Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,212
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]

Alichoongea Lukuvi Kanisani

cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi akiwa mmoja wa wanamtandao anajua fika kwamba linapokuja suala la ubaguzi, Salim Ahmed Salim alibaguliwa na mtandao wakati wa mchakato wa urais ndani ya ccm (2005). Je hapa palikuwa na suala la serikali tatu? Tanganyika na CUF au Chadema? Hapana, kulikuwa na CCM, iliyoshinda baadae kwa zaidi ya 80%.

Salim alibaguliwa kwa lugha ya:
Hizbu, Mwarabu, Mpemba.

CC Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, MwanaDiwani, Ritz, Pasco, FJM, Nape Nnauye, Tumaini Makene, Mwigulu Nchemba

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Ndugu yangu hao Wakristo unawapakazia bure, Kiini cha CCM kung'ang'ania Serikali mbili ni kujiwekea Kinga baad ya kuiba na kupora Raslimali za Wanyonge na zingine kuhamishia ughaibuni....
Nimefurahia kwamba sasa ndo ule wakati muafaka wa wananchi kuchukua hatua kamili ya kujikomboa toka mikononi kwa mkoloni dhalimu CCM.

Ingawa huwa sikubaliani nawe katika mengi, ninaanza kuona kwamba umeanza kupata uelewa baada ya kuguswa suala la Imani ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Lakini tunapowambia CCM ni Janga la Taifa kwenye tasnia ya Kijamii, Kiuchumu, Kisiasa na Kimazingira nk...
 
Exactly. Kwa nafasi yake hakustahili kusema vile lakini nimempongeza kukiri kuwa yeye hana sifa ya kupindisha kwa maana kakiri na hakunukuu lakini kakiri. Kwa uoni wangu hata baadhi ya wajumbe mle ndani hawakufurahi maana kadhihirisha wazi chuki yake . Nimemuona Mh kingwala sura yake imenuna sana sio pengine kwa dini yake(ziwezi kujuwa hisia zake) lakini imewaharibia wale wenye ajenda ya kutumia UPOFU WA CCM ZANZIBAR KUENDELEZA MFUMO uliopo kuwa wanaweza kuelewa. Kinachonisikitisha mle ndani mna mashehe na Uamsho ambayo ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa kihalali, wanatajwa kuwa ndio CUF na kuwa ndio wanaleta hofu ya uislamu lakini wamekaa kimya. Niwaambie kwa hili LUKUVI ameamsha hisia za wazanzibari na kuwa na DOLA kusimtie kiburi. Hakustahili kuwataja uamsho pale tena kwa propaganda ile yeye ni kiongozi wa serikali. Katika namna ile LAZIMA WATU WATAAMI(NI MUUNGANO NI MFUMO KRISTO TU. Amezidisha TATIZO sasa SUBIRI HUO MOTO WAKE. Tuijenge Tanzania bila upendeleo wa kidini.
 
Lukuvi kachemka kwa kueneza siasa za udini ni hatari sana! kibaya zaidi amepewa nafasi ya ufafanuzi badala ya kuomba radhi na angalau kusema "walininukuu vibaya" kama kawaida yao, lakini leo bungeni kayarudia yaleyale kwa msisitizo zaidi hapo hana pa kuponea. Mh.Jakaya Kikwete, tafadhali tuondolee huyu mdini mara moja ikiwa kweli unajali amani ya nchi hii.
 
Katika viongozi ambao huwa najiuliza imekuwaje wakawa viongozi ni LUKUVI japo mimi ni mkristo lakini obvious amefanya kitu cha kipuuzi..kwenda kuongea masuala ya kisiasa kanisani huku akijenga hoja kwa mlengwa wa dini tena nyingine its totally a disgrace. viongozi wa namna hii wanalipeleka Taifa pabaya mno..Tuing'ang'anie Zanzibar kwa sababu wakiwa na serikali yao wataifanya nchi yao kuwa ya kiislamu! Kama wao wazanzibari wataona inafaaa kwao kwa maslahi yao kufanya hivyo baada ya wao kuwa nchi kamili sasa kuna ubaya gani? Kwa hiyo huu muungano ni wa lazima na utaendelea milele kwa sababu eti tukitengana nao watakuwa nchi ya kiislamu? Kwani mimi nikiamua kuvunja nyumba yangu ya tofali na kuamua kujenga ya chuma utanilazimisha nisijenge kwa sababu wewe hautaki? Hapa ndipo inapojidhihirisha misingi ya huu muungano si imara na upo tu kama kiini macho!!
 
Lukuvi akiwa mmoja wa wanamtandao anajua fika kwamba linapokuja suala la ubaguzi, Salim Ahmed Salim alibaguliwa na mtandao wakati wa mchakato wa urais ndani ya ccm (2015). Je hapa kulikuwa na suala la serikali tatu? Tanganyika na CUF au Chadema? Hapana, kulikuwa na CCM, iliyoshinda baadae kwa zaidi ya 80%.

CC Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, MwanaDiwani, Ritz, Pasco, FJM, Nape Nnauye, Tumaini Makene, Mwigulu Nchemba

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.

Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi and company wanadhania kwamba ushindi wa kura ya maoni kuunga serikali mbili kwa upande wa Tanzania Bara ndio utakuwa ni ushindi kamili. Wanasahau kwamba bao 1-0 itakuwa ni half time tu, watahitaji 2-0 kubeba point zote tatu kwa kushinda zanzibar. Hilo halitatokea, na kauli kama hivi makes matters even worse for CCM in Zanzibar. Bila ya kujua, anachofanya Lukuvi ni kuvunja muungano baada ya matokeo ya kura ya maoni kuwa 1-1.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Lukuvi akiwa mmoja wa wanamtandao anajua fika kwamba linapokuja suala la ubaguzi, Salim Ahmed Salim alibaguliwa na mtandao wakati wa mchakato wa urais ndani ya ccm (2015). Je hapa kulikuwa na suala la serikali tatu? Tanganyika na CUF au Chadema? Hapana, kulikuwa na CCM, iliyoshinda baadae kwa zaidi ya 80%.

Salim alibaguliwa kwa lugha ya:
Hizbu, Mwarabu, Mpemba.
Uchambuzi wako unaonyesha wazi kuwa tatizo ni ccm!
 
Bibie! Naamini kuwa wewe ni mmoja kuwa mmoja wa watetezi wa Ndugu JK! Swali langu ni mmoja je huyu rahisi anapotetea sirikali mbili je naye anabaraka za kanisa ili Zenji isiwe na mamlaka kamili. Ni kwa faida ya CCM au kabnisa
 
Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.

Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?
Kuna masuali mengi tu na wasiojuwa inabidi tuwaambie. Inaonekana wazi mh JK kalazimika kubadili msimamo katikati ya safari nadhani ni kwa hizi hofu za watu (Phobia) kama mtakumbuka suali la kadhi yule waziri Membe alipoitwa tu na muadham kardinali aligeuza msimamo kuhusu mahakama ya kadhi na JK naye alitoboa siri katika hutuba yake ya bunge kuwa kuna kiongozi wa dini mmoja ( anajulikana) alimpa ushauri wa serikali mbili na yeye kukubaliana naye kuwa bora tujaribu huo mtazamo wa mtu wa mungu. Jk kalazimika HAFLA KUBADILI MWELEKEO WA UMMA AMBAO ALISHAUJENGEA MATUMAINI KWA VITENDO VYAKE. kumbuka nani alimlazimisha kuleta mchakato kwani? kumbuka kauli zake za kuwataka watu wake wajiandae kisaikolojia, kumbuka jinsi alivyokwamua mchakato kila mawaziri wake walipopinga hatua za maridhiano? kumbuka kauli za kuhamasisha maridhiano na ile image yote ya kuipongeza tume ya WARIOBA leo ziko WAPI? hivi hamjajuwa tu? lazima kuna kitu na tayari picha imeanza kuonekana. Kwa mimi hata kama CCM wana maslahi yao kwa hili lakini na hili la upendeleo wa dini liko wazi.(Samahani kwa wale wakiristo) Haya ni mambo ya mjadala kwa sasa na kila kitu kina maana kipindi hiki. Tusidharau kitu. Hii kauli ya LUKUVI INATUCHONGANISHA SANA. Msitetee kwa ushabiki .Imeleta na kusadikisha kile ambacho siku nyingi kinasemwa huo ndio ukweli.
 
....hahahhaaaaa the white widow kaguswa na mkuki wa lukuvi kwenye dini, maovu ya ccm hayapo kwenye dini tu mpaka maisha yako ya sasa yanavurugwa kwasasbabu ya hofu ya ccm.....
 
Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Ndugu yangu hao Wakristo unawapakazia bure, Kiini cha CCM kung'ang'ania Serikali mbili ni kujiwekea Kinga baad ya kuiba na kupora Raslimali za Wanyonge na zingine kuhamishia ughaibuni....
Nimefurahia kwamba sasa ndo ule wakati muafaka wa wananchi kuchukua hatua kamili ya kujikomboa toka mikononi kwa mkoloni dhalimu CCM.

Ingawa huwa sikubaliani nawe katika mengi, ninaanza kuona kwamba umeanza kupata uelewa baada ya kuguswa suala la Imani ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Lakini tunapowambia CCM ni Janga la Taifa kwenye tasnia ya Kijamii, Kiuchumu, Kisiasa na Kimazingira nk...
tatizo mleta mada ni mdini sana inamana hujui kuwa uamsho ndyo wanaochoma makanisa?na haohao ndyo wanaodai jamhuri ya zanzbr mbona hujawahi kuwalaani wanaochoma makanisa.tatizo hamtaki ukweli .mi binafsi nataka serekali 1
 
WEWE faizafox ni mnafiki sana, na wala hujui unachokiongea, kwani huyo Lukuvi yupo chama gani na anaeneza Sera za chama kipi? unajifanya unauchungu na uislam hapo hapo unaunga mkono sera za chama ambacho kwa madai yako kina hofu ya uislam, poor you!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom