Rais Samia kuwateua Bulembo, Lukuvi ni maandalizi ya 2025?

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Uteuzi uliofanywa juzi na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwateua vigogo wanne wa kisiasa kumsaidia katika eneo la siasa na uhusiano wa Jamii umetafsiriwa ni "Kuimarisha safu kuelekea michakato ya kisiasa", hasa uchaguzi Mkuu wa 2025

Vigogo walioteuliwa juzi ni Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Balozi

Rajab Luhwavi, Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo na Waziri wa zamani wa Nchi, Ofi si ya Rais, Huduma za Jamii na Utawala Bora visiwani Zanzibar, Haji Omar Kheir.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa na kijamii walieleza kuwa mazingira ya sasa ya kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mchakato wa Katiba mpya na Uchaguzi Mkuu 2025, Rais ana- hitaii safu mahiri itakayowezesha kukamilika kwa mambo hayo salama.

Hata hivyo uteuzi huo pia unahusishwa na kutuliza hali ya mambo ndani ya chama tawala kinachadaiwa kukabiliana na misuguano ya kimakundi

Wachambuzi wanaeleza historia na uzoefu wa kisiasa wa wateule hao ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikalini vimechagiza kuteuliwa kwao. Hata hivyo baadhi ya watu wamewashauri wateule waifanye kazi hiyo kwa masilahi ya Taifa na kuepuka kujipendekeza zaidi 'machawa' kwa alivewateua, bali wamsaidie kwa ushauri sahihi na kumuambia ukweli.

Mhadhiri wa Rasilimali Watu na Utawala Bora kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Dares Salaam (TUDACo), Dk Lazzaro Swai alisema ubobezi wa walioteuliwa una-tosha kuifanya kazi hiyo.

"Ilimradi walioteuliwa wana ubobezi kwenye maeneo husika, wanatosha kuifanya kazi hiyo. "Siasa ni suala mtambuka, ukija kwenye uchumi kuna siasa, uhu-siano wa kimataifa kuna siasa, siasa za ndani pia zinahusiana na siasa," alisema.

Kuhusu idadi ya walioteuliwa, Dk Swai alieleza mtu mmo-ja hatoshi katika maeneo yote na walioteuliwa ni kutokana na uzoefu wao katika nafasi husika. Lakini, aliweka wazi kuwa uteuzi huo unalenga ajenda zijazo za kisiasa alizonazo mkuu wa nchi hivyo anahitaji wateule wamsaidie
 
Ndiyo. Anapanga safu ya ushindi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom