Luhanjo kamsafisha David Jairo hana tuhuma yoyote ya Rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Luhanjo kamsafisha David Jairo hana tuhuma yoyote ya Rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Arafat, Jul 24, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  "...Jairo ambaye yuko chini yake, analazimika kwenda likizo kuanzia juzi ili kupisha uchunguzi wa awali ambao unalenga kubaini iwapo ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zinazoongoza Utumishi wa Mmma.(Philemon Luhanjo kwa mujibu wa nukuu ya Gazeti la Mwananchni)

  Kwa mijibu wa hii kauli ya Luhanjo uchunguzi unaofanyika hauna haja na ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa sababu makosa aliyofanya Jairo yameshapindishwa na si ya rushwa tena na hamna uchunguzi wowote wa rushwa dhidi yake, hivyo kamsafisha na tuhuma za rushwa, wanachofanya sasa ni kumpaka mafuta tu!

  Kwa mujibu wa Sheria Na.6 ya 2001 (Public Finance Act) hakuna kosa watakalo mkumba nalo Katibu Mkuu wa Wizara maana yeye ndio Accounting officer wa Wizara na fedha yote ya serikali katika wizara husika ipo chini yake, yeye ndiye mwenye VOTE ya ku-control fedha hizo na matumizi yake hivyo matumizi yeyoye atakayofanya ili mradi yawe na lisiti halali ni sahihi na haki; swali lililo baki hapo na wanalotaka kuja nalo ni kama hayo matumizi si halali au la! Ni kazi rahisi sana, kuwa na lisiti za soda na hotel walizolipa zenye gharama sawa na matumizi yaliyofanyika sidhani kama inawashinda hawa watu ambao hawana hata chembe ya aibu katika nyuso zao.

  View attachment 34348
  Wanacho angalia watu wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu ni kile kinachoitwa "General accepted accounting practice" yaani kama matumizi yaliyofanyika yakitunzwa vyema ki-hasibu na gharama zake ni bei halali ya soko huo ndio utakao kuwa mwisho wao, swali kwanini hawaku institute uchunguzi wa tuhuma ya rushwa? badala yake Luhanjo anaenda mbali hadi kusema kosa la kinidhamu! Kusema kosa la kinidhamu tayari ni kumsafisa na makosa ya kijinai ambayo ni fraud na corruption.

  Ushauri wangu kwa serikali, badala ya kupoteza fedha zaidi kumpaka mafuta Jairo, rais atangaze kuwa Jairo hana kosa na kuwa anampangia kazi nyinge maana haina jinsi yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na Majeshi yote bado yana mtii na kumpigia Mizinga hasiwe na shaka apunguze matumizi yasiyo lazima katika uchunguzi ambao tayari wameshau elekeza katika dimbwi, awe wazi na atangaze maamuzi yake juu ya Jairo, Pia Pinda kwa mujibu wa maelezo yake bunge alisema Jairo ni wakufukuza tu, ila anamsubiri rais sasa asimamie maneno yake ajiuzulu kama kweli hana unafki katika maneno yake na matendo yake akae pembeni maana ukitofautiana mtazamo na mawazo kiasi cha kuoneka kama hivi ni bora kupisha hili husiwe sehemu ya usafi au uchafu huo unao upinga.

   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  My foot this country!!!

  Siku hizi kila niki-log inn JF natoka kicchwa kinawaka moto!!
   
 3. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  unazijua sheria za kazi wewe? luhanjo alifafanua kwa kirefu sana hili.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  tuone kama majirani wa kule ada estate watapigana vikumbo!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hizi sheria zina apply kwa baadhi ya watu tuuu eennh!! tena Vigogo
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya maneno hayana ukweli kabisa. Hakuna kitu - General accepted acoounting practice, ambazo hazifuati malengo yaliyopitishwa ktk matumizi ya fedha hizo (allocated). Huwezi kutumia fedha za mafuta ukatoa receipt za Hotel na malazi ulokwenda kujichana wewe na kimwana ati kwa sababu tu wewe ni katibu mkuu kisha unadai una mamlaka yote. Na zaidi ya yote haya basi tusingekuwa tunapitisha bajeti bungeni isipokuwa waziri na wizara yake wanapewa Kitita cha fedha ktk account kisha wao wataamua wazitumie vipi..

  Tunajua Jairo hawezi kusimamishwa kazi wala kuwekwa hatiani kwa sababu wanapokea fedha hizo za posho ni wenyeviti, makatibu, wajumbe, na sekretaiet ili kupitisha bajeti ya wizara na ni utamaduni uliokuwepo miaka nenda rudi. Barua hiyo hiyo mnayotaka kumwadhibisha Jairo imejieleza wazi kupanda kwa posho hizo.

