Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

Ukweli gani tena? Mbona alikwishasema na kurudia kile anachokijua kwamba Kikwete hawakukutana barabarani? Wahenga waliosema: Nionyeshe rafiki yako, nikuambie tabia yako walikosea?

"........Nionyeshe rafiki yako, nikwambie tabia yako!"

Kwa hivyo ni Zero toa Sifuri?
 
Kama hii ni kweli basi huyu jamaa anazidi kuonyesha jinsi asivyostahili kuwa Rais wa nchi yetu 2015. Yaani kuna madudu yalifanyika kuhusiana na mkataba wa Richmond/Dowans naye anayajua lakini kaamua kutuficha Watanzania miaka yote hii, sasa anaona maslahi yake yanataka kuharibika ndio anataka kutueleza nini kilichojiri!!!! Mwalimu aliona mbali sana pale aliposema huyu jamaa hastahili kabisa kuwa Rais wa nchi yetu.
Mkuu hivi si inasemekana kulikuwa na ripoti mbili?
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Hana lolote huyo. Alikuwa wapi siku zote? Anadhani tutamwamini? Anajidanganya
 
So he is tryin to Blackmail his way out of troubles, mwache avunje mti alokalia. Sisi wengine tutafurahi tu.
 
Mkuu hivi si inasemekana kulikuwa na ripoti mbili?

Inawezekana Mkuu lakini sina hakika, inaelekea Magamba wameingiwa na woga wa hali ya juu katika kuwafukuza Lowassa na Chenge. Kwa mara nyingine tena inaelekea Magamba yatashindikana kuvuliwa. Tusubiri ili kujua kitakachojiri.
 
wanapenda wayoyaita magamba yawavuke, lakini bahati mbya yako miilini mwao. Wakiyavua yakavulika, wao watakuwa uchi maana nguo yao ni hayo. Na kama wakijitahidi sana kuyavua, tutayaona makovu makubwa ya ufisadi yaliyo miilini mwao na hilo linogopwa zaidi. Wanaowaita mahamba si wakubwa wala nchi, bali ni wale wanaovizia mifupa idondokayo mezani pa wala nchi. Lowasa alikuwa waziri mkuu shupavu, Chenge alikuwa mwanasheria makini. Hawawezi kufanya ujinga wowote ambao wanaujua matokeo yake. Kwa hili lazima walikuwa wengi wakijua hakuna wa kuwauliza matokeo yake. Narudia; kama wao ni magamba,kama ni ya mti basi mti wenyewe upo na magamba hayo yakikwatuliwa mti nao utajifia kwa kunyauka. Na kama ni ya nyoka basi nyoka huyu ni wa jamii ya kenge asiye na desturi ya kujivua gamba la akilazimisha kujivua basi kenge nalo libaki bila ngozi nal bila shaka litajifia.
 
Lakini kwa watuy makini EL must be stupid and ignorant. Ina maana anjua exactly about Richmond!! Sasa ni kwa nini hasemi Anasubiri nini? Ina maana sio MZALENDO NAYE NI MZANDIKI TU NA MWIZI!! Mwallimu aliwahi kusema ' Edward you are Corrupt' Na ndivyo alivyo! Maana asingekuwa hivyo angeisha toa tamko au ni kura ya turufu wa 2015? Mzandiki basi. I dont buy his porojo!!!
 
Kama kweli ndani ya NEC wote wanajiona kuwa ni wasafi sidhani kama ingewachukua muda mrefu kiasi hiki kumsulubu Lowasa... hii ishu ya Richmond kuna jambo linafichwa na Lowasa amefanywa mbuzi wa kafara, tatizo kila mtu anaogopa kumuanza...
 
Kwa hiyo hasemi ukweli kwa sababu yuko NEC.....Huu uongo mwingine hauna hata kipimo..

ithis is not lowassa. Lazima ni marafiki wake au wapambe wanaotamani awe rais. Huyu ndugu mjanja lowasa hawezi kuropoka hivi. Nakataa, hawa ni wapambe nuksi. Ila kama ni yeye ni jambo zuri pia kujua kuwa yuko kwenye kona amepanick na ni vizuri sie kujua vitu vinavyomchemsha akaloose cool.
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Yeye Lowasa anajua kabsaa amechelewa! Anachotegemea ni huruma ya JK!
 
kwanini anasubiri mpaka aenguliwe?? angekuwa mzalendo wa kweli anayefahamu kitu kuhusu richimond angesema sasa hivi kabla hajaondolewa na NEC, EL ni wale wale tu waizi na hakuna jipya!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Too little too late; he should be advised by his handlers that this strategy could backfire on him!! Mkweree atammaliza hata kama hawakukutana uchochoroni!! Lowassa should be wise enough to know by now that in politics you never have permanent friends; Nyerere and Kambona's friendship could be a good reference point for him.
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Mmh! Cdhan kama wanaweza mng'oa huyo mmasai.
 
Unafiki wa watu wa ccm, Hata kama alikubali kuiba kwa niaba bado mwizi ni yeye na nashangaa hakuna mpango wa kumpeleka mahakamani
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima
Hata akitaja ataendelea kudharaulika, kwasababu angekuwa Mzarendo angesema tuu bila kujari kitu chochote. Lowasa ni fisadi tuu
 
Hafai huyo,si aseme!
Sasa ndo napata picha y mwakyembe alosema ana meng kuhusu richmond
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Si alisema tatzo ni uwaziri mkuu,sa cri gan?
Lowasa bana, anazeeka vibaya sana; anatuambia kuwa anasiri kubwa ya ukweli wa Richmon, na anajua kuwa tunachokifaham sisi Watanzania wa kawaida kuhusu Richmond ni uwongo wa maksudi! Kwa kitendo chake cha kuwaficha watanganyika ajue ni kushiriki uhalifu! Tukilegeza kamba huyu jamaa atakuja kuwa raisi wa Tanganyika Miaka michache ijayo, na nina hakika ataendeleza siasa na utendaji wa kulindana kimakundi kama anavyofanya Mkweere! Simwamini hata kidogo huyu mzee.
 
siyo kwamba anazeka vibaya anatafuta mtu wa kuzeeka nae sjui atakuwa Nape au Jk, yetu macho
 
Kwahiyo EL anasubiri wamwage ugali yeye amwage mboga, mbona itakuwa raha!!
 
Back
Top Bottom