Uzalendo sio kuwa chawa wala kusifia Serikali

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
Katika miaka ya kuanzia 2015 Zana nzima ya uzalendo imekuwa ikipotoshwa Sana. Kipindi cha awamu ya tano neno uzalendo liligeuzwa kuwa ni Hali ya mtu kusifia serikali na w viogozi wake. Ikifika mahali mtu yoyote akikosowa serikali au kiongozi akawa anaitwa msaliti au kibaraka.

Na wale walio kuwa wanasifia serikali au viogozi wakawa wanaitwa wazalendo. Hata kama hizo sifa ni za kinafiki au za kiujaja ujaja za kutaka aonekane ili wapewe vyeo au chochote kutoka kwa wenye madaraka. Hiyo Hali ya upotoshaji kuhusu maana halisi ya uzalendo kimezidi kushamili. Na watanzania wengi wameisha chaganywa kuhusu maana halisi ya mtu kuwa mzalendo au penda nchi yake.

Mimi nataka ni tafusiri maana ya kuwa mzalendo kwa uelewa wangu. Kama nitakosia nitafurahi kukosolewa. Mtu kuwa mzalendo ni ile Hali ya kuipenda nchi yake na wananchi mwezake. Mtu unakuwa uko tiyara kupoteza masilahi binafusi kwaajiri ya masilahi ya nchi yako.

Au masilahi ya wengi. Kwa mfano wewe kama ni waziri ukaona mkataba ambao hauna faida kwa nchi Bali unafaida kwa watu wa chache. Basi unakuwa tayari kuwambia hao watu kuwa mkataba huo haufai na kama hautasitishwa basi utatoka hadharani na kuwaelezea wananchi kinacho endelea hata kama utapoteza nafasi yako kwa kosa la kuvujisha siri potelea mbali.

Mtu wa namna hiyo ni mzalendo wa kweli. Mfano mwingine: wewe kama ni mfanya kazi serikalini kama polisi tukaambiwa na mkuu wako wa kazi kutekeleza amri ambayo ni kinyume cha sheria na na katiba ya nchi halafu wewe ukaataa na kusema huwezi kwenda na kinyume na sheria za nchi amabozo uliapa kuzilinda, bora upoteze kazi. Hapo utakuwa umeonyesha uzalendo wa kweli.

Mfano mwingine. Wewe ni mfanya biashara kaona biashara ya kuuza madawa ya kulevya inaweza kuinunuwa halaka lakini ukakumbuka kuwa hiyo biashara kufanikiwa kwake ni kuangamiza vijana wa taifa lako basi kasema bora nife masikini kuliko kuuza madawa kwa Watoto wa taifa langu.

Pia huo ni uzalendo. Yaani uzalendo kwa kifupi ni kuwa mwaminifu kwako mwenyewe na kwa taifa lako. Mtu ambaye sio mzalendo ni mtu yoyote ambaye anafanya mambo ovyo ovyo eidha yawe yake binafusi au ya mwajiri wake. Kwa mfano msimamizi wa uchaguzi anaye tangaza matokeo ya kura za wizi huyo hawezi kuwa mzalendo hata kidogo.

Polisi anaye pokea rushwa hawezi kuwa mzalendo hata kidogo. Haki u anaye towa huku u zisizo zigatia haki hawezi kuwa mzalendo. Raisi ambaye amechaguliwa kwa kura za wizi hawezi kuwa mzalendo hata kidogo. Mfanya biashara za magendo hawezi kuwa mzalendo. Yoyote anaye saidia wizi wa kura hawezi kuwa mzalendo. Mwalimu anaye vujisha mtihani hawezi kuwa mzalendo.

Mwanafuzi anaye honga mwalimu ilia msaidie kufuli mtihani hawezi kuwa mzalendo. Mbunge ambaye amekuwa mbunge kwa kura za wizi au kupita bila kupigwa hawezi kuwa mzalendo.

Polisi anaye bambikia watu kesi au anaye umiza wananchi bila sababu hawezi kuwa mzalendo. Kwa mfano hiyo nafikiri nimeeleweka. Kama siko sahihi naomba ni sahihishwe.
 
Back
Top Bottom