  Sasa yawezekana Bi. Beatrice alivamia mti bila kujua ndio makazi ya chui. Nia na lengo lao ni kumtupia lawama Jairo mshikaji wa JK kumwokoa Ngeleja na Malima kambi ya Magamba. Kushtuka kwa Pinda na viongozi wengine wotee ni kwa sababu hawakutegemea mkenge alolishwa Beatrice ungewaumbua wengi na hasa kundi la watu waliokusudiwa. Hata hivyo kusafishwa kwa Jairo sio kwa manufaa yake bali kwa manufaa ya wabunge ambao walikuwa wakivuta na walitaka kuvuta fedha hizi isipokuwa sasa ni wakati wa kumalizana wakijipanga kwa mwaka 2015..

  Just imagine wizara moja ya nishati walitakiwa kuchanga karibu millioni 190 kwa ajili ya posho hizi bado wizara ntyinginezo na hutjamsikia waziri wala katibu mkuu yeyote toka wizara nyingine akishangaa! HAKUNA kwa sababu ni general practice bungeni kutoa posho ambazo fedha zake kuchangishwa toka taasisi mbali mbali acha mbali matajiri wanaofuatilia tender..

  Inaweza kuwa ngumu kweli kumweka Jairo hatiani kwa sababu fedha hizi huchangishwa, na kama sikosei kwa muda mrefu sasa hivi wizara zote mwisho wa mwaka wa matumizi huwa ktk deficit yaani wametumia zaidi ya kile walichopewa kwa bajeti ya mwaka 2010/2011 na hapa walipo wanasubiri mgao mpya wa 2011/2012. Hiyo michango haipo ktk mfuko wa wizara na pengine hushughulikiwa nje ya vitabu vya wizara wakiwatumia mawakala wa kulobby.
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bado sijapata picha: Huyu Jairo kasafishwa lini na Luhanjo? Mtoa hoja atufafanulie vizuri hapa!
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Mleta mada hujui kitu.. Hata kuandika risiti hujui. Nenda ama rudi shule
   
 9. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,648
  Likes Received: 5,241
  Trophy Points: 280
  Teh! Hii ndo'tanzania zaidi ya uijuavyo! Ndo'maana mwisho wa cku alipata hadi confidence ya kunena kuwa "wabunge kama ze comedy"???
   
 10. h

  hittler Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo madhara yakuongozwa na kundi washkaji hawajui walifanyalo ila aibu itawakumba siku za usoni. Mzee Luhanjo amezeeka hakumbuki wala hana habari na maslai ya taifa
   
 11. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Like sand in Grass this is Days of our Lives.Time will tell.
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NI KWELI JAIRO HANA HATIA HATIA IKO KWA JK NA WABUNGE WALIOZOEA KUHONGWA ILI KUPITISHA BAJETI MBOVU

  nyAMBAFU HATA HUYO SHELUKINDO FUNGU LILIMPITIA PEMBENI THIS TYM AKAAMUA KULIPUA ILA MKUMBO HUO HUO
   
 13. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Ndio nchni yako Mkuu, Kumbuka waliapa CCM nitakulinda mpaka kufa badala ya kuapa Tanzania nitakulinda mpaka kufa! Hawa ni watu hatari kwa Taifa hili.
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Nazijuwa sheria za kazi kuliko unavyofikiria wewe, tupe sehemu inayokataza kumchunga na tuhuma za rushwa!
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Na hapo ndipo swala la kumpaka mafuta linapo anzia, assume hakuna records ya hizo fedha katika vitabu vya serikali then, jibu rahisi sana watakalo towa ni kuwa hayo maneno ni ya uongo na uzushi mtupu, ni wivu wa kijinga kwa Jairo.

  Ndio maana nimekwambia hawa wana-angalia accounts za Serikali kama zina kasoro yoyote kutokana na hiyo tuhuma.
   
 16. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #16
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii nukuu mbona kama imechakachuliwa vile, sio 'Like sands through the hourglass so are the Days of our Lives..'​ mwongozo wako tafadhali
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Kasafishwa kutoka katika tuhuma ya rushwa kuja kwenye finance audit ambayo ni ukaguzi wa accounts na kuangalia kama kuna kosa la kinidhamu alilolifanya, kama ikiwa hizo fedha alizo kusanya zitaonyeshwa vyema katika vitabu au kama ikiwa wanajuwa jinsi walivyozikusanya na kuwa hazionyeshi kasoro yoyote katika vitabu vya hizo taasisi basi hana kosa tena.
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  We una elimu gani? Nadhani matatizo ya elimu uliyonayo ndio yanakufanya huelewi na baya zaidi huelewi kuwa huna elimu.
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ndio maana tulitaka tuhuma iwe ya rushwa na uchunguzi ufanyiwe juu ya rushwa, kitu ambacho kinge wabana pia na wabunge wanaongwa, lakini sasa ni kama wanapooza swala husika.

  Maana kama wabunge wanapitisha bajeti kwakuhongwa unadhani hiyo Bajeti ipo kwa Maslahi ya nchni kweli? Ingelikuwa ni busara kufanya uchunguzi wa rushwa ili wote Jairo wabunge wetu wana hongwa wapate haki yako chini ya sheria ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma.
   
 20. L

  Lua JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi kuhusu jairo mnategemea jipya gani kutoka kwa magamba.
   
Loading...