Lugha zenye kudumaza: Masikini, Wanyonge, Uzalendo na Mabeberu

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,781
2,301
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors.

Bahati mbaya wanasiasa wa chama hiki tawala, hizi ndio zimekuwa ni lugha za kuwahadaa Watanzania kisa tu kupata umaarufu.

Kinyume cha matumizi ya lugha hizi chochezi na dumazi za wanyonge na blah blah ni kuwaona wengine ni matajiri ambao wanapaswa kuishi kama mashetani. Pamoja na mapambio haya, hawa wanaoitwa masikini wako vilevile na hali zao ndio zimezidi kuwa mbaya zaidi.
Badala ya kuweka mikakati ya kupimika ya muda mrefu, kumekuwa na mikakati ya kishabiki.

Wapo wengine mbele za watu wanaitwa mabepari lakini nyuma ya pazia ndio wanaotukopesha (maana deni linazidi kukuwa) na ndio wahisani.

Kifupi, kinachoendelea sana ni udanganyifu wenye kisiasa wenye lengo la kuwafanya wenye uwezo kwamba hawafai isipokuwa wale "wanyonge na masikini".

Ni muhimu kuwafanya Watanzania watambue hali ya umasikini na si kuwaita masikini na majina mengine chochezi.

Tutumie wakati wa sasa tuondoke kwenye siasa zisizo na tija, tujikite kwenye uhalisia wa kuwakwamua Watanzania.
 
Kuna watu nchi hii wasipowaitwa wanyonge kwenye sanduku la kura hupati kitu na wala hutaonekana kwamba wewe ni mzalendo.

Wanasiasa wanajua kucheza na biti la wajinga wengi(wanyonge). Wanyonge ni kundi kubwa la watu wasioijua kesho yao wao bendera fuata upepo tu.

Furaha ya majinga haya ni kuona matajiri wakiitwa majizi, wazungu wakiitwa mabeberu na wawekezaji wakiitwa wanyang'anyi.

Kiufupi wanyonge ni kundi la watu wa ajabu ambalo halitaulaki hata Ufalme wa Mbingu. Wanaulakije wakati roho zao ni mbaya kuliko neno "mbaya" lenyewe?
 
Hizi ndio siasa za halaiki au populism alizozitaja mzee Mkapa kwenye kitabu chake.

Hii kuita watu wanyonge ni kuwachonganisha wananchi wa kawaida na wananchi wenye nacho, kuwafanya wafikiri kuwa umasikini wao umetokana na hao wenye nacho na yeye ndio mkombozi wao.
 
Kiuhalisia Mimi Sio mnyonge , naomba serekali Ya wanyonge inaitoe kwenye kundi hilo ,
Huwa silipendi hili Neno
 
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors..
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya CCM.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia!

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm...
Cha msingi ni kuacha maneno chochezi na yenye kudumaza. Wananchi wamedumazwa na kuamua kujiita wanyonge na masikini huku wapingaji hoja wakiambiwa sio wazalendo na wako na mabeberu.

Ujinga wa namna hii, unaligawa Taifa kwa kujenga chuki na hata kuvuruga mfumo wa biashara. Hitaji ni mfumo wa kupambana na umasikini, utoaji haki na uwajibikaji.
 
Mbona na wewe unawapangia Chadema cha kusema? Au ndio nyani haoni kundu lake? Funika kwanza tundu lako ndio uanze ya wengine
 
Cha msingi ni kuacha maneno chochezi na yenye kudumaza. Wananchi wamedumazwa na kuamua kujiita wanyonge na masikini huku wapingaji hoja wakiambiwa sio wazalendo na wako na mabeberu.

Ujinga wa namna hii, unaligawa Taifa kwa kujenga chuki na hata kuvuruga mfumo wa biashara. Hitaji ni mfumo wa kupambana na umasikini, utoaji haki na uwajibikaji.
Kuna ubaya gani kujenga chuki na nyumbu?
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya CCM.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia!

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Jikite kwenye mada Mkuu! Ni kuhusu wanyonge sio hao uliowataja! Ukitaka anzisha Uzi kuwahusu.
 
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors.

Bahati mbaya wanasiasa wa chama hiki tawala, hizi ndio zimekuwa ni lugha za kuwahadaa Watanzania kisa tu kupata umaarufu.

Kinyume cha matumizi ya lugha hizi chochezi na dumazi za wanyonge na blah blah ni kuwaona wengine ni matajiri ambao wanapaswa kuishi kama mashetani. Pamoja na mapambio haya, hawa wanaoitwa masikini wako vilevile na hali zao ndio zimezidi kuwa mbaya zaidi.
Badala ya kuweka mikakati ya kupimika ya muda mrefu, kumekuwa na mikakati ya kishabiki.

Wapo wengine mbele za watu wanaitwa mabepari lakini nyuma ya pazia ndio wanaotukopesha (maana deni linazidi kukuwa) na ndio wahisani.

Kifupi, kinachoendelea sana ni udanganyifu wenye kisiasa wenye lengo la kuwafanya wenye uwezo kwamba hawafai isipokuwa wale "wanyonge na masikini".

