MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Uongozi bora ni msingi wa kujenga jamii yenye maadili mema, kuthamini utamaduni, uadilifu, kuheshimu utawala wa sheria na kutokuwepo na rushwa na maovu mengine.
Uwazi wa viongozi kuhusu mali zao na mienendo yao ya kiuongozi ni takwa la chini kabisa katika uongozi wenye kuzingatia misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji kwa umma.
Kwa msingi huu ndiyo maana vyama vya siasa kama ACT-Wazalendo kinamtaka kikatiba kila kiongozi wake kutaja mali zake.
Umuhimu wa dhana ya uwazi umedhihirika ndani ya CHADEMA baada ya kujikuta baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakimshambulia Edward Lowassa bila kufahamu kutokana na kutofahamu vizuri mali zake.
Mbunge Mnyika alianza kulalamika na kulaani wale ambao wamezuia Mradi wa Maji kuwafikia wana Dar es Salaam kwa sababu wamejenga nyumba juu ya njia ya mabomba ya maji na kusababisha mradi wa maji kusimama. Bahati mbaya Mnyika hakufahamu kuwa aliyejenga hiyo nyumba ni Kaka yake na Edward Lowassa ambaye alipewa kiwanja na Edward Lowassa kinyume cha sheria wakati akiwa Waziri wa Ardhi na Makazi mwaka 1993–1995.
Mbunge mwingine aliyelalamika na kulaani ni Mbunge wa CHADEMA wa Jimbo la Monduli, Julius Karanga wakati akichangia majadiliano ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, bungeni kuhusu dhuruma wanayofanyiwa wananchi wa Monduli.
Karanga aliitaka serikali iwagawie wananchi shamba la Makuyuni lenye ekali zaidi ya 380,000 ililopo wilayani Monduli kwa sababu serikali imelitelekeza. Karanga alidhani mwenye shamba kwa sasa ni serikali bila kufahamu kuwa baada ya serikali kulitaifisha kutoka kwa Mfanyabiashara Stein ili ligawiwe kwa wananchi, Edward Lowassa aliamua kujimilikisha hilo shamba.
Mbunge huyu pamoja na wabunge wangine wa CHADEMA walipigwa butwaa baada ya kuambiwa hilo shamba alijimilikisha Edward Lowassa lakini Waziri Lukuvi, akasema kuwa serikali imesikia kilio cha mbunge Karanga kwa sasa iko mbioni kuligawa kwa wananchi.
‘’Kama Mheshimiwa Mbunge, Karanga alikuwa hajui kwamba shamba hilo la makuyuni alijimilikisha Lowassa, basi imekula kwake, shamba linachukuliwa na serikali na kuligawa kwa wananchi. Najua kazi ni ngumu kwako, lakini naomba tushirikiane shamba hili liende kwa wananchi. "Ninayo hati hapa ya shamba hilo imesainiwa na Lowassa, nasema tutairekebisha ili shamba hilo ligawiwe kwa wananchi." alisema Lukuvi huku wabunge wengine wakicheka.
Lowassa anatakiwa awasaidie wana CHADEMA kwa kuwaeleza mali zake ili wasijikute wanampiga ‘’madongo’’ ya kisiasa wakidhani wanaipiga serikali bila kufahamu kutokana na ukosefu wa uwazi kutoka kwa Lowassa.
Hii inadhirihisha kuwa wanaCHADEMA wengi hawamjui Edward Lowassa pamoja na kuimba nyimbo zinazosema Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko.
Niliwahi kusema, katika mambo yote ambayo Lowassa amelitendea haki taifa ni kuhama CCM.
VIDEO ikionyesha nyumba ya Kaka yake Edward Lowassa ikibomolewa kwa nguvu na serikali kupisha ujenzi wa bomba la maji.

Iliyokuwa nyumba ya Kaka yake na Edward Lowassa ikibomolewa kupisha ujenzi wa bomba la Maji kwa wakazi wa Dar es Salaam