Lowassa watajie CHADEMA mali unazomiliki

Lowassa watajie CHADEMA mali unazomiliki

Sukari bei juu halafu unkuja na hoja ya kutupotezea maboya.
Jee una habari bei ya MAHINDI katavi iko nafuu sana. The cheapest in the whole of East Africa kwa sasa, Fanya jitihada ukanunue magu nia yako 100, peleka kenya au Zambia, utapata faida mzuri, nunua sukari mifuko 70 lipia kodi na ingiza Tanzania , utarudisha ile helal yako mara 3.

Ushauri wa kukuendeleza, kama huna mtaji, mtafute mwenye mtaji, mshauri vizuri na mwambie mutants kazi na mugawane faida , yeye ni mtaji na wewe u juzi na wakati wako.
 
Monduli pale kuna mtu anaitwa Kadogoo ndo mwenyekiti wa Halmashauri ile ni kibaraka mzuri wa lowassa nadhan chadema wamtumie huyu atwasaidia kumjua lowassa maana fact ni kwmba kumpokea lowasa chadema kulifanyikaga kw kukurupuka tu bila uchunguzi wa kina kuhusu huyu mtu
Nyie mshachunguza uchafu wenu huko ccm Maana imeoza
 
Siko hapa kumtetea Lowassa, lakini katika mambo yanayotuacha hoi wananchi ni pamoja na hili. Hakuna asiyejua jinsi viongozi wa ccm walivyozitumia nafasi zao kulihujumu taifa hili.

Hali hiyo ndio inafanya ccm iwe tayari hata kwa machafuko kubaki madarakani ili kulinda maslahi ya viongozi wake wachache, kwani inajua pindi watakapopoteza dola wenye kumiliki mashamba kama Lowassa, viwanja vya wazi na viwanda isivyo halali watakuwa ni wengi kupita kiasi. Rais Magufuli alianza na kasi kubwa kwenye awamu yake, lakini kadiri siku zinavyokwenda anazidi kushindwa kutekeleza majukumu yake, kwani anaopaswa kuwabana ndio hao wanaojiita vigogo wa ccm. Usishangae sasa Lowassa kuanza kuibuka kwa kasi kwani ameshajua rais ameanza kuujua ukweli na hana la kufanya zaidi ya kuwa mpole. Kwa maneno marahisi hawezi kukata tawi alilokalia. Kasi yake naifananisha na jinsi alivyoanza JK, lakini akaishia kuwa mtalii wa kiwango cha guiness book of record.
Unachofanya ni kujaribu kumtetea Lowassa kwa kutumia kinga inayosema, hata wale pia wana madhambi kama Lowassa!

Ninakubaliana na wewe, ni kweli pia kuna viongozi wengi ndani ya serikali na CCM au waliostaafu ambao wamepata mali ambazo hazina maelezo mazuri.

Kusema CCM iko tayari kwa machafuko kuliko kuachia madaraka nadhani ni hisia zako tu kwa sababu hakuna ushahidi unaotoa matokeo ya unachokisema. Tukubali tu kuwa upinzani Tanzania na hasa Tanzania Bara bado ni mchanga kiasi kwamba hata watanzania wengi hawawaamini wapinzani kama wako tayari kukabidhiwa nchi. Ninasema hivyo kwa research zote zinabainisha ninachokisema.

Kuhusu Rais Magufuli kushindwa kutekeleza majukumu yake nadhani tatizo lako hufahamu pattern za siasa zilivyo pale kiongozi mpya wa nchi anaposhika madaraka. Kwenye pattern za siasa kwa sasa ni phase ya pili ambayo Rais hutumia muda mwingi mezani baada ya kumaliza phase ya kwanza ambayo huwa ni kuonyesha mwelekeo wake kwa Taifa. Kwa sasa ni muda wa kugawa majukumu baada ya wafanyakazi kufahamu mwelekeo wa Rais. Jaribu kusoma vitabu vya masuala ya siasa na uongozi.

Huwezi kumlinganisha Rais Magufuli na Rais Kikwete kwa sababu hata haiba wanatofautiana sana achilia mbali utendaji wao. Kikubwa zaidi, Majukumu ya kitaifa wakati wa utawala wa Rais Kikwete ni tofauti na majukumu ya kitaifa wakati huu wa utawala wa Rais Magufuli
 
Kina Mkapa,Kikwete,Kinana,Mwinyi,na Magufuli wameshakutajia mali zao wanazomiliki au una mahaba na Lowasa...Usiwe mnafiki kwa kujifanya una uchungu na Nchi hi huku jumba unalolitukuza ndo linanyonya watanzania na kupelekea wengine kupoteza maisha.
 
jamaa mnafiki sana sijaona kosa la mbunge ikiwa shamba linamilikiwa kinyume na utaratibu kwani viongoz ndo wenye hisa na nchi hii? eti lowasa angesema ili mbunge akienda bungeni aongee kwa tahadhari hajui kama uongo hudumu kwa siku moja ukweli hubak milele.

kweli hawa ndo watumbua majipu kama sio usanii? lengo lake lilikuwa kumponda lowasa ajabu viongoz wote wa kitaifa wakubwa hakuna hata alieweka mali zake wazi ndani ya chama chake hadi nje kwenye jumuia. hoja mfu kabisa kaleta huyu na imasemekana wapo vijana watatu humu jf toka huko kazi yao ni kueneza uongo tu.
 
Swali la kujiuliza ni je, kama kuna dhamira ya kweli, kwanini Wabunge wa CCM wamepinga wazo la muswada wa kutenganisha biashara na siasa? Hapa ndio utajua jinsi gani ccm ni wanafiki. Kwani kwa biashara ya real estate kati ya Lukuvi na wafanyabiashara WAKUBWA WAKUBWA, na pia biashara za viongozi wengine wengi tu ngazi 'zooooote', wataathirika.

Mimi sipingi suala la viongozi kutangaza mali zao, nachopinga ni mchezo mchafu wa kisiasa wa CCM unaotumika kutenga walio wenzetu na wasio wenzetu. Basi. Njooni na objective approach, tutawaunga mkono.

cc MsemajiUkweli
Mimi napenda kuona upinzani ukionesha mifano pale wanaposema CCM haifanyi vizuri
 
Ahahaa!!;nadhani hata swali la nyongeza halikuwepo!!;kamati ya chadema lazima imjadiri!!
Swali la nyongeza litapatikana vipi wakati alipigwa butwaa baada ya kusikia kuwa shamba anamiliki Lowassa.
 
Mi ckuiz post za hiv hta sipotez muda kusoma. Nikiisha soma kichwa cha hbar na paragrap ya kwanza inatosha. Kwanini nijichoshe na hiz propaganda zilezile hkuna hta jipya.

NIMEZUNGUKA MADUKA YA KITAANI KWETU LEO YOTE HKUNA SUKARI.
Wewe hata kuandika kwa ufasaha ni majanga, utaweza kusoma vizuri thread yote?
 
Unachofanya ni kujaribu kumtetea Lowassa kwa kutumia kinga inayosema, hata wale pia wana madhambi kama Lowassa!

Ninakubaliana na wewe, ni kweli pia kuna viongozi wengi ndani ya serikali na CCM au waliostaafu ambao wamepata mali ambazo hazina maelezo mazuri.

Kusema CCM iko tayari kwa machafuko kuliko kuachia madaraka nadhani ni hisia zako tu kwa sababu hakuna ushahidi unaotoa matokeo ya unachokisema. Tukubali tu kuwa upinzani Tanzania na hasa Tanzania Bara bado ni mchanga kiasi kwamba hata watanzania wengi hawawaamini wapinzani kama wako tayari kukabidhiwa nchi. Ninasema hivyo kwa research zote zinabainisha ninachokisema.

Kuhusu Rais Magufuli kushindwa kutekeleza majukumu yake nadhani tatizo lako hufahamu pattern za siasa zilivyo pale kiongozi mpya wa nchi anaposhika madaraka. Kwenye pattern za siasa kwa sasa ni phase ya pili ambayo Rais hutumia muda mwingi mezani baada ya kumaliza phase ya kwanza ambayo huwa ni kuonyesha mwelekeo wake kwa Taifa. Kwa sasa ni muda wa kugawa majukumu baada ya wafanyakazi kufahamu mwelekeo wa Rais. Jaribu kusoma vitabu vya masuala ya siasa na uongozi.

Huwezi kumlinganisha Rais Magufuli na Rais Kikwete kwa sababu hata haiba wanatofautiana sana achilia mbali utendaji wao. Kikubwa zaidi, Majukumu ya kitaifa wakati wa utawala wa Rais Kikwete ni tofauti na majukumu ya kitaifa wakati huu wa utawala wa Rais Magufuli

Sitaki kumtetea Lowassa kwani hata msimamo wangu dhidi yake unafahimika. Unaweza kupitia post zangu kuhusu Lowassa ukipenda. Ninachosema ni kwamba hicho alichokizungumza Lukuvi kwake ametumia hilo la shamba la Lowassa kama mtaji wa kisiasa na sio utendaji wa uadilifu kama ambavyo angetaka ieleweke. Lengo langu ni kwamba kwenye umiliki wa mali bila kufuata sheria za nchi kwa viongozi wengi ni jambo la kawaida sana na hakuna anayejali kwani wanajua mkono wa sheria unaangalia kundi fulani kwenye jamii. Sitaki kukulazimisha kuhusu ccm kuhakikisha inabaki madarakani hata kwa machafuko ila kama hujui kusoma hata picha huelewi?

