Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

CCM haina uwezo wa kuondoa rushwa kwa sababu kila kiongozi wa ccm amewahi kuona mtu anatoa rushwa au kukutoa;hivi mwenyekiti wao anao ujasiri wa kuwashughulikia watoa rushwa walio mpa urais.Pia ccm iliwahi kumtetea ED kwenye Richmond leo imeona ufisadi upi aliotenda?
 
TAARIFA KUTOKA KWA MTU WA KARIBU NA EL

MAPACHA WATATU EL,AC NA RA ,WAMEKUWA WAKIFANYA VIKAO KWA SKYPE TOKEA TAMKO LA CHAMA LA KUTAKA WAACHIE NAFASI ZAO,MPASHAJI ANASEMA MAPACHA HAO WAMEKUWA WAKIFANYA ONLINE MEETING KILA SIKU KWA ZAIDI YA MASAA SABA KWA KUTUMIA SKYPE KWANI WAMEKUBALIANA WASIKAE PAMOJA KUTOKANA NA TISHIO LA KUWAUA AMBALO MMOJA WAO ALILINASA KUTOKA KWA SHUSHUSHU WAKE AMBAYE NI MMOJA WA VIONGOZI WA VIJANA WA CHAMA CHA MAGAMBA ALIYEWEKWA KWENYE MPANGO HUO NA CHAMA HICHO CHA MAGAMBA

MY TAKE;hawa mapacha wanajipanga kujibu mapigo na kuufutilia mbali utawala wa JK;;,UWEZO WANAO,SABABU WANAZO NA NGUVU WANAYO.

NGOMA INOGILE,VITA VYA PANZI KUNGURU TWALAAAA

haya sisi masikini watanzania yetu macho tunachotaka ni roho zetu watuachie kwani haya maswala ya maendeleo ni ndoto kwetu.
 
Hatoswi mtu hapo, Jakaya ni tunda la kazi za Lowassa na Rostam; bila ya hao wawili hakuna Kikwete wala Rais wa Tanzania!! Hawa jamaa wana uwezo wa kuingusha serikali ya Tanzania na hili lilikwishathibitishwa na Pinda bungeni aliposema kuwa anawaogopa hawa mafisadi kwani wana uwezo wa kuiyumbisha nchi!! Watch out those are words from the PM uttered in parliament!

Tunda? Sema uozo wa hao wawili!!
 
nakumbuka sentensi ya kwanza JK alipoingia madarakani alisema URAIS HAUNA UBIA!

leo ukimfata ukamkumbusha hii kauli....atakubishia sana na atasema hakuwahi kutamka namna hiyo.........ki ukweli ni kwamba jk hana ujanja, na hwa jamaa wakiamua hamalizi mda wake pale magogoni.......na ajilaumu yeye kwa kiburi chake....mwaka jana aliwapeti pet hawa jamaa majimbo kwao.....leo amewageuka tena kwa kutojitambua....hakika hayuko salama yeye na ccm yake
wacha hawa jamaa wapige hizo online meeting zao huku wakiweka swa mambo ya pesa zao huko nje ndo utawajua
 
hakuna marefu yasiyo na ncha........
Mwisho wa ubaya ni aibu.........
Hao mapacha watatu.... Kiama chao kimefika.....
Masikiniii.........wanaondoka kwenye ulingo wa siasa kwa aibu kubwa........
 
  • Thanks
Reactions: Ame
hapo tutakua tumeiuza tanzania.watu kama hao(mapacha3) ni bora wanyongwe wakafie mbali au wapigwe tu shaba!!
 
Huu ni mwendelezo wa sinema wanayotuonyesha Chama Cha Magamba. Ulishawahi kuona wapi mtu anatoswa kwa kubebembelezwa? Ulishaona wapi mtu anayekata mkono unaomlisha? Nina hakika hata akina Nape wanacheza ngoma wasioijua. Wanapiga makelele majukwaani bila kujua kuwa gamba ni Mzee mwenyewe! Hivyo vikao hata Bwana Mkubwa Kabisa anahudhuria. Alivyo dhaifu, masikiini hajui hata cha kufanya, anabaki anaugilia moyoni
 
From Boys II Men to Mapacha Watatu, haya Mramba nae kundi gani?Zakia Meghji nae? mbona yako magamba meengi tu na hawatuambii muarabu wa Dowans kalipwa au hajalipwa?

Ni hivi kamanda Msekwa ndo alisimama na kutaja hawa mapacha, hakukuwa na mwingine aliyethubutu kuongoza list. Hawa jamaa ndo ikala kwao ila kiukweli wako wengi sana mle chamani ndio maana hata Rostam aliposimama kujitetea, alisema mimi kama fisadi na watu hawanipendi basi nisingeshinda ubunge na JK asingepata kura zote hizo toka jimboni kwangu.

Baada ya hapo alisimama meghi na kumshambulia sana RA kuwa yeye ndo chanzo cha matatizo ndani ya chama na anapaswa aondoke. Baaada ya kushambuliwa kote huku na wajumbe karibu wote wengine wakinong'ona kwa chini bila kupaza sauti.

Ndipo RA alisema hivi kwa kimombo ''you won but the battle is not yet over'' alimwambia kauli hii meghi wakati kikao kimeisha hata ukifatilia kikao kile aliyekuwa anaongoza kikao ni Kinana sio JK.

JK alikuwa amekalia kiti tu pale aliyependekeza NEC na CC zijizulu ni Kinana na ndiye alipendekeza kutoswa kwa hawa jamaa. JK alikuwa pale kukubaliana na kila hoja anayotoa Kinana na mwisho akawa anasema, '' jamani tumekubaliana humu ndani wote, wala tusitafutane ubaya. Wote huu ni dalili ya uoga.


 
hakuna marefu yasiyo na ncha........
Mwisho wa ubaya ni aibu.........
Hao mapacha watatu.... Kiama chao kimefika.....
Masikiniii.........wanaondoka kwenye ulingo wa siasa kwa aibu kubwa........

ni ngumu sana kufa kirahisi hawa jamaa.........watakufa na wengi wakitoka ccm kama wataamua kuweka ukweli wote hadharani....hata jk atango'ka
 
TAARIFA KUTOKA KWA MTU WA KARIBU NA EL

MAPACHA WATATU EL,AC NA RA ,WAMEKUWA WAKIFANYA VIKAO KWA SKYPE TOKEA TAMKO LA CHAMA LA KUTAKA WAACHIE NAFASI ZAO,MPASHAJI ANASEMA MAPACHA HAO WAMEKUWA WAKIFANYA ONLINE MEETING KILA SIKU KWA ZAIDI YA MASAA SABA KWA KUTUMIA SKYPE KWANI WAMEKUBALIANA WASIKAE PAMOJA KUTOKANA NA TISHIO LA KUWAUA AMBALO MMOJA WAO ALILINASA KUTOKA KWA SHUSHUSHU WAKE AMBAYE NI MMOJA WA VIONGOZI WA VIJANA WA CHAMA CHA MAGAMBA ALIYEWEKWA KWENYE MPANGO HUO NA CHAMA HICHO CHA MAGAMBA

MY TAKE;hawa mapacha wanajipanga kujibu mapigo na kuufutilia mbali utawala wa JK;;,UWEZO WANAO,SABABU WANAZO NA NGUVU WANAYO.

NGOMA INOGILE,VITA VYA PANZI KUNGURU TWALAAAA

Mkuu Son of Peasant, usije jidanganya hata kidogo juu ya EL,RA na Chenge.
Wakicheza na JK hawajui wanachezea nini.
Madaraka ya Rais wa Jamhuri ni makubwa saana and they wont know what hit them.
Sasa hivi JK na Rais ni kitu kimoja, ndani ya Jamhuri sasa hivi si ajabu vyombo vyote viko alert kwa tishio lolote toka kwao.
Kama una uhusiano nao hawa jamaa washauri waende Dubai au Costa Rica kutoa madudu yao hadharani.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom