LOWASSA ni tishio

Ukisema Mufti Mkuu ni tishio sitakuewa. Ukisema Mufti Mkuu ni tishio kwa amani ya Watanzania ndipo nitakapoelewa. Sasa Lowassa ni tishio kwa vipi?
 
Huku ni kuhamisha attention ya wachangiaji na huu ni mpango mahususi wa mafisadi. Mufti ameingiaje humu? Tanzania hii public enemy number 1 ni LOWASSA!
 

...Za kwako za Kweli zi Wapi?

 

...EEEeeeh??? Kumbe ameishalinunua na Tanzania Daima??? Nilidhani alikuwa amenunua baadhi ya waandishi tu kama yule Mzee wa ukurasa wa kati wa toleo la Jumatano ambaye hawezi kuandika makala bila kusifia utendaji kazi mzuri wa Lowassa! Katabazi? Mullinda? Whew!
How Sad. There goes one of my very few favorite newspapers....!
:noidea:
 

Acha kuwa Mjinga.
 
Ni kweli Lowassa ni tishio particularly kwa UFISADI. No question about that.
 
Lowassa atawahonga mpaka dakika ya mwisho jina lake litaenda Kamati Kuu.. Majina matano (5) hatopita. Watamchuja Central Committee. Majina matatu yataenda NEC Lowassa, KWAO.. Ubaya kawanunua na TISS kwahiyo mmh! SIjui itakuwaje..
 

Najiuliza kwa nini iwe hivyo kwa mtu ambaye amejiuzuru kwa fedheha kiasi hicho! mtu ambaye amekuwa madarakani siku nyingi bila mafanikio kwa nchi tunayoweza kuyakumbuka.

Wale muliouliza ufisadi wake;
1. Hebu tuachane na matendo yake pale AICC
2. Alianza na pesa ya mafuriko ya Tanga.
3. Baadaye akauza viwanja vya mnazi mmoja.
4. Baadaye anasifika kwa Richmond na dowans.
5. Wizara ya maji pia hakupita hivi hivi maana nasikia kila mwezi akaunti yake ilinona kwa kipato toka kwa kila injinia wa maji wa mkoa.
6. Hapo Arusha vipi vioski vya stationery vinavyolazimisha kila mkutano ununue kwake?
7. Hapo Dar kwa wenye mahoteli vipi vurugu za kulazimishwa kupeleka mashuka kwenye laundry zake? Nasikia musipofanya hivyo TRA wanawazonga.

Lazima kama hizo kwa sasa, je, vipi akipewa U-rais itakuwaje? Mbona tutalawitiwa kwa nguvu!


Hitimisho dogo kwangu kwamba anaweza kuwa tishio kwa CCM lakini siyo kwa wa-Tz wote na hasa walio timamu. Tatizo ni mpangilio wa CCM na kamati zake. Hebu angalia viwango vya ufahamu vya wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Ni ndogo kiasi kwamba bado mtu kama Kingunge ndo thinkers wao. Enzi hizi za dot com. Engine ya chama huanzia kwa katibu wake, vipi huyo katibu wa CCM? Vijana wanasema kama ni moto, kuni mbichi. Hauwaki hata siku moja.

Sasa waangalie vijana wa CCM. Nani wa kutumainiwa kwa ufahamu wa mambo ya nchi na Dunia? Hao ni vijana wa wakati ambao nchi ina vijana zaidi ya laki moja ktk vyuo vya elimu ya juu. Enzi za mkongo wa mawasiliano ili kila mtu aione dunia nyumbani kwake. Kwa nini hakuna kijana mwelevu huko UVCCM?

Ukisha iona structure kama hiyo huyu mtu hawezi kutoa bilioni mbili wakagoma kutoa support.

Ni Tishio lao huko huko CCM.
 
Mimi nauliza Lowasa tishio kwa nani?? Watanzania awamtaki kabisa kama atajaribu mwaka 2015 basi ajipendi kwa sababu atamalizika na kama atapita kama anavyo jimarisha basi nchi hii ya TANZANIA itauzwa na WaTanzania ndani ya nchi yao. Kweli kama anataka uraisi mwaka 2015 then arudishe mali zote alipata kwa ufisadi na wizi kwa WaTanzania bila kusita. Alafu akiri kwa dhati kua yeye ni fisadi na kuunda hiyo kampuni ya RICHMOND na wote wanaosika.

Kwanza huyo mIran Rostam dawa yake iko jikoni. Anatujafua nchi yetu nakujidai yeye ni Mafia sisi ni zaidi. AJARIBU ataiona. Pesa za WaTanzania ameiba inamtia kiwewe kwa na dharao na kiburi asubiri tuu. Tunajua sana kwa ameweka wavijana wa CLOUDS FM kama kanyaboy tunasubiri. Heri yako Rostam umezoea ----
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa....ni njaa yakusumbua au hauna akili timamu.
huyu jamaa anaweza kuwa tishio kwako pekee
 
Mkuu vipi tena mbona unaingia kimugongo mugongo huku ukitaja majina hovyo hovyo? Mbona unaleta maajabu ya sisimizi kumeza dafu?
Kuhusu Lowassa kwangu ni kama malaria..... haikubaliki
 
nawaonea huruma kambi ya rowasa sababu hata adui yenu hamumfahamu poleni sana! najua mnalipwa pesa nyingi ila mjue adui yenu mkubwa yumo ndani ya ccm VILAZA NINYI!

Very true! Lowassa na wenzie watamalizana na siasa za Ki-kaskazini na siasa za Pwani na sio upinzani.
 
Yaani lowasa akiwa rais wa tz, nadhani ategemee katiba ya sasa mchakachuo wanaotaka leta katiba mpya 2014, vinginevyo no
 
Duuu
Hii sokuijua kabisaaa

 
Hivi ni lini Watanzania tutakuwa serious..???hivi unaweza kusimama mbela ya jukwaa na kumtetea Lowasa?????????

Hebu tuwekee jamvini ubaya wake ukilinganisha na wana ccm wengine. Maana kabla ya Mambo ya Dowans kila mtu alikuwa anamsifia sasa kwakuwa nimi ni adui mkubwa wa watu wanafiki hebu tuambie ubaya wake ukiachiria mbali huu wa Dowans ambao serikali yote ilihusika.
 

Ndiyo maana nikasema hakuna mwenye hoja ya maana ya kumshitaki Lowasa!! Huu ulioandika hapa ni UZUSHI MKUBWA. kwa mfano hakuna asiyejua kuwa aliyeuza viwanja vya Mnazi mmoja miaka ya 1993 ni Rais Mwinyi hii hata taahira anajua, Lowasa kipindi hicho aliingia kwenye mgogoro mkubwa na mzee mwinyi kupinga uuzaji wa viwanja hivyo ambapo alitoa masaa kadhaa kwa manispaa ya ilala iwe imeondoa uzio wa mabati uliokuwa umewekwa hapo. baada ya muda kupita bila manispaa kuondoa wananchi walienda wenyewe kuyaondoa kitu kilichompa heshima kubwa Lowasa leo hii unatuambia Lowasa ndiye aliyeuza viwanja? HUU NI UONGO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…