Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.

===========
UPDATES:

Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil

More updates to follow

Hapo kwenye msimbazi, hebu atuambie walilipia kwa kutumia nini? Tunataka tujue gharama za chakula na malazi ni kiasi gani? Hawa wakisafiri huwa wanapewa Imperest, sasa wanalipwa vipi tena na EWURA.
 
Inarahisisha kazi ya CDM kufika 2015,endelea kuharibu ****** ili tupate justifications nyingi za kukupindua juu chini kama wajinga wenzio huko kask
 
IF SOME ONE IS THINKING DIFFERENT FROM YOU DOESNT MEAN HE/SHE IS WRONG.
JAMANI TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MTUHUMIWA NA MKOSAJI...HUO NDIO UTAWALA WA SHERIA...TUACHE SIASA UCHWALA ZINAKWAMISHA SANA MAENDELEO YETU...MMEAMBIWA
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti SASA HAPO MNATAKA NINI? KWANI HUO NDO UTARATIBU WA KUPITISHA BAJETI ZA WIZARA ZOTE...ISHU SIO JAIRO...ISHU IKO KWENYE UTARATIBU
 
Bajeti ya wizara ni Tshs 1.2trilion, these guys spend Tshs 500million for facilitation and these top fellow just sits there with his gray hair and says its okay to spend that much to get the budget passed by NA?? Damn it!

You came out with good narration but poor analysis to support your perception.The facilitation is just 0.04% of the budget.I hope you can use the analysis to finalise your comment.
 
Shelukindo ndiye aliyeharribu sakata zima; kuhamisha fedha za serikali kwenda kwenye akaunti za serikali ni ngumu sana kuifanya iwe ufisadi Kama wezi wa EPA wangechukua zile bilioni 133 na kuziingiza kwenye akaunti ya wizara ya afya au elimu sidhani kama watu wangesema ni ufisadi. Labda improper yes lakini corruption the bar is very high. Shelukindo hakutaka watu wakamatwe.. vinginevyo angesubiri wabambishwe.

Nahisi hakuharibu ila ilikuwa strategy ya kuwa preempt opposition...pengine walishapata habari kuwa hilo bomu lingelipuliwa ikabidi walitegue! Magamba wanaakili wewe acha mchezo sijui hiyo akili kwanini hawaipelekagi kwenye kuendeleza nchi...
 
Tuhuma hizo zilikosa uzito gani? Nadhani kwa sababu hatujui ripoti imesema nini inakuwa vigumu kulizungumzia hili suala.

Ila kutokana na hali halisi, yaani, maneno ya Waziri Mkuu bungeni na kwamba kutakuwa na kutafutana mchawi kati ya Jairo na wafanyakazi wa Wizara si busara kumrudisha wizarani! Waziri Mkuu ni bosi wake! Alimhukumu kabla ya kujua ukweli. Wafanyakazi wa wizara ndio waliomuuza kwa kina Shelukindo. Ni bosi wao!

Hii nchi ina mapungufu kila upande. Kwa wanaotaka mabadiliko na walioko madarakani. Wote wana mapungufu makubwa. Wote wanataka sifa kwa kutotenda au kutekeleza maslahi ya wananchi! Kila mtu anataka aonekane kiongozi bora sio kwamba ni kiongozi bora!

Inakwaza sana kufikiria mwisho wa haya yote!
Kwa kauli aliyoitoa pinda siku hiyo kuhusiana na jairo ni aibu kubwa sana kwa kiongozi makini, sipati picha anatakiwa achukue hatua gani....
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.

===========
UPDATES:

Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil

More updates to follow
Walio msingizia waburuzwe mahakamani basi. Kumbe huyu mtu ni innocent???
 
hata kama pesa hazifiki 1bil. Inamaana watendaji wangapi wa wizara wanaoenda bungeni na kugharimu pesa zote hizo. Jamani hebu tuwe realistic, inamaana kila mwaka wizara inatumia above Mil 500 kwa kuwahudumia watumishi wake bungeni kwa muda huo mfupi wa kipindi cha bunge?!
 
