Lukuvi: Filikunjombe ni mtu wa CHADEMA

Lukuvi: Filikunjombe ni mtu wa CHADEMA

Kwa hiyo Kikwete ni Rais wa wananchi ambao walimchagua tu? Katika demokrasia alieshinda ndie aliechaguliwa....na hakuna tena wa kusema sikuwepo...sikumchagua....kidemokrasia tunasema waliomchagua!
Demokrasia ya wapi hiyo?.

Hawa ni wawakilishi wa wananchi na siyo wawakilishi wa wananchi waliomchagua. Hii tofauti ina maana kubwa sana katika demokrasia ya kweli.
 
Hapa kazi ya kumpiga chini Deo na kumpa kiti Pindi imeanza kuchukua kasi...Hakuna anayefikiria mantiki ya anachokisema Deo. Watamwita kila jina na kumuhusiha na kila chama ila "wanamtandao" wameanza kumsafishia njia Pindi Chana Ludewa 2015 kwa tiketi ya CCM.
 
Samahani hapo kwenye red ndugu yangu, CUF?umeshawai kusikia mpinga hoja CCM wakamuita CUF wanasema huyu CHADEMA tu maana ndiyo wanaowanyima usingizi sasa
Hawawezi kusema CUF kwasababu sio chama cha upinzani. Chenyewe nisehemu ya serikali na CCM ndio maana wabunge wake sasa hivi wako kama wagonjwa walio kwenye comma!
 
Msema kweli siku zote ni Mpenzi wa Mungu na ukweli siku zote unauma. Filikunjombe ni mzalendo isipokua amevaa kiatu ambacho sio chake (CCM). Wakati ufiki akivue! Nakufunika kwa Damu ya Yesu akuepueshe na wabaya wako.
 
Lukuvi ni Fisadi wa Elimu! Ni mwalimu wa UPE! Ni swahiba wa JK tangu wakiwa Nachingwea!

Anadai ana Diploma ya Russia! haifahamiki alisomea kitu gani! wala mwaka aliosoma haujulikani!!

ushahidi zaidi soma kitabu cha "MAFISADI WA ELIMU" cha kainerugaba Msemakweli
 
Lukuvi anatenga masaa matatu kila siku kukariri kanuni za Bunge ili aweze kutoa taarifa,kuhusu utaratibu na muongozo wa spika! Jamaa ni kilaza kwa maana halisi!
 
Dear Lukuvi, Mzindakaya alikuwa upinzani? What about Mama Malecela? Steven Nandonde je Kimbau? Hivi kwenye Chama chako mtu mwenye mawazo tofauti/mbadala ni mpinzani? Hiyo ndiyo new version ya demokrasi huko CCM? Chama kitakuwa na afya njema kama wote mtakuwa na mawazo ya kufanana?
 
Mataifa makubwa kama USA na RUSSIA kuna vipindi walitaabika sana kutokana na Uasi/double Agent uliokuwa unafanywa na Wanausalama! Tafiti zilizofanyika zinaonesha kuwa wanausalama wasipodhitiwa wanaweza kuiangamiza nchi kutokana na magonjwa ya akili ambayo huwapata wakiwa makazini, ndo maana wenzetu huwa wanachagua watu wenye processor kubwa siku zote!
Tatizo la lukuvi et al Wanaugua magonjwa ambayo huwapata wanausalama wengi, wengine hujikuta wanawatesa hata wake ama waume zao! CCM wameona ni vema kuwatumia hawa wagonjwa katika kukabiliana na mabadiliko ya kisiasa yanayoletwa na CHADEMA!...Ndugu zangu lazima mtambue kuwa a lunatic person can destroy even his/her own opulence...
 
subutuni kumtimua muone?
Anatua chadema men
na anashinda mem
 
lukuvi hana elimu ya juu...lakini ni mtu mwenye busara na uzoefu wake katika uongozi umemfanya kuwa bora kuliko hata baadhi ya wasomi wanaojisifia usomi wao.....

kuwa wazi bro hebu tupe japo mifano miwili tu ya ubora wake na faida zake kwa watanzania!!
 
Lukuvi ni Kilaza

Mwambieni Lukuvi kuwa Filikunjombe ni mbunge makini sana asiyependa ushabiki. He knows ni kwa nini yuko bungeni. Hongereni sana wananchi wa Ludewa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ila namuonea Huruma sana Filikunjombe, Maana hata Horace Kolimba ilianza hivi baadaye Usalama wa Taifa ukafanya kazi yake kama kawaida

Kazi ya kung'oa kucha na meno?
TIS.. NI JANGA LA KITAIFA.
 
Nadhani kuna umuhimu wa wanasiasa wetu kupewa semina kuwa kila mmtu ana haki ya kutoa maoni yake na mwanachama mwenzio akikosoa mwenendo wa chama hadharani au kwenye vikao vya ndani ni bora zaidi kuliko kueleza mafichoni kwa chama pinzani ambapo tunasema ni unafiki. Filikunjombe hakupenda unafiki ndiyo maana akaweka wazi vivyo hivyo Mwalimu Nyerere alikuwa anakosoa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali na chama waziwazi ushahidi ni kitabu cha Miongozo miwili Kupaa na kutunguliwa kwa Azimio la Arusha kilichotolewa kwenye tamasha la mwalimu pale UDSM hivi karibuni. Pia ni jana tu nimeona kwenye habari TBC1 Kinana akiwaambia wana ccm kuwa ni lazima kuikosoa serikali na viongozi wa chama pale wanapokosea na kukipongeza wanapofanya vyema. Hivyo sioni kosa la huyu bana mdogo Filikunjombe.
 
Hawawezi kusema CUF kwasababu sio chama cha upinzani. Chenyewe nisehemu ya serikali na CCM ndio maana wabunge wake sasa hivi wako kama wagonjwa walio kwenye comma!


sio cuf, sema Cuf na Nccr si vyama pinzani
ila CHADEMA ndio chama pinzani.
(sera kubwa ya wakoloni weusi/magamba ni kuidhoofisha CDM ng si kuwatumikia wananchi)
 
Back
Top Bottom