Hili unalosema kwamba pattern za kisiasa ni kama unatamani afanye vizuri zaidi ya hapo. Ukweli ni kuwa iwapo hatawabana hawa tunaowatuhumu yeye, basi ujue hakuna kitakachoendelea kwani watu wanaimba mdomoni pamoja na yeye lakini hawako naye moyoni kwani anagusa maslahi yao.
 
Asipotaja hawa jamaa watamfilisi wakiamini wanaiwajibisha serikali.
Na wameamua kumpiga nyundo za kichwa!

Bila kufahamu kama yeye ndiye mwenye makosa anaweza akadhani baadhi ya wabunge wa CHADEMA wanamfanyia kampeni chafu ili wammalize zaidi kisiasa!
 
Inaonekana bila kumtaja mwanaume Lowasa mnapata homa eeee, fanyeni kazi kwa bidii au ndo mmesha kunywa kinywaji cha aina ya Kitwanga!!
Hata shetani anatajwa sana!

Nani amekuambia hatufanyi kazi kwa bidii?

Lowassa inabidi awatajie CHADEMA mali zake ili wasiendelee kumpiga nyundo za kisiasa.
 
Fisadi gani ambae yupo nje ya CCM lakini bado mmekosa namna ya kumshughulikia zaidi ya kulia lia tu kwenye vikao vya kamati kuu (CCM)?

Fisadi gani ambae mbele ya TV (live kitaifa) alisema wazi kwamba Richmond ni ya Kikwete na kwamba aliamua kufuta mkataba lakini Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Luhanjo akasema hapana kwa sababu Rais amese mkataba usifutwe? Lowassa akaenda mbali na kusema kama mnataka zaidi tukutane mahakamani. Hadi leo kimyaaaa. Hamuwezi thubutu kwani mnajua mtaumbuka.

Tangia wakati huo, wananchi wakaelewa pumba ziwekwe ungo upi, na mchele ungo upi. Wakaelewa kwanini Mwakyembe alisema bungeni kwamba kamati yake inalazimika kuficha mengine ili kuilinda serikali. Serikali gani hiyo inayolindwa baada ya kumtoa Waziri Mkuu, upo hapo?

Wananchi walishagutuka. Walishaelewa kwamba utawala wa awamu ya nne ulijaa fitina na nguvu za giza. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa Urais, wananchi walimpa Lowassa ushindi kabla hamjaleta wataalam wenu wa nje kuja kutungua takwimu angani kabla hazijateremka kwa Lubuva pale NEC. Na Lowassa amerudia mara nyingi kwamba 'hata Magufuli anajua kwamba ushindi wake ni wa kuiba kura', lakini katika hili, hadi leo, CCM na serikali yake kimyaaa.Hamuwezi thubutu kwani mnajua mtaumbuka.

Katika hili danganyeni wengine, sio wananchi waliompa kura ya ushindi Lowassa, ambao pamoja na kutoboa kibaba cha kura, zikabakia 6 million plus.
kamanda naona hujitambui. aliyekuwa akipiga mbinja kuhusu ufisadi ni nani kati ya ccm na upinzani. khaaaa... ! au unajifanya huoni wala kusikia. nadhani wewe na wengineo ndio mliiondoa list of shame mtandaoni. wananchi sio wajinga. hatuisahau list ile. haya ulinza maandiko ya Kubenea miaka yote kuhusu ufisadi huu.wakidai wana ushahidi tosha. haya rejea maneno mbalimbali ya Mbowe ,Lissu Mnyika Dr Slaa Mdee mchungaji Msigwa na wengine wengi. hata clip za Lema hujaziona.jamani wewe unaishi wapi. sasa nani aliyeshupalia ufisadi huu
 
Lowasa mwizi sana ekari laki tatu amejimilikisha bila kulipa hata senti tano...ameifilisi sana hii nchi.
 
Na wameamua kumpiga nyundo za kichwa!

Bila kufahamu kama yeye ndiye mwenye makosa anaweza akadhani baadhi ya wabunge wa CHADEMA wanamfanyia kampeni chafu ili wammalize zaidi kisiasa!
Na pengine ndo hivyo. Wanajitoa ufahamu si unajua siasa za hapa bongo, ni kujitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom