Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Oh! kaka kumbe bado upo?
pole kwa kazi..naona uko bize sana 'kunusuru' chama kwenye hiki
kinyesi.

Mkuu hamna wa kuinusuru watu wanaoaminiwa ndani ya Chadema ndio wasaliti
 
Huyu kijana!!!!!!!!!!!! inatia shaka kuamini kama anaweza fanya mambo haya maana ni mtu ambaye hata huwezi kumdhania...I know him since we were at DUCE it is an implicated story!!! Let the Police force ensure justice is met.Pole Ludovick
 
Hivi Ben Saanane yuko wapi? au kazi yake ilishakwisha? maana hiki kitimtim?.....wapi mwana Intelijensia wa Magwanda Ben?! kuna mtu alisema huku ..mkisha baini kama Ben anafanya kazi kwa niaba ya nani..then it will be too late!
Huo ndio ukweli. Jamaa ni usalama wa taifa tena amesomea kuleta mitafaruku ndani ya vyama vya upinzani. Alivyoleta maswala ya masalia kulikuwa na tuhuma za yeye kumwekea zitto sumu, umemsikia akikanusha? Alichofanya ni kuwaonyesha kina mbowe kuwa zitto mbaya lakini hapohapo kumwonyesha zitto kwamba atauawa kwa sumu na upande mwingine. Kama chadema mnajua mambo ya inteligensia, huyu jamaa upigeni marufuku kabisa kujihusisha na chama na kuwapiga marufuku viongozi wa chama kujihusisha nae
 
Anayedaiwa kupiga video iliyosababisha kukamatwa kwa Rwakatale ( pichani ) maarufu kwa jina la Ludovik Joseph amekamatwa mkoani Iringa .kijana huyo anadaiwa kuwa ni mhitimu wa chuo kikuu cha DUCE

--------------------------------
Ndugu zangu,
Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.

Namfahamu kijana Ludovik tangu akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.

Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi kwa namna fulani nimeshtushwa nazo.

Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii. Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti kwenye Mjengwablog kila asubuhi.

Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog.

Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.

Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana. Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima.

Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo.

Ni mimi:
MAGID MJENGWA

Credit: mjengwablog
KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKARE NAYE AMEKAMATWA - MPEKUZI
 
Vyombo hivyo vya usalama vifanye kazi kwa weledi ili ukweli ujulikane.
Haya angalieni msije mkavua nyangumi la bahari kuu maana naona wavuvi wanasogea sogea tu Magogoni...Pataumbuka mzazi wake Liz halafu Policcm waanze kujuta na kulala makaburini maana ndo mnakoelekea huko kwasababu kuna thread hapa inaonyesha akina salva wanapongezana huko magogoni sijui kama wanaelewa mawimbi haya ya udhalimu kama yatashindwa kumlowanisha Baba Liz...Taratibu jamani nyie polisi msiwachezee CDM kirahisi hivyo
 
Kijana alietengeneza hiyo video alipata mafunzo maalum ya propaganda thru Youtube nchini Israel....sidhani kama vyombo vya dola havijui kinachoendelea...
 
kwa hiyo umafia huo alilipwa ili achafue cdm mbona imekula kwake ameongeza maadui wengi zaidi kabla ya kuponya jeraha lililoko ndani ya ccm
 
Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana. Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima.

Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo.

Ni mimi:
MAGID MJENGWA

Credit: mjengwablog
KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKARE NAYE AMEKAMATWA - MPEKUZI

Tuelewe kipi. Ludovick ameshiriki kuteswa kwa Kibanda au ameandaa video ya Lwakatare?
 
ngoja 2one maana hii move inaelekea kumpata director aliyeiandaa mwisho wa siku staring aliyecheza atakuwa hewani,karibun hollywood!
 
Mi siamini kama huyu dogo alihusika kuandaa video hii. Maana sipati mankiki kuwa muandaaji akubali jina lake, na sauti yake halisi vibaki recognisable kwenye dili chafu kama hii, tena mtu mwenyewe graduate!!!
Angekuwa amehusika lazima angefanya editing kuhakikisha identities zake hazibaki kwenye hiyo video

Otherwise ametumiwa na makachero, ili kwa kutambuliwa kwake aende 'akiri' uongo mahakamani kuwa kweli Lwakatare alikuwa namuagiza kufanya uovu, ili aitie CDM hatiani...
 
Hii ina mashiko. Sidhani kama ni mwalimu makini kwanza angekubali kuhusika katika uchafu huo, lakin pili angekubali kuacha vidhibiti kama ilivo katika ile movie. Anatumiwa na amekubali kutumika.
 
Kwani alishindwa kuvituma mpaka akuletee, kuna kitu alikuwa anakimbia Dar na ww Majjid inabidi uhojiwe.
Utata mwingine hapo kwenye bold, mbona tuliambiwa alipewa gari la polisi, hii teksi inaingiaje? au polisi nao walimwacha sehemu. Jamani muwe mnajipanga vizuri kwenye hizi movie zenu vinginevyo hamuwezi kumdanganya hata mtoto mdogo.

Asante kamanda
 
Mr. ABLE huo sasa ni uchochezi, au umeshajitengenezea hifadhi yakishakuwa unayoyataka utuache sisi tunapigana wenyewe kwa wenyewe?uchochezi sio mzuri
 
Mi siamini kama huyu dogo alihusika kuandaa video hii. Maana sipati mankiki kuwa muandaaji akubali jina lake, na sauti yake halisi vibaki recognisable kwenye dili chafu kama hii, tena mtu mwenyewe graduate!!!
Angekuwa amehusika lazima angefanya editing kuhakikisha identities zake hazibaki kwenye hiyo video

Otherwise ametumiwa na makachero, ili kwa kutambuliwa kwake aende 'akiri' uongo mahakamani kuwa kweli Lwakatare alikuwa namuagiza kufanya uovu, ili aitie CDM hatiani...
Hiyo inaleta mantiki kwako, lakini kumbuka hawa jamaa wakati wanaandaa hawakujua kama mission impossible yao itagundulika.

Criminal psychologist wamebainisha kuwa kadri criminals wanavyofanikiwa katika mission zao, ndivyo huzidi kujijengea imani kama wako smart na hawawezi kukamatwa. Kujigengea imani huko huwafanya wajione kama wako empowered na kuanza kuchukua shortcuts huku mental focuses yao ukipungua bila kujua kama law inforcement wao ndiyo wanaongeza nguvu na mental focuses kuwasaka. ndiyo ilivyotokea kwa huyu jamaa.
 
Naweza kutabiri
kitakachofuata, Kijana Ludovick ndie atakayetumika kuhalalisha matamshi
ya Lwakatare katika ile Clip, nahisi atasema ni kweli Lwakatare
aliniagiza kufanya hayo kwa kuwa target ni Lwakatare na CDM. Muhimu ni
ludovic kufahamika kwa undani zaidi. Hii itatupatia malengo yaliyopo
nyuma ya pazia.
Haswaaa, hapo umepatia. Hata mimi naona hivyo.
 
Back
Top Bottom