Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 20, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  • Wasubiri barua zao kujibu mapigo, CCM yawaita Mapacha Watatu

  WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijipanga kuwaandikia barua makada wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga) na Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), makada hao wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili watoe kile waliochokiita maamuzi mazito dhidi ya CCM, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.

  Makada hao maarufu kwa jina la Mapacha Watatu, wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili wavunje ukimya na kueleza upande wa pili wa shilingi kwa madai kuwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), hakukuwa na azimio lolote lililopitishwa la kuwataka wapewe siku 90 za kujiengua na pia hakukuwa na azimio la kuandikiwa barua.

  Mmoja wa makada hao, aliliambia Tanzania Daima Jumatano mjini Dodoma kuwa Rais Jakaya Kikwete na chama chake wamefanya jambo la hatari dhidi yao pengine kwa kujua au kutokujua lakini lazima wajibu mapigo ili jamii ielewe.

  "Sitaki kuzungumza sasa hivi na huo ndio msimamo wetu. Waswahili wanasema akutukanaye hakuchagulii tusi, tunaangalia, tunafuatilia kwa karibu mambo yote kuanzia ndani ya vikao hadi sasa kinachoendelea kwenye mikutano ya hadhara hakika ni udhalilishaji wa hali ya juu. Tusubiri barua, tutajua la kufanya," alisema kada huyo, mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi.

  Aidha, baadhi ya watu wa karibu walidokeza kuwa kitu cha kwanza kinachotarajiwa kufanywa na makada hao mara tu baada ya kukabidhiwa barua zao, ni kurejesha kadi za CCM, hatua itakayofanya wapoteze majimbo yao ya uchaguzi, lakini watahakikisha lazima chama kithibitishe ufisadi wao.

  Kada huyo hakutaka kuzungumza kwa undani jinsi walivyopokea maamuzi ya NEC na hatua inayoendelea kwenye mikutano ya hadhara inayohutubiwa na Katibu Mkuu, Willson Mkama, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa sekretarieti mpya ambao jana walitua mkoani Iringa.

  Katika mikutano ya hadhara inayodaiwa kuwa ni ya kujitambulisha, Nape amekuwa akiwataja Mapacha Watatu: Lowassa, Rostam na Chenge kwamba wametakiwa kujiondoa kwenye ujumbe wa NEC ndani ya siku 90, vinginevyo watang'olewa kwa nguvu.

  Nape ambaye hadi sasa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, alienda mbali kwa kusema watuhumiwa hao hivi karibuni wataandikiwa barua na kuorodhesha tuhuma zao; na kusisitiza azimio la NEC la kuwataka wang'oke vinginevyo wataenguliwa na chama.

  Hata hivyo, katika hatua nyingine, azimio la kutoa siku 90 kwa watuhumiwa hao wa ufisadi limeibua vita ya kisiasa kati ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na makada hao.

  Wadadisi wa mambo ya siasa, wanaona kuwa kilichotokea mjini Dodoma ni muendelezo wa minyukano ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015 na siku za baadaye pia kwani mkakati wa kujivua gamba, ulipangwa makhsusi kwa ajili ya kuwaengua wao wakati orodha ya mafisadi ndani ya chama hicho ni ndefu.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe wa NEC wanaodaiwa kupanga kusuka mpango huo, umethibitisha pasipo shaka kwamba Rais Kikwete, aliendesha vikao kwa kupanga wajumbe kutoa hoja za kuwang'oa Chenge, Lowassa na Rostam.

  Kiongozi mmoja wa siku nyingi wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano anasema hoja ya kutaka Kamati Kuu na sekretarieti nzima kujiuzulu, ililenga kuwatema Mapacha Watatu, ndani ya vikao hivyo vyenye nguvu kwa njia ambayo ingemuepusha Rais Kikwete katika lawama za moja kwa moja.

  "Chama chenye maadili, falsafa, mwongozo na itikadi, hakiwezi kuwapigia kampeni watu wanaohusishwa na ufisadi kwamba wanafaa huku kikisema hakuna ushahidi, halafu baada ya kupata ubunge na wengine hata kuongoza kamati nyeti za Bunge, chama hichohicho kinawataka watoke kwa madai kuwa hawafai. Ushahidi wa sasa kwamba hawafai, wameupata wapi?" alihoji mjumbe mmoja wa NEC.

  Wadadisi wa mambo ya siasa wanaohoji hatua hiyo, wanasema uongozi mpya wa CCM ulipaswa kujikita kueleza matarajio ya chama siku zijazo na mikakati ya kujiimarisha na kueleza maazimio mengine ya NEC.

