Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Itabidi sasa hata viongozi wanaotuhumiwa na ufisadi watengwe na jumuiya za dini zao na kufanyiwa maombi maalumu Mungu awaadhibu na familia zao, maana hii kusafishana kwa serikali ya ****** sijui kutaisha lini.

Mimi nasema hata kama hakuna taasisi 20 ila zilichangwa hela ambazo nikijumlsha haraka haraka naona kama ni mil 518. Ambazo kwa haraka haraka ni kama madawati 3,453 (518m/150,000) tena madawati ya kisasa kabisa.
 
kama pinda aliweza kutoa hukumu palepale, na Shelukindo aliweza kuongea kwa machungu namna hiyo basi mimi binafsi nawaomba hawa waheshimiwa watoe tamko lao kuwa wao watashikilia msimamo wao huo wa jairo kufukuzwa kazi...vinginevyo wajiuzulu na waachane na siasa maana hawatatufaa kama ndio wanaongea kwa hasira halafu wanageukwa na KikweteKikwete
 
Reactions: Ame


yeah nimesikia kwenye habari zilizovunjikavunjika za ITV mida ya mchana... hivi jamani niambie haya tuseme kuwa haikuwa rushwa ni kuchangia watendaji wa wizara kwenda kushughulika na bajeti bingeni.. hivi ndio zichangwe milioni 500.....

Kha hivi kwa matumizi gani ya kufikia pesa hiyo.. hata hao watendaji wangekuwa 100 na hata kama hilo bunge lingefanyika uswis bado gharama zisingefika huko.. haya sasa masikhara yaani gharama za kwenda kusoma bajeti kwa watendaji wa wizara zifikie milioni 500.

Yaani kama wamemchomoa jairo huko. basi wizara nzima pamoja na waziri wake waadabishwe kwa ufujaji wa makusudi.. watoe takwimu za matumizi ya hizo mil 500 walitumiaje au watazitumiaje.....

HII INCHI NAHISI TULIVAMIA ENEO LA MAKABURI HAIWEZEKANI WATU WANAJIFANYIA MAMBO WANAVYOTAKA TUINAWAANGALIA HKU SIO KULALA NI KUWA MFU.. ngoja nikaangalie ramani ya AFRIKA vizuri pengine hili eneo lilitengwa kwa ajili ya makaburi na ss tumelivamia nakuweka makazi ndio maana tunakuwa mazezeta kiasi hiki.
 
I have no comment! kila mtu ni kula tu kwa kwenda mbele. Naota vurugu zaja nchini.
 
Hii serikali inatupeleka wapi sasa. Mtu ambaye ametuhumiwa kwa uwazi kabisa anarudishwaje tena kazini. It beats me!

Leo imekuaje tena Mwita25 tuko pamoja kwa hili? sababu wewe kila kitu chenye manufaa hua unapinga,hongera na uendelee hivi hivi,issue hapa lipigwe dude nchi nzima kushinikiza gvt iwachukulie hatua wezi wote wa nchi hii
 
Hao ndio viongozi wa Bongland! kama kweli ucchunguzi wa kina ungepita jairo asinge survive maana anazo tuhuma nyingi za wizi na ufisadi achilia hizo tuhuma za Mhe. Beatrice Shellukindo.

Vyombo vyetu haviko makini kabisa ndio maana kila mtu anafanya anavyotaka! Hivi Luhanjo anastaafu lini? JK kwanini anambeba huyu mzee? Kila siku anaongezewa mikataba ina maana hatuna young blood kushika nafasi hiyo?

Tumemchoka Mzee Luhanjo anatupeleka kubaya! yeye na jairo lao moja na wanakula pamoja ndio maana kesi ya ngedere haiamuliwi na nyani.
 
Ningekuwa mimi namfukuza kazi mara moja - PM

Naunga mkono hoja, lazima baraza la mawaziri livunjwe na kumuondoa PM. Huwezi kukaa na PM anayetoa matamshi ya rejareja ya jinsi hii tena bila kufanya utafiti wa kina. Kuendelea kubaki naye rais atakuwa anajitukanisha mbele ya anaowaongoza na mbele ya jairo.
 
Mmmh!!! Hii ni balaa, yaani hii nchi sijui vipi!!
 
Mods naomba ruhusa nitukane kidogo tu, japo kidogo tu nisjekufa kwa presha....pls nasubiri.
 

Now i can agree with you
 
foolish!ni kweli tunadharauliwa kiasi hiki
 
haaa!
yan majameni tukiipitisha tena hii mijitu, tutauzwa completely
 
? Jamani ni kweli nime confirm hapa Tbc1 Jairo kesho anarudi kazini kwamba tuhuma zilikua si za kweli,dah! najisikia tumbo kuuma kabisa,hivi kweli tutafika ndugu na hii hali
 
Wabunge wa CDM, CUF NCCR , TLP jitokezeni mseme mkiwa bungeni huko zaidi ya wizara ya Jairo mmepokea na kuvuta pesa za "mawasiliano ya bajeti " za wizara gani. Mkisubiri serikali ijipange jinsi ya kujibu mapigo na jinsi ya kuremba hiyorushwa mtaumbukaaaaaaa
 
JF jukwaa la siasa halina uzushi umbea ni michuzi huko na viblog vya udaku pole sana aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…