Lukuvi: Filikunjombe ni mtu wa CHADEMA

Lukuvi: Filikunjombe ni mtu wa CHADEMA

Samahani hapo kwenye red ndugu yangu, CUF?umeshawai kusikia mpinga hoja CCM wakamuita CUF wanasema huyu CHADEMA tu maana ndiyo wanaowanyima usingizi sasa

Hii mkuu ipo sana kwetu kule Mchambawima nafikiri unaelewa namaanisha nini.
 
Kwanin wasiseme Sitta, Mwakyembe, Magufuli ni wa CDM?
 
Wananchi wa Ulanga kwa Mfano wana athirika vipi na Matokeo ya Ubunge wa Arusha? Acha kuchanganya mambo wewe, hoja yako iwe Mbunge yoyote ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwahiyo ni mbunge watanzania wote, lakini kwenye maswala ya uchaguzi majimbo yanajitegemea, huwezi toka ulanga ukaja kupinga matokeo Arusha mjini ambako wewe hata hujaandikishwa kama mpiga kura! Usipotoshe maamuzi ya Mahakama ya Rufaa.
Mbona unajibu kwa jazba. Kwa kutanguliza jazba, hata imekufanya kutokuelewa nini nilichokuwa ninakisema kutokana na sababu zipi.

Nimepotosha nini hapo?. Kusema marumbano ya kisheria ni kupotosha.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...dbless-lema-iliyosomwa-disemba-21-2012-a.html
 
Waliokuchagua kwanza kabla ya blah blah za national politics.
Ndio maana ya kuwa Mwakilishi wa jimbo.

First things first.
Usijitoe fahamu.
Tatizo hukufuatilia mtiririko wa mabandiko kujenga hoja yako hii ambayo iko nje ya maana ya hoja yangu.
 
Tatizo letu kubwa ktk nchi hii ambalo litatusumbua kwa muda mrefu sana ni kwa Watawala wetu kufikiri kuwa adui wao mkubwa anayewanyima usingizi ni Chadema. Na kusahau kuwa adui mkubwa ambaye amesababisha Watanzania wengi tukose imani na Serikali ni umasikini unaowatafuna watanzania ambao ni wa kujitakia au makusudi kwa kuendekeza rushwa na ufisadi uliokithiri. Ambao kwa bahati mbaya sana umekosa Kinara wa kuukemea hadharani na kuukataa. Wote wako kapu moja na wameoza wote hakuna wa kumshutumu mwenzie kuwa umeoza. Maaana na yeye ataulizwa je na wewe?.
Watanzania kwa dini zetu zote tuombe Mungu atufikishe 2015 tubadili upepo huu usiambukize kizazi kijacho.
 
Haya ni maneno ya ujumbe wa Botswana kwa nchi ya Kenya in Kiswahili..
"Tuna ahidi kushirikiana na serikali yako kwa kuwa wananchi wa kenya ndio waliokuchagua na kuanzia sasa wewe ndiye Rais wao"
Kwani wewe huu ujumbe umeuelewa vipi?. Na umetolewa katika mazingira gani ya kisiasa. Halafu pia maandiko au mawasiliano ya kidiplomasia huwezi kuyachanganya na lugha ya sheria ya ndani ya nchi.
 
Kwa hiyo yeye michango yake ni kwa wananchi waliomchagua?. Duh. Vipi wale ambao hawakumchagua?.


Ngw'amapala una ubongo wenye kasi mno kukimbiliakutoa tafsiri nyembamba kwa maneno mapana. Hiki ndicho kilichodhihirika katika tafsiri yako hapa. Nimesikitishwa sana!
 
Ngw'amapala una ubongo wenye kasi mno kukimbiliakutoa tafsiri nyembamba kwa maneno mapana. Hiki ndicho kilichodhihirika katika tafsiri yako hapa. Nimesikitishwa sana!
Uniwie radhi mkuu kama nimekukwaza na mikwaruzo ya kisiasa.

Sikujenga tafsiri nyembamba bali nilikuwa ninaweka sawa tafsiri inayolenga kujenga ubaguzi wa kisentesi uliojificha katika utumishi wa umma.

