Lowassa ni zaidi ya Rais, Vivuko vyote kutoa huduma bure

Lowassa ni zaidi ya Rais, Vivuko vyote kutoa huduma bure

nilikuwa najibu aliyesema hakuna nchi isiyotoza nauli katika kivuko/pantoni.. .zipo nyingi Kenya ikiwa mojawapo.

Huko Kenya mnakotoa mifano kila siku utadhani maisha ni mazuri sana huko, yangekua mazuri wakenya wangekua wanakuja kutafuta kazi Tanzania? Vipi kuhusu mgomo wa walimu ambao wanagoma kila mwaka kwakutolipwa mishahara yao?
 
Nijuavyo mimi, hakutakuwa na gharama za kivuko, utalipia tu kiingilio cha getini.
 
wakati wote akiwa waziri mkuu na aada ya hapo vivuko vimekuwepo. Na nchi zte duniani vivuko vinalipiwa. Ni sawa na kusema kuwa maji ni hiaji la lazima kwa kila mtu na hivyo inapaswa yatolewe bure. Watu wanaopenda vya bur utawajua tu.

hapa umepotoka kidogo/usa vivuko kama hivi vipo vya bure pia
 

nawaza kwa sauti pamoja na majukumu mengine ya serikali ni pamoja na hilo suala la kuvuka kigamboni inapaswa kuwa huduma kwani wale watu wa kigamboni kukaa kwao kule isiwe kama adhabu kuna watu wanamaisha ya kawaida sana kulivusha gari kwa tsh 3000 ausubuhi na jioni ni kuwaumuza afterall pesa ya pale watu wanapiga tu
ifike mahali serikali zetu ziangalie namna ya kupunguza ugumu wa maisha kwa kupunguza baadhi ya kodi.tukiondoa mashangingi, wakuu wa wilaya wakuu wa mikoa ,balaza dogo la mawaziri nadhani tunaweza songa mbele
VIVA LOWASA VIVA
 
Mwambie Lowassa Na Daladala Tupande Bure Nazo Maana Nazo Ni Kama Daraja Kutoka Majumbani Kwetu Mpaka Ofisini......!!!

Daladala ziko kila route; hata hao wanaopanda kivuko bado wanahitaji kupanda tena daladala. Kinachogomba hapa ni kwamba baadhi ya wananchi wasiumizwe kwa kitu ambacho hawana hiari nacho; hawakuchagua kutenganishwa na bahari hivyo hili lisitumiwe kama sababu ya kuwaumiza. Kwa serikali inayojali hilo wala halina mjadala.
 
Hivi Daraja Linatumia Mafuta?Daraja Linatumia Mashine?Daraja Linaendeshwa Na Watu?

Wanachomaanisha watu ni kuwa pantoni kama ya Kigamboni ni sawa na daraja. Huwezi ukajihesabu kuwa upo safarini kutoka ng'ambo moja kwenda nyingine kama ilivyo Dar - Znz. Kumtoza mwenda kwa miguu ni ulofa wa serikali inayosamehe kodi badala ya kukusanya na kisha kuomba omba kodi za wananchi wa mataifa mengine.

Amka kutoka usingizi, saa ya ukombozi imefika.
 
Daladala ziko kila route; hata hao wanaopanda kivuko bado wanahitaji kupanda tena daladala. Kinachogomba hapa ni kwamba baadhi ya wananchi wasiumizwe kwa kitu ambacho hawana hiari nacho; hawakuchagua kutenganishwa na bahari hivyo hili lisitumiwe kama sababu ya kuwaumiza. Kwa serikali inayojali hilo wala halina mjadala.

mkuu ukitumia kigezo hicho hata wazanzibar nao wataomba kutoka dar had zenji waende bure kwani nao hawakuomba watenganishwe na bahari vilevile.....
 
LOWASSA ni zaidi ya Rais

Thinking yake nadhani ni kubwa sana. Huu ni ukweli usio pingika. Nawaza kwanini sikuwa wa kwanza kufikiria hili.

Kwanini watu wanavuka kigamboni?? Jibu lake Rahisi W anakwenda Kwenye makazi Yao. Kivuko ni kama Daraja. Serikali haina fedha kwa Sasa kuweka Daraja la zege badala yake imeweka Daraja litembealo..PANTONI.