IF SOME ONE IS THINKING DIFFERENT FROM YOU DOESNT MEAN HE/SHE IS WRONG.
JAMANI TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MTUHUMIWA NA MKOSAJI...HUO NDIO UTAWALA WA SHERIA...TUACHE SIASA UCHWALA ZINAKWAMISHA SANA MAENDELEO YETU...MMEAMBIWA
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti SASA HAPO MNATAKA NINI? KWANI HUO NDO UTARATIBU WA KUPITISHA BAJETI ZA WIZARA ZOTE...ISHU SIO JAIRO...ISHU IKO KWENYE UTARATIBU

hili ndo tataizo la masaburi

Utaratibu gani unazungumuzia? kwanini wizara haitengi fungu lake kwa ajiri ya mambo hayo? Mihela yote hiyo ya nini? wizara nyingine sinakosa fungu wenyewe wanachezea
 
jamani hivi nini hasa wanataka kutueleza sisi ni mabwege???
- je ewura malipo ya malazi na chakula walilipia kiasi gani??
- je hao watendaje hawalipi kutoka ofisi zao husika???
 
ina PINDA alivyosema ingekua amri yake angemfukuza kazi pale pale Jairo hakuwa na kosa?ccm wezi tuu nguvu ya mikono yetu inahitajika kuondoa uovu
 
IF SOME ONE IS THINKING DIFFERENT FROM YOU DOESNT MEAN HE/SHE IS WRONG.
JAMANI TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MTUHUMIWA NA MKOSAJI...HUO NDIO UTAWALA WA SHERIA...TUACHE SIASA UCHWALA ZINAKWAMISHA SANA MAENDELEO YETU...MMEAMBIWA
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti SASA HAPO MNATAKA NINI? KWANI HUO NDO UTARATIBU WA KUPITISHA BAJETI ZA WIZARA ZOTE...ISHU SIO JAIRO...ISHU IKO KWENYE UTARATIBU

Kwahiyo mtu anapokosea utaratibu hapaswi kuadhibiwa?,Hiyo pesa ilitoka kwenye fungu gani?Je bajeti ya kila mwaka kwa kila wizara huwa inatenga pesa kwa ajili hiyo?.Kama siyo ni halali kutumia pesa tofauti na matumizi yaliyoelekezwa?Ningekuelewa sana kama ungesema ishu si Jairo peke yake bali ni watendaji wote wa taasisi zilizohusika.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
IF SOME ONE IS THINKING DIFFERENT FROM YOU DOESNT MEAN HE/SHE IS WRONG.
JAMANI TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MTUHUMIWA NA MKOSAJI...HUO NDIO UTAWALA WA SHERIA...TUACHE SIASA UCHWALA ZINAKWAMISHA SANA MAENDELEO YETU...MMEAMBIWA
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti SASA HAPO MNATAKA NINI? KWANI HUO NDO UTARATIBU WA KUPITISHA BAJETI ZA WIZARA ZOTE...ISHU SIO JAIRO...ISHU IKO KWENYE UTARATIBU

Kwani hayo matumizi si sehemu ya bajeti ya hizo wizara? Kwanini isingewekwa kwenye past budget? Kwahiyo una justify matumizi ya serikali yasiyokuwa budgeted how can you differentiate that from corruption?

Je kama hao viongozi watatumia huo mfumo kuomba ziada na kwakuwa hazipo budgeted si ndiyo hivyo tuna changa 500m for ezample and 100M goes into my pocket nani anafanya monitoring kama hiyo pesa si sehemu ya budget? unapofikiria wengine hawawezi ku perceive ujue kuwa we all have common sense which is not common to every one of us.

Ufisadi ni one of the imformal institution kwenye governance yetu tusipolikubali hili basi tutakuwa wasindikizaji wa maendeleo ya dunia huku sisi tukiendelea kukimbiza mwenge nyuma ya mataifa mengine duniani.
 
kwangu hii si breaking news na haiwezi kuwa breaking news! Ingekuwa na itakuwa breaking news iwapo Jairo atachukuliwa hatua za kinidhanu na kisheria.

Niliamini na bado naamini kuwa kwa uzoefu alionao, Jairo alikuwa anafanya best practice ya utendaji wa kawaida unaofanyika Serikalini.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kama alisimamishwa kazi sababu ya kuchangisha pesa kutoka taasisi mbalimbali....., iweje arudishwe kazini sababu tu namba ya hizo taasisi na kiasi kilichochangishwa ni kidogo?

Je kosa ni udogo wa michango au ni kuchangisha pesa (rushwa)......?, kama walijua tangia mwanzo kuchangisha sio kosa na ni utaratibu wa kila siku kwanini walimsimisha kazi?, walikuwa wanachunguza nini sasa?
 
Back
Top Bottom