Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Ccm ndo imeshikwa pabaya, wameshindwa politics wamekuja na style tofauti kabisa na siasa, nadhani walianza kuona dalili za wazi kwamba through jukwaa hawawezi kupambana na M4C so better wabadili tecnics, and yes why not, wana serikali, wana pesa nini cha kuwazuia?
lakini here me, TUTASHINDA!

yeah CCM imeshikwa pabaya -- kuna mathematical progression ku-prove; Miaka ya 80 -90 -- kura 99%. Mwaka 2005 kura 84%. Mwaka 2010 kura 61%. Mwaka 2015 .....45% (projected). Na ndiyo maana wanakuja na hizi movies huku wakitegemea mbeleko ya polisi.

CCM mtaondoka tu.......na udhalimu wenu!
 
kula like mkuu japo natumia haka kasimu mchina

Watanzania mkoje? Mnajua kweli Manyerere? The most opportunistic mwanahabari miongoni mwao wote! Kwanza nasikia Ludovick alikamatwa kabla ya yeye Manyerere kupost thread yake ile ya awali iliyosema atafutwe mtu aitwaye Ludovick.

pili si kweli alivyosema kuwa habari za kutekwa Kibanda ziliripotiwa polisi asubuhi baada ya tukio. Asome gazeti la Mtanzania vizuri.

Manyere asichezee akili za watu. Tunajua movie hii inawezeshwa kwa kiasi kikubwa na msaada wa polisi, lakini itashindikana tu.
 
Hii video sio Bad lips, nimeangalia mara 4 tena, chadema waongee na Lwakatare kawauza very cheap

mimi nimeiangalia mara 7 na ni bad lips reading. Haitasimama kortini kamwe ingawa kama ni propaganda dhidi ya CDM, basi ni propaganda kali inayosaidiwa na polisi.
 
Kumbe mtu mwenye CHIZI sasa hiyo STORY na kupokea HELA western union wapi na wapi?
mtu anapokutumia hela western union lazima awe anakujua!!!! isitoshe wakati wa kupeana maelezo ya siri kama
jina lililotumika lina makosa alitakiwa kumwambia mtumaji, Western union wanataka kitambulisho chenye picha na kinachokubarika,
no wonder hata video ya Lwekatare ina makosa kibao kama watu wenyewe ni hawa

si unajua tena ndugu zetu kujisifu
 
Huyu mtu nimemfahamu kupitia jukwaa la wanabidii na nimeongea naye kwa simu mara kadhaa!Msimamo wake kisiasa kule wanabidii alijonesha kama chadema, sasa haya ya video na hili la kukamatwa linanitatiza!Ila kama ni kafara Mungua amrehemu kama ni mnafiki apelekwe kunakostahili!

Mkuu Bukanga,
Nakutaarifu kwamba na wewe unatakiwa kukamatwa ! Una mawasiliano ya karibu na mtuhumiwaaa....
This time tutawajua wengi !
 
mimi nimeiangalia mara 7 na ni bad lips reading. Haitasimama kortini kamwe ingawa kama ni propaganda dhidi ya CDM, basi ni propaganda kali inayosaidiwa na polisi.

kama hii ndo imeandaliwa kwa msaada wa polisi na usalama pamoja na wataalamu wa chama, tuko nyuma saana kwa technologia, hata uwezo wao wa kufikiri ni wa kutilia shaka
 
Hivi kama inadaiwa hiyo video imepikwa kwa kuwekewa maneno si jerked original video watu wachambue wajue pumba na mchele
 
Ludovick Joseph Akamatwa Na Polisi

Saturday, 16 March 2013 | Na Mjengwa


Ndugu zangu,

Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.

Namfahamu kijana Ludovik tangu akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.

Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti kwenye Mjengwablog kila asubuhi. Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog. Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.

Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana. Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima. Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo.

Hapa chini ni maelezo niliyoyaandika kwenye ukuta wangu wa facebook, siku ile Ludovick alipopatwa na mkasa wa kuvamiwa usiku;
... Na Msaidizi Wa Mwenyekiti Naye Alitekwa Na Majambazi Jana Usiku!

"Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"
Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.

Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji. Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na majambazi.

Nikamsaidia Ludovik. Na kwa vile yeye ni Yanga, basi, nikahakikisha nampa suruali na jezi ya Simba!

Naam, iko siku, kila mtu ataishabikia Simba!

Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo."
 
Sheria ya ugaidi ipo na itumike huyu. Alikua akipanga mipango ya kigaidi ya kudhuru
Sheria hii haipo kwa waislam tu
Lazima itumike hapa huyu jamaa

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.
Kwani alishindwa kuvituma mpaka akuletee, kuna kitu alikuwa anakimbia Dar na ww Majjid inabidi uhojiwe.
Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji. Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na.
Utata mwingine hapo kwenye bold, mbona tuliambiwa alipewa gari la polisi, hii teksi inaingiaje? au polisi nao walimwacha sehemu. Jamani muwe mnajipanga vizuri kwenye hizi movie zenu vinginevyo hamuwezi kumdanganya hata mtoto mdogo.
 
Sheria ya ugaidi ipo na itumike huyu. Alikua akipanga mipango ya kigaidi ya kudhuru
Sheria hii haipo kwa waislam tu
Lazima itumike hapa huyu jamaa

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

which is which?
 
Ya alikuja na Teksi, Alipata habari kupitia radio call ya polisi.
 
Kwahiyo lwakatare katoka kwenye kesi yake yakuwa yeye ndiye aliyekuwa akipanga njama za kumuumiza kibanda?
 
Kwahiyo lwakatare katoka kwenye kesi yake yakuwa yeye ndiye aliyekuwa akipanga njama za kumuumiza kibanda?

mkuu kuna jamaa kafunguka humu kwamba ni wahusika wa hii tamthilia ya isidingo....hawezi kutoka ila nasikia hali yake kiafya si nzuri kwa siku hizi alizokamatwa anasumbuliwa na kisukari.
 
Back
Top Bottom