Kumbukizi: William Lukuvi akitetea ujenzi wa bwawa la umeme na kupingwa na Zitto Kabwe

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,770
15,248
Video hii inaonyesha namna aliyekuwa waziri wa aridhi wa awamu ya tano Mh William Lukuvi akielezea umuhimu wa nchi ya Tanzania kujenga bwawa la umeme ikibidi kwa fedha zetu wenyewe baada ya wafadhili kugoma kutoa misaada wala kukopesha.

Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na aliyekuwa mbunge wa Kigoma mjini wakati huo bwana Zito Kabwe kwa hoja kwamba mradi huo unaenda kuharibu mazingira na kwamba serikali ya Tanzania haina fedha za kutekeleza mradi huo hivyo ikimbilie kwenye gesi.


View: https://youtu.be/PFf5KzV8W4A?si=YiYOBptJ98tEUGag
 
Kwa mambo ya kisenge ya nchi hii, bwawa litakamilika, lakini umeme bado utakuwa sintofahamu, nchi hii ni shamba la bibi watu wanataka kupiga tu.
 
Namkumbuka Yule Jamaa Wa Utafiti Akasema Mradi Haufai Na Wafanyakazi Wa Mradi Wakanye Kilometres 2 Nje Wasijechafua Maji

Jiwe Kwenye Uzinduzi Wa Flyover Tazara Akasema Na Yule Aliyesema Wafanyakazi Wakanye Kilometres 2 Akabadili Andiko Lake Haraka Maana Anatumika Na Mabeberu

Asipobadili Tutanfanyizia Hii Nchi Ni Yetu Lazima Mradi Ujengwe Haraka
 
Back
Top Bottom