile aliamua kujikuza ili aweze kuingia disco na kunywa pombe. Cheti chake cha kuzaliwa ndio msema kweli.
 
Huyo mtoto ni dhehebu gani,kwasababu kama ni Mkatoliki rekodi zake zote zipo ktk Parokia alizaliwa! Ukiondoa issue ya umri,mimi sioni hata kama ana kesi ya maana ya kujibu! Lakini pia hii ni fundisho kwa vijana wanaopenda kuishi maisha ya ujanjaujanja!
Asante Angel.yaani mtu na akili zako unatuambia alisema ana 18 kwenye tv show au movie hiyo ndio proof ya umri wake?this is ridiculous!teenagers dunia nzima wanadanganya umri ili waingie club,wanunue sigara,wanunue pombe!tena kwenye nchi ambazo wako strict itakuwa Lulu!kadanganya ili apate driving license na passport aweze kusafiri(shwa) na kasaidiwa na watu wazima wasio na utu wala aibu....
 
forensic people tumien carbon fourteen mtajua ana umri gani faster!! au tumieni nguvu za mabuti ya mwemaaaaa, kamata baba/mama ya toto weka ndani yeye taeleza wapi naundia hii toto!

kwani hao rita hutoa vyeti mara mbili mbili? Kama majina yanatofautiana na la kwake si hao rita basi wamwandikie jina sahihi na kwamba ana 17? Nchi hii klia mtu mjuzi.
 
Huyu mtoto atakuwa amefoji sana vyeti vya kuzaliwa maana ninavyojua pale uhamiaji wakati anaomba passport lazima aliambatanisha cheti chake cha kuzaliwa nafikiri ndo maana jamaa wamekamata hizo document zake za kuombea passport ambazo zinaonyesha ana 18 years. Haya baba na mama kila mtu anasema lake kuhusu jinsi mtoto alivozaliwa huyu anasema alizaliwa dar mwingine alizaliwa kilimanajaro kazi ipo,,, kifo cha nyani miti yooooote huteleza huyu anaweza kufungwa kwanza kwa kosa la kudanganya na kufoji nyaraka muhimu za serikali. Halafu yeye mwenyewe alifanya sherehe kubwa sanaaaa akisema ni siku yake ya kuzaliwa na alikuwa anafikisha miaka 18. Nafikiri hili liwe fundisho kwa wengine
 
Jamuhuri imetoa vithibitisho kwamba (ELIZABETH MICHAEL)Lulu ana zaidi ya miaka18.
Aidha mawakili wa Jamuhuri wakiwakilisha vidhibitisho hivyo wamesema wamepata baadhi ya vidhibitisho ikiwemo cd iliyorekodiwa kabla na moja ya chombo cha habari CLOUDS TV chini ya mtangazaji "ZAMARADI MTETEMA"zinamuonyesha Lulu akikili kwa mdomo wake kwamba ana zaidi ya miaka18.Aidha vidhibitisho vingine vilivyopatikana kutoka police vinaonyesha maelezo ya Lulu kwenye form wakati akiomba pass ya kusafiria na driving licence zinaonyesha Lulu(ELIZABETH MICHAEL)ana zaidi ya miaka18.

Nyie mawakili wa serikali fuatilieni mambo haya ili kupata ukweli uliyo beyond the shadow of doubt: moja, kwa kuangalia alizaliwa hospitali ipi, ili makaangalie records zake, yaani toka mama yake anaudhuria clinic na siku ya kuzaliwa kwake na kuruhusiwa ila kama hakuzaliwa nyumbani. Pili, angalieni records za maendeleo ya mtoto kwenye clinic ya watoto under five aliyokuwa anahudhuria. Tatu, muombeni a-present kadi yake ya clinic when under five. Nne na mwisho, nendeni kule alikoanza kusoma hasa records zake za standard one and form one enrolments.

JK atakuwa kamwondolea aibu wakili wake Jaquina kwa kumteua kuwa jaji ila inaonyesha jinsi wakili hakuwa makini na sasa ndio jaji, je atakuwa jaji makini?
 