  "Nape na wenzake hapaswi kuendelea kumzungumzia Lowassa na wenzake; haya mambo wameyamaliza kwenye vikao. Wanapaswa kueleza matatizo ya msingi ya chama na taifa kwa ujumla, hasa utekelezaji wa Ilani ya CCM," alisema.

  Anasema ingawa wanakubaliana kimsingi na hatua ambazo CCM inatakiwa kuzichukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wanashangazwa na hatua ya Nape kutangaza azimio ambalo si sehemu ya mambo yaliyojadiliwa na kukubalika ama kwa kura au kwa kauli moja na wajumbe wote.

  Hatua ya Nape inafananishwa na matukio ya hivi karibuni hususan wakati John Chiligati akiwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi kwamba amepata kutaja mara kadhaa taarifa isiyo sahihi ya maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu tofauti na kile kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo.

  Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kuilipa au kutoilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai Tanzania karibu shilingi bilioni 100.

  Chiligati anatajwa pia kupata kutoa maazimio ya kupotosha wakati aliposoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Safi sana, acha Chama Cha Magamba kife kabisa!!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Wakuu picha ndio kwanza linaanza.

  Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto
  • Wasubiri barua zao kujibu mapigo, CCM yawaita Mapacha Watatu

  na Mwandishi wetu

  [​IMG] WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijipanga kuwaandikia barua makada wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga) na Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), makada hao wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili watoe kile waliochokiita maamuzi mazito dhidi ya CCM, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.
  Makada hao maarufu kwa jina la Mapacha Watatu, wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili wavunje ukimya na kueleza upande wa pili wa shilingi kwa madai kuwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), hakukuwa na azimio lolote lililopitishwa la kuwataka wapewe siku 90 za kujiengua na pia hakukuwa na azimio la kuandikiwa barua.
  Mmoja wa makada hao, aliliambia Tanzania Daima Jumatano mjini Dodoma kuwa Rais Jakaya Kikwete na chama chake wamefanya jambo la hatari dhidi yao pengine kwa kujua au kutokujua lakini lazima wajibu mapigo ili jamii ielewe.
  “Sitaki kuzungumza sasa hivi na huo ndio msimamo wetu. Waswahili wanasema akutukanaye hakuchagulii tusi, tunaangalia, tunafuatilia kwa karibu mambo yote kuanzia ndani ya vikao hadi sasa kinachoendelea kwenye mikutano ya hadhara hakika ni udhalilishaji wa hali ya juu. Tusubiri barua, tutajua la kufanya,” alisema kada huyo, mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi.
  Aidha, baadhi ya watu wa karibu walidokeza kuwa kitu cha kwanza kinachotarajiwa kufanywa na makada hao mara tu baada ya kukabidhiwa barua zao, ni kurejesha kadi za CCM, hatua itakayofanya wapoteze majimbo yao ya uchaguzi, lakini watahakikisha lazima chama kithibitishe ufisadi wao.
  Kada huyo hakutaka kuzungumza kwa undani jinsi walivyopokea maamuzi ya NEC na hatua inayoendelea kwenye mikutano ya hadhara inayohutubiwa na Katibu Mkuu, Willson Mkama, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa sekretarieti mpya ambao jana walitua mkoani Iringa.
  Katika mikutano ya hadhara inayodaiwa kuwa ni ya kujitambulisha, Nape amekuwa akiwataja Mapacha Watatu: Lowassa, Rostam na Chenge kwamba wametakiwa kujiondoa kwenye ujumbe wa NEC ndani ya siku 90, vinginevyo watang’olewa kwa nguvu.
  Nape ambaye hadi sasa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, alienda mbali kwa kusema watuhumiwa hao hivi karibuni wataandikiwa barua na kuorodhesha tuhuma zao; na kusisitiza azimio la NEC la kuwataka wang’oke vinginevyo wataenguliwa na chama.
  Hata hivyo, katika hatua nyingine, azimio la kutoa siku 90 kwa watuhumiwa hao wa ufisadi limeibua vita ya kisiasa kati ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na makada hao.
  Wadadisi wa mambo ya siasa, wanaona kuwa kilichotokea mjini Dodoma ni muendelezo wa minyukano ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015 na siku za baadaye pia kwani mkakati wa kujivua gamba, ulipangwa makhsusi kwa ajili ya kuwaengua wao wakati orodha ya mafisadi ndani ya chama hicho ni ndefu.
  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe wa NEC wanaodaiwa kupanga kusuka mpango huo, umethibitisha pasipo shaka kwamba Rais Kikwete, aliendesha vikao kwa kupanga wajumbe kutoa hoja za kuwang’oa Chenge, Lowassa na Rostam.
  Kiongozi mmoja wa siku nyingi wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano anasema hoja ya kutaka Kamati Kuu na sekretarieti nzima kujiuzulu, ililenga kuwatema Mapacha Watatu, ndani ya vikao hivyo vyenye nguvu kwa njia ambayo ingemuepusha Rais Kikwete katika lawama za moja kwa moja.
  “Chama chenye maadili, falsafa, mwongozo na itikadi, hakiwezi kuwapigia kampeni watu wanaohusishwa na ufisadi kwamba wanafaa huku kikisema hakuna ushahidi, halafu baada ya kupata ubunge na wengine hata kuongoza kamati nyeti za Bunge, chama hichohicho kinawataka watoke kwa madai kuwa hawafai. Ushahidi wa sasa kwamba hawafai, wameupata wapi?” alihoji mjumbe mmoja wa NEC.
  Wadadisi wa mambo ya siasa wanaohoji hatua hiyo, wanasema uongozi mpya wa CCM ulipaswa kujikita kueleza matarajio ya chama siku zijazo na mikakati ya kujiimarisha na kueleza maazimio mengine ya NEC.
  “Nape na wenzake hapaswi kuendelea kumzungumzia Lowassa na wenzake; haya mambo wameyamaliza kwenye vikao. Wanapaswa kueleza matatizo ya msingi ya chama na taifa kwa ujumla, hasa utekelezaji wa Ilani ya CCM,” alisema.
  Anasema ingawa wanakubaliana kimsingi na hatua ambazo CCM inatakiwa kuzichukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wanashangazwa na hatua ya Nape kutangaza azimio ambalo si sehemu ya mambo yaliyojadiliwa na kukubalika ama kwa kura au kwa kauli moja na wajumbe wote.
  Hatua ya Nape inafananishwa na matukio ya hivi karibuni hususan wakati John Chiligati akiwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi kwamba amepata kutaja mara kadhaa taarifa isiyo sahihi ya maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu tofauti na kile kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo.
  Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kuilipa au kutoilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai Tanzania karibu shilingi bilioni 100.
  Chiligati anatajwa pia kupata kutoa maazimio ya kupotosha wakati aliposoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.  [​IMG]
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  CCM wasiwabambike mzigo wa lawama RA, EL na Chenge. Ni lazima watafute chanzo cha tatizo ni nini bila kuona uvivu wa kufikiri.
  Kwa upande wangu naona tatizo kubwa lililowafikisha hapo walipo ni kuliacha azimio la Arusha na kuanzisha azimio la Zanzibar.

