Lowassa watulize watu wako

Lowassa watulize watu wako

Njanga Tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
843
Reaction score
655
Baada ya kukatwa kwa Mzee wetu wingu zito limetanda miongoni mwa sisi wafuasi wake hasa kutokana na ukimya huu wa Mzee wetu.

Mzee Lowasa kumbuka siku tunaianza safari yetu pale arusha ule umati mkubwa wa watu,kumbuka pia wakati wakutafuta wadhamini ule utitiri wa watu uliokua nyuma yako.
Hakuna mkoa ulipita usitikisike kwa kishindo chako. Wakumbuke wadhamini elfu 87 tulio nyuma yako.

Mzee wangu naomba ututulize sisi wafuasi wako mana kuna sintofahamu kubwa ndani ya mioyo yetu. Kumbuka sisi ni wengi kuliko wale walioamua kwa utashi wao.

Kama ukiamua kusema chochote sisi tutafuata tu tuko tayari siku zote na muda wote.Asikudanganye mtu eti CCM haijapasuka njoo uku uone watu walivyosusa na kuchukizwa na walichokifanya.

Nakusihi mzee tutulize watu wako lasivyo unatuacha kwenye wakati mgumu.Fanya hima jembe langu nakutegemea sana.

#Lowasa watulize watu wako
 
Lowasa na wafuasi wake hawana madhara
 
Safari ya matumaini kuelekea ACT wasaliti ndiyo imepamba moto.
 
Mapambano bado yanaendelea! Tuendelezi mapambano hadi kieleweke!
 
Ni Kama mas'hara Ila ukweli Ni Kwamba MPASUKO MKUBWA UPO WATAANZA KUUSHUHUDIA WAKATI WA KAMPENI
 
wewe mbona hujatulia unaandika kama ffu wamekuunganishia

Sijakuelewa.
 
Mlikuwa
Brain washed kwa kufuata mkumbo badala ya akili zenu. Mwacheni baba watu apumzike. Nyie hamna tofauti na wafuasi wa Kibwetere kwani mlijitoa fahamu mkamfuata fisadi mmepata mlichotaka ebu nyamazeni kukwepa aibu. Kumbuka hata wajanja kama Mzee Mengi waliingia mkenge.
 
Funguka sasa mapambano yanaendelea kivipi? Ndani ya CCM au nje ya CCM? Supporters wanasubiri kusikia direction baada ya ile kauli mbinu yenu ya #HakatwiMtu kupigwa chini kwa kishindo.

Hapa mwenye macho haambiwi tazama.Vita ya panzi nafuu ya kunguru.
 
Mzee mwepesiiiiiiiiiiii........teh teh...
 
Ingiq Team ushindi UKAWA ndiyo habari ya Town kwa sasa...Wakribishe na wenzako.
 
Tatizo mliahidiwa vyeo na ahadi kedekede.

Na nyie ndio mliokuwa mnamjaza ujinga Lowassa na kumtoa mamilioni ya pesa.

Fanyeni kazi vijana sio mnarubuniwa na wanasiasa Halafu mnaanza kupiga kelele Lowassa sasa hivi anawazia afya yake sio nyie wanasiasa njaa.
 
Back
Top Bottom