Hii nchi kila kitu ni ubabaishaji! Kama kweli hii nchi inafuata sheria yakutoa vyeti vya kuzaliwa na kuzingatia umri wa mtu mbona hawalizingatii hili ambalo wameliweka kwenye chupa za bia kwakuandika kua HAIUZWI CHINI YA UMRI WA MIAKA 18?
Laga.JPG

Mkuu bajeti yetu inategemea kodi nyingi kutoka kwenye ulabu. na hesabu rahisi tuu, lazima tunywe sana ili kodi iwe kubwa na mapato kwa serikali yaongezeke.
Juzi nilimuona mtoto wa Kawawa nae anatetea tumbaku kwa nguvu zote.
Hii ndo Tanzania, kwa wasioijua
 
sasa hapo ni amekwisha na je atashtakiwa kwa kosa jingine la kuidanganya mahakama au inakuwajewajuzi wa sheria tujuzeni.... maskini lulu jela itamuozea

waliomshauri walikosea sana kwani wamejisahau kuwa lulu alikuwa na leseni ya kuendeshea gari,passport ya kusafiria na kumbumbuku ya hitu hivi hupaki serikalini hata kama wazazi wake walikwenda kufoji cheti cha kuzaliwa rita tayari lulu alishatengeneza leseni na pasi ya kusafiria kitambo

Mimi nina mtizamo tofauti na haya yote yaliyotokea na yanayoendelea kutokea.

Kwa kifupi huyu mtoto na wazazi wake (mmoja kama sio wote) dhiki imewafikisha hapo. Upo uwezekano mkubwa kuwa Lulu hajafikisha miaka 18 (au by then hakuwa na miaka 18) lkn hizi confusion zinaletwa na matukio ya kuendekeza njaa aliyoyafanya hapo nyuma.

Naamini upo wakati ambapo Lulu alikumbwa na ukosoaji mkubwa juu ya kazi yake ya usanii ukilinganisha na umri. Kwa lugha nyingine, jamii ilikuwa inahoji kwa nini mtoto mdogo hivi anavaa nguo za uchi na kushiriki maigizo yenye kumzidi umri? Katika ku- justify matendo yale ambayo kiukweli ni machafu (km hili la kuwa na mahusiano na Kanumba), Lulu, kwa kushirikiana na mama yake watakuwa walifanya jitihada nyingi za kuonesha kuwa Lulu ni mkubwa kwa hiyo ana haki ya kufanya yale anayofanya. Moja kati ya mambo yaliyofanyika kupata justification hiyo ni ile BIRTHDAY PARTY ya kutimiza miaka 18, na hata yeye mwenyewe alikuwa akipenda ijulikane hivyo ili tusihoji uhalali wa mtoto kuigiza na kuingizwa vitu vikubwa.

Sasa haya ya leo ni matokeo ya mafanikio ya usanii wa nyuma. Furaha ya nyani imeishia jangwani. Mabinti tulieni na wamama muache kuendekeza dhiki. Katika dunia ya leo, si ajabu kuona mama akimsapoti binti yake anayetembea na mume wa mtu na bila aibu huyo mama anaweza kumuita huyo mwanaume mpumbavu MKWE sababu tu ya vijisenti. Mama huyo si ajabu akawa wa mbele kanisani na binafsi asione shida mbele ya Mungu wake.

Lakini wakati tunayajadili haya ya Lulu, tukumbuke pia na yule marehemu naye ni mkora vile vile. Najua mtanuna kwa kuwa si kawaida ya wengi kumsema marehemu, lkn wote tufahamu hata yeye hakuwa sahihi. Wote tutakufa lkn juu ya nini ukafe kwa harakati za UZINZI.
 
Asante Angel.yaani mtu na akili zako unatuambia alisema ana 18 kwenye tv show au movie hiyo ndio proof ya umri wake?this is ridiculous!teenagers dunia nzima wanadanganya umri ili waingie club,wanunue sigara,wanunue pombe!tena kwenye nchi ambazo wako strict itakuwa Lulu!kadanganya ili apate driving license na passport aweze kusafiri(shwa) na kasaidiwa na watu wazima wasio na utu wala aibu....

kudanganya umri ili kupata:
Cheti cha kuzaliwa(kutengeneza kipya)
Pasi ya kusafiria
Leseni ya udereva
..................
..................
Vyote hivyo kisheria ni makosa, hivyo huyu binti bado ana kesi ya kujibu.
 
Back
Top Bottom