Ni Viroja, vituko vipana sana kwamba mkawatoza watu fedha kuvuka Daraja. Ni jukumu la serikali kujenga na kuwezesha miundombinu na pitio. Kivuko ni daraja. Haiwezekani kuwatoza Nauli watumiaji wa Daraja.

LOWASSA sijui kaugunduaje ukweli Huu ambao hatukuugundua tokea awali. Serikali imawajibu wa kuwatumikia wananchi na sio kuwafanya mitaji.

Vivuko vyote nchini Lazima vitoe huduma kwa wananchi na sio mradi wa wachache.

Hata umeme ni huduma, maji pia, zahanati na elimu pia, hata kula chakula majumbani kwetu ni huduma, kila kitu ni huduma!Iam just expanding your thoughts, akili za bavicha hizi lazima!Mtaomba mpaka hela za kuchepukia mwaka huu
 
Wanachomaanisha watu ni kuwa pantoni kama ya Kigamboni ni sawa na daraja. Huwezi ukajihesabu kuwa upo safarini kutoka ng'ambo moja kwenda nyingine kama ilivyo Dar - Znz. Kumtoza mwenda kwa miguu ni ulofa wa serikali inayosamehe kodi badala ya kukusanya na kisha kuomba omba kodi za wananchi wa mataifa mengine.

Amka kutoka usingizi, saa ya ukombozi imefika.

Mkuu Tukubaliane Kitu Kimoja...Hivi Daraja Lina day To Day Expenses Like Kununua Mafuta,kutengeneza Engine Kama Pantoni?Hata Kama Ni Route Fupi Stil Kuna Expenses Na Ndizo Zinazolipwa Na Wananchi....
 
Kuwatoza watu kwenye kivuko ni sawa na adhabu, bora huyu baba ameliona! Mungu tusaidie tuweze kuifurahia nchi yetu
 
Wakati wote akiwa Waziri Mkuu na aada ya hapo vivuko vimekuwepo. Na nchi zte duniani vivuko vinalipiwa. Ni sawa na kusema kuwa Maji ni hiaji la lazima kwa kila mtu na hivyo inapaswa yatolewe bure. Watu wanaopenda vya bur utawajua tu.
Alikuwa waziri mkuu kwa muda gani..? Maana kabla hajaanza hata kazi vizuri mlimletea mizegwe nyie waswahili..?
 
mkuu ukitumia kigezo hicho hata wazanzibar nao wataomba kutoka dar had zenji waende bure kwani nao hawakuomba watenganishwe na bahari vilevile.....

Kwa suala la Kigamboni kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili, kama pangekuwa na daraja, ni mwendo wa dakika chache tu kwa miguu tofauti na Zanzibar. Kwa kuwa Serikali haitaki kujenga daraja pale (ambalo ni jukumu lake la msingi) basi ihudumie hizo pantoni na wananchi wavuke bure kabisa. Mshaurini jamaa a-copy na hii maana kwa kudesa hajambo.
 
Kuwatoza watu kwenye kivuko ni sawa na adhabu, bora huyu baba ameliona! Mungu tusaidie tuweze kuifurahia nchi yetu

Sio vivuko tu Mkuu. Hadi toilets siku hizi watu wanapiga hela (ubinafsishaji) hadi unajiuliza kazi za manispaa ni zipi? Sawa watu binafsi wanaotaka kujenga vyoo kwa minajili ya kufanya biashara wafanye hivyo lakini kwenye maeneo muhimu kama stendi, vituo vya daladala lazima huduma hizi ziwepo tena bure na kwa gharama za serikali. Yaani nchi hii ukibanwa na tumbo la kuharisha ghafla kama huna hela imekula kwako tofauti na enzi za Mwalimu huduma zilikuwa bure kabisa. Vivyo hivyo viingilio stendi kuu za mabasi, n.k.
 
Kwa suala la Kigamboni kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili, kama pangekuwa na daraja, ni mwendo wa dakika chache tu kwa miguu tofauti na Zanzibar. Kwa kuwa Serikali haitaki kujenga daraja pale (ambalo ni jukumu lake la msingi) basi ihudumie hizo pantoni na wananchi wavuke bure kabisa. Mshaurini jamaa a-copy na hii maana kwa kudesa hajambo.

Mkuu Hilo Daraja Halijajengwa Bado So Must Kuingia Gharama Kwa Wananchi....
 
Back
Top Bottom