Mbunge anapaswa awatumikie wananchi wake na siyo wapiga kura wake.
 
Akihojiwa asubuhi hii na kituo cha redio cha Ebony FM mkoani Iringa juu ya maneno ya Mh. Deo Filikunjombe juu ya wabunge kuingilia kazi za Nape Nnauye, alohoji: "Unamaanisha mtu wao?" (akimaanisha wa CHADEMA), kisha akasema "sisi ndio tunajuana vizuri mle ndani".

Lukuvi ni kati ya Mafisadi wa elimu dunia...ndio maana wote tunajua IQ yake na fikra ni minus, kati ya wale watu wa kusogea kwa 'mbeleko'...hatuna la kumhoji!
 
Hapa kazi ya kumpiga chini Deo na kumpa kiti Pindi imeanza kuchukua kasi...Hakuna anayefikiria mantiki ya anachokisema Deo. Watamwita kila jina na kumuhusiha na kila chama ila "wanamtandao" wameanza kumsafishia njia Pindi Chana Ludewa 2015 kwa tiketi ya CCM.

Ataenda CDM happ mtampiga chura teke
 
Akihojiwa asubuhi hii na kituo cha redio cha Ebony FM mkoani Iringa juu ya maneno ya Mh. Deo Filikunjombe juu ya wabunge kuingilia kazi za Nape Nnauye, alohoji: "Unamaanisha mtu wao?" (akimaanisha wa CHADEMA), kisha akasema "sisi ndio tunajuana vizuri mle ndani".

Mkuu hapo ni lugha gongana za mnara wa baberi, Jana katibu wao Kinana akiongea ziarani Ludewa? aliwahimiza wana CCM waisimamie serikali, kwa maana waikumbushe na kuikosoa inapoenda mrama.... leo LUKUVI nadai wanao ikosoa ni wachadema tu.... Thanks God mnara karibia unaanguka
 
Kwa hiyo Kikwete ni Rais wa wananchi ambao walimchagua tu? Katika demokrasia alieshinda ndie aliechaguliwa....na hakuna tena wa kusema sikuwepo...sikumchagua....kidemokrasia tunasema waliomchagua!

Mkuu usichanganye vitu hapa. Kikwete ni rais wa nchi ni kiongozi wa watu wote ila Deo ni mwakilishi wa Ludewa, nako huko ludewa kuna waliomchagua na wasio mchagua lakini anawawakilisha wote ila katika jimbo lake tu. Hayo ndo anayoyatetea yeye na yupo sahihi sana. Majimbo mengine nayo yana wawakilishi ni jukumu la wawakilishi wao kuwatetea kama hawafanyi hivyo hilo ni tatizo la wawakilishi wao. Sasa nyie mnapotaka mbunge mmoja awasemee na wengine hiyo sio sawa unless ni jambo la kitaifa. Lakini mh. Deo amewasemea wananchi wake vitu viwili 1. Barabara ya lami na 2. Meli aliyoahidi rais. Kwisha
 
Demokrasia ya wapi hiyo?.

Hawa ni wawakilishi wa wananchi na siyo wawakilishi wa wananchi waliomchagua. Hii tofauti ina maana kubwa sana katika demokrasia ya kweli.

Mkuu ni kweli ni wawakilishi wa wananchi wote waliomchagua na wasiomchagua lakini katika jimbo lake. Unless kuwa na jambo la kitaifa ndo anawajibika kutetea wananchi wa nchi nzima. Hii ndio sababu tuna majimbo tofauti na hata ukifuatilia sababu za uanzishwaji mikoa na wilaya mpya utapewa hii sababu " ili kuwapelekea wananchi maendeleo na uwakilishi wa karibu". Mh. Filikunjombe hana wajibu wa kuwatetea wananchi wa nje ya jimbo lake kwa mambo ambayo si ya kitaifa maan hao wananchi wana wawakilishi wao wenye hadhi, mamlaka na jukumu kama la Deo.
 
na ndo tutambue hawa watu ni wa aina gani,hawako kwa ajili yetu.Eti tunajuana mle ndani na ndio maana kwao ni sawa kabisa kwa hali walonayo watanzania na nashangaa sana watu wanawashabikia wakati wao hawamo ndani maana wapo wenye ndani yao na hiyo ndani ni kwa ajili yao wenye tu na wenye ndani hiyo wana sifa na hulka ya aina moja na ndio maana Bwana Fili sio mmoja wao kwa kua anagusa pabaya kila wakati, na kwa hilo tu atakua nje ya undani huo aliouzungumza,watanzania tutambue thaman ya utu wetu maana kauli zao tu ni kipimo tosha cha kujua utashi na malengo yao,,maana neno huashiria kile kilichoujaza moyo wa mtu(undani)
 
Filikunjombe anafanya na anatimiza kile anachopaswa kufanya kama mbunge(kuwakilisha wananchi wa jimbo lake, kuikosoa na kuishauri serikali). Kungekua na wabunge kumi tu wa ccm wakatimiza majukumu yao kama mheshimiwa Filikunjombe hakika serikali ingekua inaona aibu na kutekeleza ahadi zake.
Tatizo ni mfumo mbovu wa chama tawala uliojijengea kwamba hakuna mbunge wa chama tawala anayetakiwa kupinga hoja yoyote ile ya mbunge kutoka chama tawala na kupinga kwa nguvu zote hoja za upinzani hata kama zina maslahi kwa taifa. Mfumo huu umewafanya wabunge wa ccm wawe wazembe na kudumaza uwezo wao wa kujenga hoja maana hata wasiposhauri kitu serikali kwa upande wa chama chao wanaonekana wamefanya la maana zaidi kuliko kuongea na wapinzani kupata hoja.
MANENO YANGU KWA MH. FILIKUNJOMBE; Kazi unayoifanya wananchi wanaiona, Ccm wakikufukuza au kukuengua katika kula za maoni 2015 kwa kutimiza majukumu yako kama mbunge ndani ya Bunge,gombea kupitia upinzani na nauwakika utakitetea kiti chako hata kwa kuwa mpinzani wao
 
Lukuvi hana Elimu ya juu...lakini ni mtu mwenye busara na uzoefu wake katika uongozi umemfanya kuwa bora kuliko hata baadhi ya wasomi wanaojisifia usomi wao.....
Yup; unataka kusema elimu yake pamoja na kwamba si ya chuo kikuu inamzidi ya yule Dr. wa kubumba na kubumba a.k.a. fastjet au msafiri morimori?
Kama ndivyo basi hongera kwa utafiti uliotukuka ingawa kuna lundo la wanaofanana fanana ndani CCM.
 
Inatia moyo kuona kwamba kumbe kila mwenye itikadi ya kutetea wanyonge na maono ya kuikomboa nchi anaitwa "wao" a.k.a chadema
 
Jamani nadhani huu upuuzi wa CCM lazima tufike hatua tuseme baasi sasa nibora nchi ikaongozwa kijesh kamda dhan hii hali maana sikuzote ukweli ni ngum kuupokea msemakweli huwa hapendwi na wachache na uchaguzi ujao Filikunjombe lazima apite iwe kupitia CCM AU CHADEMA maana anauzika yule.
 
Mkuu ni kweli ni wawakilishi wa wananchi wote waliomchagua na wasiomchagua lakini katika jimbo lake. Unless kuwa na jambo la kitaifa ndo anawajibika kutetea wananchi wa nchi nzima. Hii ndio sababu tuna majimbo tofauti na hata ukifuatilia sababu za uanzishwaji mikoa na wilaya mpya utapewa hii sababu " ili kuwapelekea wananchi maendeleo na uwakilishi wa karibu". Mh. Filikunjombe hana wajibu wa kuwatetea wananchi wa nje ya jimbo lake kwa mambo ambayo si ya kitaifa maan hao wananchi wana wawakilishi wao wenye hadhi, mamlaka na jukumu kama la Deo.
You nail it. Dude.

Nimekumbana na watu wengi kwa kutokutambua kutokana na mazoea ya kimatamshi, wanashindwa kutofautisha maelezo uliyoyatoa.

Thanks
 
Back
Top Bottom