Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

Lowassa amwombe Slaa amsaidie vinginevyo imekula kwake...sahau Urais..umepewa nafasi ukawa mlafi...

Waambie cdm wakusaidie naona ndio waliobaki wanao kuhurumia at least..kwakuwa mmetoka wote kaskazini (home town of cdm hard core blind followers)
 
huyu anataka kutuharibia nchi isitawalike heheee kweli mwosha huoshwa
Lowassa ana haki za kimsingi kuendelea kubakia CCM la sivyo taratibu na katiba ya CCM izingatiwe ikiwemo ya kutolewa ushahidi kuwa ni fisadi.

If ccm hawana huo ushahidi LOWASSA et al tutaendelea kuwaunga mkono abakie CCM

Jaman CCM kwa nini mvunje Katiba yenu ili mpate kuwahukumu mapacha? (USHAHIDI NI MUHIMU KUWEKWA MEZANI)
 
Hurray wajina wangu EL! kama ni kweli hiyo ni haki yako mheshimiwa saana. Mafisadi si wewe tu ndani ya CCM. Wengine ni ma-nyangumi wakati wewe papa. Angalia mhishimiwa, isije ikawa wewe, RA na AC mmegeuzwa mbuzi wa kafara! Kwani mtoto wa panya hakosi mkia na mtoto wa nyoka ni nyoka. Ili mradi EL, RA na AC mmezaliwa na nyoka mtakuwa nyoka tu. Na baba yenu amesema wao wote ni nyoka. na ndio maana wanajivua magamba, kwani we kwisaona kuku anajivua magamba? Mbado!. Msikubali kutoka bakini huko huko ninyi ni watoto wa nyoka, kwingineko hakuna nyoka wa kujiunga nao.
 
Lowassa amwombe Slaa amsaidie vinginevyo imekula kwake...sahau Urais..umepewa nafasi ukawa mlafi...

Waambie cdm wakusaidie naona ndio waliobaki wanao kuhurumia at least..kwakuwa mmetoka wote kaskazini (home town of cdm hard core blind followers)

haiwezekani ahukumiwe Lowassa bila ushahidi. Lowassa hana qualities za urais hilo liko wazi ila kuna magamba kibao hayajaguswa akiwemo JK
Komaa Lowassa usikubali kuondoka kirahisi haiwezekani mule wote ushikwe wewe uchawi.

JK akitaka awasafishe mafisadi serikalini na siyo kwenye chama manake huko kila mjumbe ni mchafu
 
Mtu hukemea na hata kukejeli matumizi ya silaha hatari ya maandamano (ambayo ni silaha ya pekee kwa Nguvu ya Umma) pale tu ambapo wao wenyewe hawajafikwa na mambo mazito kama ambavyo tulivyofikwa hadi pomoni wananchi wa Tanzania.

Nadhani sasa japo kwa uchache wake watakuja kugundua maana na manufaa ya maandamano kama njia pekee ya muonewa kuweza kutumia kujieleza chukizo zako katika jamii.

haya sisi yetu macho hawa ndio waliokuwa wakisema maandamano ya chadema yana nia ya kuvunja amani sijui haya yana lengo gani? lowassa komaa baba fisadi huko peke yako
 
Eroo hii kiwerte iko nataka sumbua Laigwanani yetu.........kanyo?

Oumono sime nikate mtu.....

Hhaahahaaa....ngoma imepata wapigaji, nangoja kuona wachezaji
 
Raha tupu mbwa koko wanaumana.Lowasa sema nao hao mwanangu usikubali , komaa nao mpaka kieleweke.
 
haya sisi yetu macho hawa ndio waliokuwa wakisema maandamano ya chadema yana nia ya kuvunja amani sijui haya yana lengo gani? lowassa komaa baba fisadi huko peke yako

Intelijensia MPOOO... nyie mnaojiita wataalam wakuona mbali MPOO? upinzani ukitaka kudai haki ambazo zitawafaidi hata nyie na jamaa zenu mnadai taarifa za INTELIJENSIA zinaonyesha kutakuwa na fujo na uvunjifu wa AMANI
 
Mkuu hii habari umeichoropoa wapi, kwa kuwa hata EL mwenyewe hana taarifa za maandamano hayo.

Acha kujikweza.Umejuaje kuwa EL hana taarifa?Yaani kwa vijiposti viwili vitatu vya kutetea mafisadi ndio unataka kutuaminisha kuwa ushakuwa karibu nao beyond kupewa vijisenti vya kwenda internet cafe kutetea mafisadi?
 
