Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Ludovick Joseph akamatwa na Polisi...

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Mungu mkubwa!

Habari za uhakika nilizozipata dakika kadhaa zilizopita zinasema mtuhumiwa mkuu wa utekaji na utesaji wa Kibanda, Ludovick Joseph, amekamatwa punde tu mjini Iringa.

Tulikotoka: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-siri-za-kutekwa-kibanda-hazitajulikana.html

UPDATE:
Ludovick Joseph Akamatwa Na Polisi

Saturday, 16 March 2013 | Na Mjengwa


Ndugu zangu,

Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.

Namfahamu kijana Ludovik tangu akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.

Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti kwenye Mjengwablog kila asubuhi. Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog. Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.

Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana. Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima. Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo.

Hapa chini ni maelezo niliyoyaandika kwenye ukuta wangu wa facebook, siku ile Ludovick alipopatwa na mkasa wa kuvamiwa usiku;

... Na Msaidizi Wa Mwenyekiti Naye Alitekwa Na Majambazi Jana Usiku!

"Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"

Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.

Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji. Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na majambazi.

Nikamsaidia Ludovik. Na kwa vile yeye ni Yanga, basi, nikahakikisha nampa suruali na jezi ya Simba!

Naam, iko siku, kila mtu ataishabikia Simba!

6_4d065.jpg

Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo."
 
Kama kwel huyu BUKOBA BOY naomb mnichangie maha*i nimu**e
 
Usiturushe roho mkuu km ni kweli Ebu weka uthibitisho hapa stejini tuuchakate

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Duu Jf ilishasema hapa,maggid mjengwa atasalimika?
 
Mchezo unaendelea , huyu Ludovic ni nani , ana mahusiano gani na waziri NChimbi, ana mahusiano gani na Membe , anafanya shughuli gani huyu , je ? Umbo lake linamwezesha kupambana na kibanda ? Au yeye ni mtu wa aina gani .....huyu anafanya shughuli gani na anaish wapi? ......
 
Ni yule aliyevuliwa nguo? Rafiki wa mjengwa? Ngoja nisubiri nione hii movie itaishaje.
 
kwenye clip ya video ya lwakatare:

15:59 ...sauti inasika ikisema '' unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ''LUDOVICK'' ndiye unamfatilia''...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

17:10 kijana anayepewa maelekezo (''Ludovick) anauliza '' kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?'' lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema '' Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza'' ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

 
Picha linaendelea bado kidogo tutaujua ukweli
 
Kama kapatikana ni vizuri sana ili ukweli uchukue nafasi yake.
 
Back
Top Bottom