Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

Binafsi napata shida kuchangia hii thread kwasababu imekaa kama tetesi zaidi. Mwandishi anaelezea kupata habari kutoka kwa watu aliowaita makada wa ccm na hakuwahoji wausika hata m1.
All in all, ccm wapo katika wakati mgumu sana. Kuwatosa watu ambao wamekuwa wakikibeba chama kwa ufadhili na inteligesia ni kazi kubwa! Binafsi naona ni faida kwa upinzani maana kama hii ni kweli, wataanza kuumbuana na hapo watarahisisha vita ya ufisadi.
 
Hapo ni patamu, na nadhani ni uoga wa maamuzi ndani ya chama, lakini mimi sioni kama kuna ubaya kwani hawavuliwi uanachama bali wanavuliwa Ujumbe wa NEC hivyo bado watabakia kuwa wanaccm, tena ningewaomba wao ndio wakajipange kwa ajili ya kukisafisha chama chao. Kwani ukiwa nje ya nec unapungukiwa na nini? Ubunge mtabaki nao, Vijisenti mtabakinavyo, na heshima mtaani mtabaki nayo, nini shida? Achieni ngazi ili nawengine washika nafasi.


Wakuu picha ndio kwanza linaanza.


Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto
• Wasubiri barua zao kujibu mapigo, CCM yawaita Mapacha Watatu

na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijipanga kuwaandikia barua makada wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga) na Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), makada hao wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili watoe kile waliochokiita maamuzi mazito dhidi ya CCM, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.
Makada hao maarufu kwa jina la Mapacha Watatu, wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili wavunje ukimya na kueleza upande wa pili wa shilingi kwa madai kuwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), hakukuwa na azimio lolote lililopitishwa la kuwataka wapewe siku 90 za kujiengua na pia hakukuwa na azimio la kuandikiwa barua.
Mmoja wa makada hao, aliliambia Tanzania Daima Jumatano mjini Dodoma kuwa Rais Jakaya Kikwete na chama chake wamefanya jambo la hatari dhidi yao pengine kwa kujua au kutokujua lakini lazima wajibu mapigo ili jamii ielewe.
"Sitaki kuzungumza sasa hivi na huo ndio msimamo wetu. Waswahili wanasema akutukanaye hakuchagulii tusi, tunaangalia, tunafuatilia kwa karibu mambo yote kuanzia ndani ya vikao hadi sasa kinachoendelea kwenye mikutano ya hadhara hakika ni udhalilishaji wa hali ya juu. Tusubiri barua, tutajua la kufanya," alisema kada huyo, mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi.
Aidha, baadhi ya watu wa karibu walidokeza kuwa kitu cha kwanza kinachotarajiwa kufanywa na makada hao mara tu baada ya kukabidhiwa barua zao, ni kurejesha kadi za CCM, hatua itakayofanya wapoteze majimbo yao ya uchaguzi, lakini watahakikisha lazima chama kithibitishe ufisadi wao.
Kada huyo hakutaka kuzungumza kwa undani jinsi walivyopokea maamuzi ya NEC na hatua inayoendelea kwenye mikutano ya hadhara inayohutubiwa na Katibu Mkuu, Willson Mkama, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa sekretarieti mpya ambao jana walitua mkoani Iringa.
Katika mikutano ya hadhara inayodaiwa kuwa ni ya kujitambulisha, Nape amekuwa akiwataja Mapacha Watatu: Lowassa, Rostam na Chenge kwamba wametakiwa kujiondoa kwenye ujumbe wa NEC ndani ya siku 90, vinginevyo watang'olewa kwa nguvu.
Nape ambaye hadi sasa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, alienda mbali kwa kusema watuhumiwa hao hivi karibuni wataandikiwa barua na kuorodhesha tuhuma zao; na kusisitiza azimio la NEC la kuwataka wang'oke vinginevyo wataenguliwa na chama.
Hata hivyo, katika hatua nyingine, azimio la kutoa siku 90 kwa watuhumiwa hao wa ufisadi limeibua vita ya kisiasa kati ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na makada hao.
Wadadisi wa mambo ya siasa, wanaona kuwa kilichotokea mjini Dodoma ni muendelezo wa minyukano ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015 na siku za baadaye pia kwani mkakati wa kujivua gamba, ulipangwa makhsusi kwa ajili ya kuwaengua wao wakati orodha ya mafisadi ndani ya chama hicho ni ndefu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe wa NEC wanaodaiwa kupanga kusuka mpango huo, umethibitisha pasipo shaka kwamba Rais Kikwete, aliendesha vikao kwa kupanga wajumbe kutoa hoja za kuwang'oa Chenge, Lowassa na Rostam.
Kiongozi mmoja wa siku nyingi wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano anasema hoja ya kutaka Kamati Kuu na sekretarieti nzima kujiuzulu, ililenga kuwatema Mapacha Watatu, ndani ya vikao hivyo vyenye nguvu kwa njia ambayo ingemuepusha Rais Kikwete katika lawama za moja kwa moja.
"Chama chenye maadili, falsafa, mwongozo na itikadi, hakiwezi kuwapigia kampeni watu wanaohusishwa na ufisadi kwamba wanafaa huku kikisema hakuna ushahidi, halafu baada ya kupata ubunge na wengine hata kuongoza kamati nyeti za Bunge, chama hichohicho kinawataka watoke kwa madai kuwa hawafai. Ushahidi wa sasa kwamba hawafai, wameupata wapi?" alihoji mjumbe mmoja wa NEC.
Wadadisi wa mambo ya siasa wanaohoji hatua hiyo, wanasema uongozi mpya wa CCM ulipaswa kujikita kueleza matarajio ya chama siku zijazo na mikakati ya kujiimarisha na kueleza maazimio mengine ya NEC.
"Nape na wenzake hapaswi kuendelea kumzungumzia Lowassa na wenzake; haya mambo wameyamaliza kwenye vikao. Wanapaswa kueleza matatizo ya msingi ya chama na taifa kwa ujumla, hasa utekelezaji wa Ilani ya CCM," alisema.
Anasema ingawa wanakubaliana kimsingi na hatua ambazo CCM inatakiwa kuzichukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wanashangazwa na hatua ya Nape kutangaza azimio ambalo si sehemu ya mambo yaliyojadiliwa na kukubalika ama kwa kura au kwa kauli moja na wajumbe wote.
Hatua ya Nape inafananishwa na matukio ya hivi karibuni hususan wakati John Chiligati akiwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi kwamba amepata kutaja mara kadhaa taarifa isiyo sahihi ya maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu tofauti na kile kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo.
Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kuilipa au kutoilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai Tanzania karibu shilingi bilioni 100.
Chiligati anatajwa pia kupata kutoa maazimio ya kupotosha wakati aliposoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.