Yasemekana alikuwa nataka kupitia mgongo wa CCM ili kujiosha, lakini ikashindikana, na sasa anaandaa kupitia kabila lake ili kuhutubia na kutoa dukuduku lake, na kupata huruma yao kwa yaliyotokea kule DODOMA. Bado hajakata tamaa. Anajiandaa ku mobilize wamasai na kanda nzima kumuunga mkono. Kwa habari zaidi, fuatilia baada ya muda kidogo.
Wamasai ni asilimia ngapi ya wana ccm wote? Au kwa vile uvccm haiwataki watu wa kaskazini?
 
RACHEL msisogeze mguu hata centimeter moja komaeni humo humo wafalme wangu na kama watakuleteeni barua za kigamba-gamba waambie waambatinishe na hard evidence... maana hiyo ramani ya mlungula lazima itachukuwa eneo lote la magogoni. EL pata loshorooo swafi hatishiwi mtu nyau.
 
Kama ni kweli ana taka kuandamana si vyema kumzuia kwa kuwa ni haki yake na tungependa wengine kupata mawazo yake kwa kuwa yeye ni mtuhumiwa tu pengine tungepata mwanga zaidi toka kwake.
 
Hizo habari cio Kweli tumewasiliana na vijana wetu rchuga wanasema hakuna ****** kaingia wocga tu akumulikae usiku?
 
Makamda na Wakuu wa JF;

Nyeti zilizofika katika dawati la Superman zinasema wale TRAINGLE TRIPPLETS aka PEMBETATU PACHA aka RACHEL inasemekana wakekataa kujibu barua walizopewa hivi karibuni zikiwataka wajieleze kwa nini wasifukuzwe uongozi na uanaachama wa Chama Cha Magamba CCM.

Nyeti zinasema kuwa EL amesema mwenye ushahidi dhidi yake na mwenye ushahidi wa nanin anpaswa kuondoka CCM kwa ufisadi aje nao na hivyo wote wamekataa katu katu kusema wala kujibu kitu.

Inasemekana kuwa ni kweli RACHEL wamekuwa na vikao vyao vya siri na mpaka sasa wamekutana mara mbili tangu watoke Dodoma kwenye vikao vya CC na NEC.

Nyeti zinasema kuwa mara baada ya Vikao vya CC. Mkuu wa Kaya alimwita EL kule Ikulu ndogo ya Chamwin Dodoma majira ya saa nane usiku na akamuuliza kuwa imekuwaje Makamu Mwenyekigoda wa Chama Cha Magamba Mh. PM akakutaja na wewe waziwazi kuwa ni FISADI na je tutafanikiwa mikakati yetu tuliyopanga huko nyuma? (NB: Hii ni Mikakati ya Boyz II Men ya EL kuwa Next pale Magogoni). Hata hivyo EL alimjibu Mkuu wa Kaya kuwa bado anatafakari kilichotokea ndani ya CC na kumwambia JK ampe muda na atarudi na jibu.

Inasemekana EL alikaa kama nusu saa na kisha akaondoka. Desk la Superman limehabarishwa kuwa EL alikwisha jua mpango wa JK wa kumtosa kwa kumzungunguka pasipo kuharibu urafiki wao. Hata hivyo hadi leo hii JK bado hajapewa jibu.

Pamoja na yote hayo RACHEL wamechukizwa zaidi na maneno ya Dogo Nape na Kada Chiligati na Mukama ambao wanaaendelea kuwapa siku 90 wajitoe au watoswe kwa kuwa eti wao ni MAFISADI.

Naye Mu-Iran RA inamesemakana kama anataka bora Jahazi sasa liingie maji na wote wazame. Yaani kama noma na iwe noma.

Kuna sana mengi yatakuja baada ya mapumziko ya Pasaka from 28th May 2011 ambacho kitakuwa na Mishindo Mkuu.

Peace and Love

Respect.

Superman.

QED
 
Imefikia patamu sasa ngoma inogile kuna wimbo unasema toka sitoki toka sitoki nimemsahau dogo aliyetoa hiyo singo. Lowassa tuko pamoja komaa humo humo ukitoka umeumia ndugu yangu kama kushuka mshuke wote.
 
TRAINGLE TRIPPLETS aka PEMBETATU PACHA aka RACHEL

aka CREAL
 
Kama Lowasa ameshagundua kuwa JK ana mpango wa kumtosa kwa kumzunguka na kama ni kweli JK ana mpango huo,basi ni mwanzo mzuri kwao wote JK na Lowasa na kwa Wadanganyika.Kama ulivyosema mkuu,tutaona na kusikia mengi tusiyoyatarajia katika siasa zetu katika kipindi kifupi kijacho
 
Back
Top Bottom