Lulu ana zaidi ya miaka 18 - Jamhuri!

Anavyo 2 na vyote vinautata 1 kinaonyesha kazaliwa moshi na kingine kazaliwa dar,na vyote vina majina tofauti,na hata wazazi wake wanatofautiana hospital aliyozaliwa.So ni usanii juu ya usani.

Tatizo wazazi walipanic kila mmoja katengeneza cha kwake bila kuwasiliana, baba akiwa Moshi chake na mama nae akielekezwa na walezi wa Lulu wakatengeneza kingine hapa Dar. Kazi kweli!!!!
 
kudanganya umri ili kupata:
Cheti cha kuzaliwa(kutengeneza kipya)
Pasi ya kusafiria
Leseni ya udereva
..................
..................
Vyote hivyo kisheria ni makosa, hivyo huyu binti bado ana kesi ya kujibu.

Ana kesi ya kujibu kudanganya umri ok,kwahio ni under 18 alifoji documents awe over 18!umri wake wa kweli uko kwenye birth certificate yake na records zake huko RITA sijui,hao RITA watoe cheti au record inayoonyesha kuwa ana 18 sio mtuambie mmemsikia kwenye TV na magazeti ya udaku akisema ana 18....mimi nina miaka 300 haya tangazeni tanzania mna oldest man alive!
 
Ushahidi mwingine alikuwa EATV kipindi cha friday night live alikiri kuwa eightee na kusema bado ni bikra na hana mpenz
 
Anavyo 2 na vyote vinautata 1 kinaonyesha kazaliwa moshi na kingine kazaliwa dar,na vyote vina majina tofauti,na hata wazazi wake wanatofautiana hospital aliyozaliwa.So ni usanii juu ya usani.
Hee....hii kali! Au umeongeza 'chumvi' mkuu?
 
Nyie mawakili wa serikali fuatilieni mambo haya ili kupata ukweli uliyo beyond the shadow of doubt: moja, kwa kuangalia alizaliwa hospitali ipi, ili makaangalie records zake, yaani toka mama yake anaudhuria clinic na siku ya kuzaliwa kwake na kuruhusiwa ila kama hakuzaliwa nyumbani. Pili, angalieni records za maendeleo ya mtoto kwenye clinic ya watoto under five aliyokuwa anahudhuria. Tatu, muombeni a-present kadi yake ya clinic when under five. Nne na mwisho, nendeni kule alikoanza kusoma hasa records zake za standard one and form one enrolments.

JK atakuwa kamwondolea aibu wakili wake Jaquina kwa kumteua kuwa jaji ila inaonyesha jinsi wakili hakuwa makini na sasa ndio jaji, je atakuwa jaji makini?

Lulu ana miaka 18 kabisaa, alisoma perfect vision na mie ndo nilimsajili. wakati anasajiliwa alikuwa na miaka 13 na hyo ilikuwa mwaka 2007 mwishoni alipokuja kuchukua form. sasa 2007 alikuwa na miaka 12 je 2012 atakuwa na miaka mingapi?? hii sintofahamu ya miaka imekuja tu baada ya huu msala wa kifo cha kanumba. hata ungekuwa wewe lazima ungetafuta pa kutokea
 
Mwacheni asote jela kwa kipindi chote atakachokuwa mahabusu. BInafsi nigependa afungwe ili liwe fundisha moja kati ya mafundisho mengi. Nchi hii tumezidi maisha ya kiujanjaujanja na uhuni kiasi kwamba ukiwa msafi unakuwa kama kituko. Mwacheni asote.
 
Mawakili wa Serikali bado amjawakilsha ushaidi sahihi mahakamni. Vyote hivyo ni picha na maongezi,
Ikiwa Lulu ana miaka 18, hii inamaanisha kazaliwa si muda mrefu uliopita, tusema mwaka 1994.
Ingawaje nchi bado ipo katika mazingira magumu ya data, na hii sio sababu ya kufikiria bado tupo
katika miaka ya giza. na ikiwa Lulu kazaliwa hospitali, kwa nini msifuatilie data za uzazi hospitalini
alikozaliwa. Sasa sisi wasikilizaji tuelewe vipi, ni uvivu au uzembe wa kazi.
 
Tatizo serikali yetu ya Jamhuri ni DHAIFU.
Kwa mtu kuwa na vyeti viwili vya kuzaliwa (Nyaraka za Jamhuri) na kuziwakilisha Mahakamani,Hilo tu ni kosa tosha la kughushi Nyaraka za Jamhuri. Ilitakiwa apewe takribani miaka 5 kwa hilo tu,ili wananchi tujifunze kuwa na adabu ya sheria za Jamhuri na Mahakama.