h.sep3.gif
 
Tanzania Daima, gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, linaendelea kutumiwa na Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kujisafisha.

Ukiisoma kwa makini habari hii, inawabeza kina Nape kwa kuwataja hadharani mafisadi hawa na inajaribu kuwatetea kuwa eti NEC haikusema wafukuzwe.

Ni aibu kwa gazeti linalomilikiwa na mwenyekiti wa taifa wa chama pendwa cha CHADEMA kuendelea kutumika kila siku kuwasafisha mafisadi hawa na kuwa jukwaa lao la kutoa propaganda.

Je, tutafika kwa mwendo huu?
 
Inafika sehemu nashindwa kuelewa. Mara ya kwanza nilijua kuwa ccm wanafanya makusudi wanayoyafanya kumbe kichwani 0000 ziro. Sasa mmemsafisha mtu vizuri na kwenye kamati ya bunge ni kiongozi wa kamati nyeti. Alafu sasa mnamzingua Mzee Lowassa eti mnampa siku 90 kwa nini hamkufanya zengwe kama kawaida yenu mapema. Kama mlivyomfanyia Samwel Sitta wa nguvu mkamuweka Bi. Kiroboto ambaye sasa hivi anachanganya madesa tu bungeni. Yaani hata kama anatuhumiwa si vyema mkamdhalilisha kiasi hiki. Kwanza umemtangaza kwamba yeye ni safi, Pili mmemkabidhi kamati nyeti ndani ya bunge, Tatu mmevunja sekretariet mkamwondoa, nne huyo Manape manauyee anawazalilisha live, sas ndo nashangaa. Kwa nini hamkuwaaambia wafanye kimya kimya mpaka muwafanye hivyo mbele ya umati. Naanza kukumbuka statement moja kwenye History kuwa 'You are planting the root of your own destruction" Chiligati alikiri kuwa CCM inaambiwa ufisadi, EPA , sijui nini lakini haina ushahidi, sasa ngoja ushahidi ukitolewa na hao mapacha watatu watakapoonesha nani alichota mkwanja wa Kagoda, n.k. Japo ni sherehe ila nimjuavyo mzee Lowassa sasa hivi yuko anasema "nyie sawa tuuuu" "mtaona tuuu eheeeeeeee" kama mtoto aliyenyimwa bajia na wenzake na siku akipata na yeye bajia atalipiza kisasi ile mbaya' ngoja tuone.
 
Mambo baaaado!!!, fungukeni "mapacha watatu" tupate uhondo sie, tumeshategesha satelites tunasubiri kunasa mambo.
Mhh TZ!!! toka boyz 2 men mpaka mapacha watatu!!!!

Mamengazi hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo !
 
TAARIFA KUTOKA KWA MTU WA KARIBU NA EL

MAPACHA WATATU EL,AC NA RA ,WAMEKUWA WAKIFANYA VIKAO KWA SKYPE TOKEA TAMKO LA CHAMA LA KUTAKA WAACHIE NAFASI ZAO,MPASHAJI ANASEMA MAPACHA HAO WAMEKUWA WAKIFANYA ONLINE MEETING KILA SIKU KWA ZAIDI YA MASAA SABA KWA KUTUMIA SKYPE KWANI WAMEKUBALIANA WASIKAE PAMOJA KUTOKANA NA TISHIO LA KUWAUA AMBALO MMOJA WAO ALILINASA KUTOKA KWA SHUSHUSHU WAKE AMBAYE NI MMOJA WA VIONGOZI WA VIJANA WA CHAMA CHA MAGAMBA ALIYEWEKWA KWENYE MPANGO HUO NA CHAMA HICHO CHA MAGAMBA

MY TAKE;hawa mapacha wanajipanga kujibu mapigo na kuufutilia mbali utawala wa JK;;,UWEZO WANAO,SABABU WANAZO NA NGUVU WANAYO.

NGOMA INOGILE,VITA VYA PANZI KUNGURU TWALAAAA
 
Tanzania Daima, gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, linaendelea kutumiwa na Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kujisafisha.

Ukiisoma kwa makini habari hii, inawabeza kina Nape kwa kuwataja hadharani mafisadi hawa na inajaribu kuwatetea kuwa eti NEC haikusema wafukuzwe.

Ni aibu kwa gazeti linalomilikiwa na mwenyekiti wa taifa wa chama pendwa cha CHADEMA kuendelea kutumika kila siku kuwasafisha mafisadi hawa na kuwa jukwaa lao la kutoa propaganda.

Je, tutafika kwa mwendo huu?

Gazeti si la chadema, gazeti linamilikiwa na m/kiti wa chadema. Kama duka la Mbowe la vipodozi la mbowe likiuza kipodozi ambacho ni expired utasema CDM ndo wameuza hivyo vipodozi? Aliyendika kariport hali halisi iliyopo. Ina maana ningeazisha mimi hii thread usingechangia? Na wewe huoni kinachoendelea. Mbona TBC wote wanarusha habari za Kina nnape wanavyojitambulisha na vilevile upande mwingine wa wanaolianalia suala hili. Acha kukariri Kiongozi.Saa nyingine inabidi uwe objective. Mbona jana Slaa jana Aliiponda serikali ya ccm na kueleza falsafa ya CHADEMA kwenye TV station ambayo muda wote wa uchaguzi ilifanya kampeni ya ccm. i.e ch 10 na hapo unasemaje.
 
Ebwanaeeeeeeeeeeeeeeee.,,, Mweeeeeeeeeeeeeeeeeeee ngoja nishangae Kinyakyusaaaaaaaa, mwemwemwemwmemwmemwmemwmemwe.

Wawaue wengine lakini sio E.L
 
HAHAHAAAAAAAAAAAAAAA,KWELI NGOMA INOGILE PATAMU SANA

TULIENI WAACHENI WAJIMALIZE WAKATI WAO HUU,KAZI KWELI KWELI ,NIMESIKIA EL NA AC WAMECHUKUA KADI ZA NCCR MAFISADI,SIJAJUA RA KAMA NA YEYE ATAENDA NCCR AU ATAENDA CUF aka CCM b

CHAMA CHA MAGAMBA
 
JK AKAE MACHO HAWA JAMAA SIO MCHEO
RA,EL NA AC mmmh naona ni muziki mkubwa sana na nahisi hawa ndio ROLE MODE WA CHAMA CHA MAPINDUZI HASA KWA KARNE HII
 
CCM wasiwabambike mzigo wa lawama RA, EL na Chenge. Ni lazima watafute chanzo cha tatizo ni nini bila kuona uvivu wa kufikiri.
Kwa upande wangu naona tatizo kubwa lililowafikisha hapo walipo ni kuliacha azimio la Arusha na kuanzisha azimio la Zanzibar. Karibu viongozi wengi ndani ya CCM walitumia madaraka yao katika kufanya biashara na kujilimbikizia mali kitu ambacho ni mwiko katika azimio la Arusha.
Sasa kwanini lawama zote ziwaende hawa watu watatu na wala si kwa CCM yote?. CCM ilibariki viongozi kujishughulisha na biashara. Ni sawa na mtu umevaa nguo zako bila ya kubadilisha kwa muda wa mwezi mzima, leo unavua na kubadilisha shati tu lakini soksi, chupi, suruali ni zilezile. CCM yote ni chafu hivyo inatakiwa kuondoka madarakani.

Pamoja na kuwa CCM imeoza kwakuacha uadilifu nakuamua ku institutionalize rushwa na unethical practice za biashara lakini wapo ambao wali over do na hawa ushahidi umekuwepo hapa JF kila grand corruption walihusika na mbaya zaidi wanataka hadi kumiliki na power ili waendelee kutunyonya na ku dictate kila kitu as if wao tu ndo watanzania nchi hii. Acha tuanze nao hawa ambao ni main roots hao subsidiary roots na branches watakufa tu mzizi mkuu ukikatwa.
 
Back
Top Bottom