  Karibu viongozi wengi ndani ya CCM walitumia madaraka yao katika kufanya biashara na kujilimbikizia mali kitu ambacho ni mwiko katika azimio la Arusha.

  Sasa kwanini lawama zote ziwaende hawa watu watatu na wala si kwa CCM yote?. CCM ilibariki viongozi kujishughulisha na biashara. Ni sawa na mtu umevaa nguo zako bila ya kubadilisha kwa muda wa mwezi mzima, leo unavua na kubadilisha shati tu lakini soksi, chupi, suruali ni zilezile. CCM yote ni chafu hivyo inatakiwa kuondoka madarakani.
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Thanks GOD! keep it up! make sure the whole CCM is down for ever......:yawn:
   
 6. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hakuna moto wowote wanatapatapa tu.
   
 7. m

  makaptula Senior Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  1.Mi nafikiri kujiuzulu sio suluisho hata kidogo, inabidi washitakiwe kama waujumu uchumi na mali zote walizo kuwa nazo zitaifishwe kwa manufaa ya Uma.
  2.Vile vile kama hoja kuu ya kujiuzulu ni ufisadi, JK inabidi awe wa kwanza kuondoka ikulu kwani yeye ni miongoni mwao la sivyo hawa mabwana wakiondoka akabaki yeye na wenzake watakuwa katika wakati mgumu sana wa kuiongoza hii nchi kwani hawa mabwana ni mamafya wakimataifa.
  3. Na kama hawa mabwana watajiuzulu nafikiri unaweza ukawa mwisho wa CCM,
  Wanaweza fikiria wajenga kumbe wabomoa
   
 8. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa mmechesha, siku zote mmekuwa wapinzani wa ufisadi, Leo mmekuwa watetezi wa mafisadi kwa Sababu ya chuki yenu dhidi ya CCM. Kwa hili CCM imewapiku nwa wananchi wamehamia. Ninyi na CDM yenu mtabaki mahameni katika moto wa milele.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Let's get ready to rumbleeeeeeee.....wacha waparurane ili Chama Cha Mafisadi/Majambazi/Magamba kisambaratike kabisa maana kikwazo kikubwa cha maendeleo nchini mwetu ni CCM.
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tujikumbushe yaliyotokea mwaka jana.....................
  [​IMG]

  [​IMG]
   
 11. kwempa

  kwempa Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Oneni...nani gamba kubwa
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  RL, RA,AC wasikubali kuondoka kirahisi as haiwezekani chama lote ni la mafisadi halafu watatu tu watumiliwe
  Komaeni mapacha watatu with time JK atasalim amri
   
 13. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ala! Wewe huijui ccm! Hata kama uko ndani bado hujajua kinachoendelea ndani, unaamini unawezakugusa ubaya wa El na Ra bila kuigusa ccm? Hapo ndipo mashaka yapo! Hapa elewa hatuongelei Cdm tunaongelea ccm, haya yote anayofanya Kikwete na Riz ni kwa mshahara upi? Je hiyo pesa ya ufisadi hakuna mahali popote inamgusa? Huo ndio wasiwasi tu kuwa kama kweli wako serious na wanayoyatangaza kuwatosa basi nina wasiwasi na ccm kuendelea kuwa hai! Tuone lakini maana pia inawezekana pia shetani mara moja kutenda jema ili akupate vizuri akuue!
   
 14. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  I say thanks for this useful post, sijui prezidaa alikuwa anafikiri nini hapo, hii ni kuwafanya watanzania wajinga wasio na uwezo wa kifikiri, ni bora hata jk angeacha wakajipigia kampeni wenyewe, sidhani kama wangeshindwa bila kikwete, pili kwani jk aliwapigia kampeni wagombea wote wa ccm, sasa kwa nini hawa. This was a big mis-calculation.
   
 15. Mwanahakij

  Mwanahakij Senior Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mafisadi wajitoe kwenye Chama cha Magamba waanzishe Chama cha Mafisadi, simple as that!
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu ina maana mimi sijaelewa au? Hao mabwana watawasha moto au watagawa mapesa? Nielewesheni aisee!
   
 17. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunatakiwa tuwe macho si kwamba tunawatetea Mafisadi la hasha. Ila tunataka kujua wamepata wapi ujasiri leo wa kusema kuwa LOWASSA, ROSTAM, CHENGE ni mafisadi? Kwani siku si nyingi wenzetu wa CHADEMA wallisema kuwa mafisadi CCM wote walikuwa upande wa kina ROSTAM, LOWASA,CHENGE. Na waliwapigia kampeni ya nguvu huyu huyu RAIS wetu alikwenda katika majimbo yao jamani tunataka CCM wadhibitishe sasa ufisadi wao hilo tu tunalitaka jamani.

  Sio tunawatetea, wakishindwa ita wakosti sana na mtakuja kuona wenyewe.
   
 18. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hatma ya CCM imefika ukingoni, kwa hatua ya kuwavua EL, AC & RA ni sawa na laana kwa chama. JK katu hatoweza kuitawala nchi hii na atapata laana kali ya muumba toka kwa watanzania wote (waislamu & wakristo), nayasema haya kwani ni jambo ambalo...WAMEKUWA PAMOJA, WAMEPANGA MIPANGO PAMOJA, WAMEFAULU PAMOJA, WAMEINGIA IKULU PAMOJA leo hii uwashushie dhambi kama hii wao tu?

  Ni uonevu usio kifani, mkuu wa nchi anapaswa kutazama mara mbili hayo aliyoongoza NEC kuamua kwani hata (hao watatu) wakipotezwa bado laana itaendelea kuwepo.

  MY TAKE:

  Ilipaswa wote wajiuzulu kuanzia mkuu wa nchi ambapo makamu wake ashike hatamu...NDIPO SALAMA ITAKUWEPO.

  Mola hawezi kuwaacha viumbe wake waliokuwa pamoja na sasa wanadhulumiana ilhali walisaidiana wakiwa ni 'boyz 2 men', kwa sasa kuwatupa tena kwa kashfa nzito shauri ya fahari hizi fupi za dunia ni uonevu na kukithiri kwa kupokea majungu toka kwa wapambe,, HAPANA;JK ANAPASWA AJITAZAME NA ATAZAME HATMA YAKE IKOJE, atakuwa hatarini abadan.
   
 19. k

  kush afrika New Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huu ni mwisho wa mafisadi na chama chao
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  chama kinapukutika........
   
Loading...