Kama ana leseni ya gari na pasi ya kusafiria (Nyaraka za Jamhuri) na zote akiwa ametia sahihi yake na vidole vyake kukiri kwamba yeye ana umri zaidi ya miaka 18,Nafikiri ni vyema na haki kwa Sheria ya Jamhuri kumchukulia kama hivyo. Hii itatufundisha wale wote tuliozoea magumashi...siku ikitokea bahati mbaya ndio utajua maharage sio mboga ni kiungo cha makande tu.
Tafakari!

Mkuu na wote waliowezesha kupatikana kwa hati hizo,wanapaswa kuchunguzwa uhusika wao katika kughushi Hati Muhimu za serikali kama ni kwa kupokea rushwa au ni kwa kutokuwa makini!
 
Anavyo 2 na vyote vinautata 1 kinaonyesha kazaliwa moshi na kingine kazaliwa dar,na vyote vina majina tofauti,na hata wazazi wake wanatofautiana hospital aliyozaliwa.So ni usanii juu ya usani.

Kumbe mtoto wa wasanii kawa msanii kama wazazi....lol....

 
Lulu ana miaka 18 kabisaa, alisoma perfect vision na mie ndo nilimsajili. wakati anasajiliwa alikuwa na miaka 13 na hyo ilikuwa mwaka 2007 mwishoni alipokuja kuchukua form. sasa 2007 alikuwa na miaka 12 je 2012 atakuwa na miaka mingapi?? hii sintofahamu ya miaka imekuja tu baada ya huu msala wa kifo cha kanumba. hata ungekuwa wewe lazima ungetafuta pa kutokea

Alikuwa ana 12 au 13?which is which?
Tuletee form alizojaza natumaini zitakuwa na maelezo ya umri kama hio shule iko makini.
Naomba utusaidie Mr Msajili.
 
Alikuwa ana 12 au 13?which is which?
Tuletee form alizojaza natumaini zitakuwa na maelezo ya umri kama hio shule iko makini.
Naomba utusaidie Mr Msajili.

Samahani Ni 13. nlishaondoka hapo siku hizi sina access na form hizo tena ndugu. Lakini pia papaa kadege ni mtaalamu wa fojari hivyo hashindwi kuleta form zikiwa zimefojiwa kuhusu umri mpya wa lulu
 
forensic people tumien carbon fourteen mtajua ana umri gani faster!! au tumieni nguvu za mabuti ya mwemaaaaa, kamata baba/mama ya toto weka ndani yeye taeleza wapi naundia hii toto!

Wakitaka kujua umri wake watumie carbon fourteen. Wachukue kucha zake na kuzipima.
 
Mimi nafikiri kama ni kosa basi hakuna kosa kubwa kama taarifa za uongo.

Imefika wakati sasa kuwepo na kitengo cha kutunza taarifa na ziwe sahihi na siyo za kubabaisha kwa sababu bila hivyo nchi yetu itafika mahali itahukumu watu vifo wakati hawahusiki.

Nasema hivyo kwani huko tulikotoka watanzania walio wengi wameendelea kutoa taarifa za uongo kwa ajili ya maslahi kadhaa binafsi kwa mfano iwe ni umri wa kumwandikisha mtoto shule, kupewa scholaship ya kwenda kusoma nje, kuoa, kuolewa, kupata kazi nk

Wakati huu Taifa linaandaa Vitambulisho vya Taifa nafikri finger print ndiyo jibu la mambo yote wale waliokuwa hawana kumbukumbu sahihi ya kuzaliwa kwao wakaape mahakamani na ushahidi wa finger print uwepo.

Hili la Lulu sasa ni kubwa kama alikuwa na vyeti viwili vya kuzaliwa kwa maeneo tofauti basi waliohusika wachukuliwe hatua kwani utatoaje cheti wakati humjui mtoto na hukumwona hii ni ile rushwa tunayoikataa

Bila kuwachukulia hatua hao tatizo litaendelea kuwa pale pale tunafuga ugonjwa ,kama Lulu aliweza kupata kazi kwenye kituo cha Luninga wakati huo bila kuangalia umri tunafuga ugonjwa kwa vyombo vinavyohusika na sheria za uajiri

Kesi hii iwe kama chachu ya kubadilisha mambo mengi maovu yanayoendelea hapa Tanzania
 
Asante Angel.yaani mtu na akili zako unatuambia alisema ana 18 kwenye tv show au movie hiyo ndio proof ya umri wake?this is ridiculous!teenagers dunia nzima wanadanganya umri ili waingie club,wanunue sigara,wanunue pombe!tena kwenye nchi ambazo wako strict itakuwa Lulu!kadanganya ili apate driving license na passport aweze kusafiri(shwa) na kasaidiwa na watu wazima wasio na utu wala aibu....

Hapa unataka kusema nini. Kutenda kosa na kutokugundulika hakuharalishi kosa. Maandishi na matamko yanayokuwa recorded yote ni sawa katika mkono wa sheria.
kama alitamka na akawa recorded, its an offence.
 
Back
Top Bottom