Ni muhimu kuwafanya Watanzania watambue hali ya umasikini na si kuwaita masikini na majina mengine chochezi.

Tutumie wakati wa sasa tuondoke kwenye siasa zisizo na tija, tujikite kwenye uhalisia wa kuwakwamua Watanzania.

Sio lugha za kudumaza. Ni lugha za kikatiba. Katibu ya nchi inasisitiza sera ya preferential option for the poor. Political philosophy zote zinazotambua ukuu wa maslahi ya pamoja dhidi ya maslahi binafsi zinatambua sera hii pia. Mfano ni social doctrine of the catholic and anglican churches. Boresha hoja yako kwa kuzingatia aya hii:

"Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii." (Katiba ya JMT 1977, 13(5))
 
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors.

Victim ni mwathirika
Survivor ni muokoka.

Ktk sakata la ykimwi victims wanapewa Arv na survivors wanatafutiwa chanjo.

Rekebisha misamiati yako
 
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors.

Bahati mbaya wanasiasa wa chama hiki tawala, hizi ndio zimekuwa ni lugha za kuwahadaa Watanzania kisa tu kupata umaarufu.

Kinyume cha matumizi ya lugha hizi chochezi na dumazi za wanyonge na blah blah ni kuwaona wengine ni matajiri ambao wanapaswa kuishi kama mashetani. Pamoja na mapambio haya, hawa wanaoitwa masikini wako vilevile na hali zao ndio zimezidi kuwa mbaya zaidi.
Badala ya kuweka mikakati ya kupimika ya muda mrefu, kumekuwa na mikakati ya kishabiki.

Wapo wengine mbele za watu wanaitwa mabepari lakini nyuma ya pazia ndio wanaotukopesha (maana deni linazidi kukuwa) na ndio wahisani.

Kifupi, kinachoendelea sana ni udanganyifu wenye kisiasa wenye lengo la kuwafanya wenye uwezo kwamba hawafai isipokuwa wale "wanyonge na masikini".

Ni muhimu kuwafanya Watanzania watambue hali ya umasikini na si kuwaita masikini na majina mengine chochezi.

Tutumie wakati wa sasa tuondoke kwenye siasa zisizo na tija, tujikite kwenye uhalisia wa kuwakwamua Watanzania.
Mm cio mnyonge hata siku moja serikal iniondoe kwenye kundi hilo maana wameubili sana uzalendo awamu ya tano lkn nyuma ya pazia wanatuibia kodi zetu
 
Huko nyuma, wale watu waliokutwa na virusi vyenye kusababisha ukimwi au ubakwaji, walikuwa wanaitwa waathirka (victims). Lakini kadri muda unavyoenda imegundulika hizi ni lugha zenye kurudisha watu nyuma na wengine mpaka sasa hivi wanaitwa survivors.

Bahati mbaya wanasiasa wa chama hiki tawala, hizi ndio zimekuwa ni lugha za kuwahadaa Watanzania kisa tu kupata umaarufu.

Kinyume cha matumizi ya lugha hizi chochezi na dumazi za wanyonge na blah blah ni kuwaona wengine ni matajiri ambao wanapaswa kuishi kama mashetani. Pamoja na mapambio haya, hawa wanaoitwa masikini wako vilevile na hali zao ndio zimezidi kuwa mbaya zaidi.
Badala ya kuweka mikakati ya kupimika ya muda mrefu, kumekuwa na mikakati ya kishabiki.

Wapo wengine mbele za watu wanaitwa mabepari lakini nyuma ya pazia ndio wanaotukopesha (maana deni linazidi kukuwa) na ndio wahisani.

Kifupi, kinachoendelea sana ni udanganyifu wenye kisiasa wenye lengo la kuwafanya wenye uwezo kwamba hawafai isipokuwa wale "wanyonge na masikini".

Ni muhimu kuwafanya Watanzania watambue hali ya umasikini na si kuwaita masikini na majina mengine chochezi.

Tutumie wakati wa sasa tuondoke kwenye siasa zisizo na tija, tujikite kwenye uhalisia wa kuwakwamua Watanzania.
Aneyeitwa masikini,mnyonge akakubali ndiye mwenye matatizo, hata Nchi Za Ulaya na Asia wakiona mtu mwenye rangi nyeusi picture ya kwanza wanayoiona ni umasikini kama wanavyoonyeshwa Mwenyekiti TV na Magazeti yao, China ilikua hivyo siku zilizopita wakakataa na kuanza kulipia vipindi, kwenye TV, magazeti ya ulaya ili kuondo hio taswira na wameweza. Watanzania wakatae kuitwa masikini na wanyonge
 
Victim ni mwathirika
Survivor ni muokoka.

Ktk sakata la ykimwi victims wanapewa Arv na survivors wanatafutiwa chanjo.

Rekebisha misamiati yako
Naomba nikiri kwamba nilelenga kuwaita wabakwaji ambao walikuwa wakiitwa victims kuwa survivors na si waathrika. Naomba isomeke hivyo.
 
Back
Top Bottom