Kivuli cha Madaraka: Unapokuwa Tishio Bila Kukusudia

Kivuli cha Madaraka: Unapokuwa Tishio Bila Kukusudia

Chura

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,425
Reaction score
2,528
Katika korido za mamlaka, kuna msemo mmoja wa kishushushu unaosema: "Ukaribu na jua unakupa joto, lakini unavyozidi sana kulikaribia jua unajiweka katika hatari ya kuteketea"Hii si kauli ya mzaha; ni onyo la kiintelijensia kuhusu jinsi ukaribu na mamlaka unavyoweza kugeuka kuwa mtego wa mauti.

Hatari ya kwanza: Kulewa "Harufu" ya Mamlaka​

Yote huanza taratibu. Mtu anateuliwa kuwa mshauri, msaidizi, au mshirika wa karibu wa mkuu wa nchi. Kwa sababu yeye ndiye anayekaa na mkuu saa nyingi, anaanza kujiona kama "mdomo" na "masikio" ya mkuu,kila favour atataka impitie yeye ikiwemo kujilimbikizia vyeo ambavyo kimsingi havina hata sababu ya yeye kuwa navyo.
Hapa ndipo dhana ya "Power Proximity" inapoanza kufanya kazi. Anaanza kutoa amri. Anaanza kusema, "Mkuu amesema hivi," au "Mkuu hapendi hiki." Hata kama Mkuu hajatamka neno hilo, watu wanatii kwa sababu wanaogopa ukaribu wake na mamlaka. Bila kujua, anaanza kujiongezea madaraka ambayo hayapo kwenye katiba wala sheria. Anakuwa "Mkuu Kivuli."

Hatari ya Pili: Mtego wa kuwa hatari bila kutarajia "Threat by Default"​

Hapa ndo pamoto zaidi. Maana ya kuwa "Threat by Default" (Tishio kwa Msingi) ni kwamba mfumo wa usalama na utulivu wa nchi unaanza kukuona kama adui, hata kama wewe binafsi unajiona ni mtiifu. Kwa nini?

Kwanza, unaharibu Chain of Command. Maafisa na watendaji wa jamhuri wanashindwa kufanya kazi zao kwa sababu wanaogopa kuingiliwa na wewe. Pili, unakuwa "Gatekeeper." Unaanza kuzuia taarifa za kweli zisimfikie mkuu, na badala yake unampa kile unachotaka asikie. Mkuu anaanza kuishi kwenye "bubble" (ulimwengu wa kufikirika) wewe ndo unakua unaamua mkuu asikie ni na kipi mkuu mkuu asisikie.

unakua hatarisho la usalama kwa sababu zifuatazo
  • Parallel Power Center: Unajenga kituo cha pili cha madaraka ndani ya kaya. Hii inaharibu mfumo wa amri (Chain of Command).

  • Target of Envy and Sabotage: Kwa sababu una nguvu nyingi zisizo rasmi, maadui wa mkuu wataanza kukutumia wewe kumshambulia mkuu au kukushambulia wewe ili kumdhoofisha na kumkomoa mkuu.

  • Information Monopoly: Ikiwa wewe ndiye pekee unayeamua mkuu asikie nini, Rais anaanza kuishi kwenye "bubble." Hili ni tishio kwa sababu mkuu anaweza kufanya maamuzi mabaya kulingana na taarifa za upande mmoja.

Hatari ya Tatu: Mgongano na Mfumo​

Ikumbukwe mfumo wa serikali na intelijensia umeumbwa kulinda Taasisi, si mtu mmoja mmoja. Mtu anapokuwa na nguvu kuliko cheo chake, anaanza kuonekana kama "kirusi."

Maadui wa serikali na maadui wa mkuu wanaanza kumtumia kama mlango wa kuingilia kumdhohofisha mkuu, na watiifu wa mifumo wanaanza kukuchukia kwa sababu unazuia haki zao. Siku Mkuu atakapohisi kuwa huyu mtu ana nguvu ya kumshinda yeye, au siku mfumo wa utakapoamua kuwa huyu mtu anahatarisha utulivu, "kivuli" hicho hufutwa haraka sana.

Nimalize kwa kutoa rai na onyo la unyenyekevu: Madaraka ya kuazima yasikufanye ujione mwenye mamlaka kamili. Unapokuwa karibu na mtoa maamuzi, nguvu unayotumia si yako ni ya ofisi. Ukianza kuigeuza kuwa mali yako binafsi, unajitengenezea uadui na mfumo mzima.

Mwisho wa siku, hakuna mtu aliye mkubwa kuliko mfumo unaomlinda. Na ukiwa tishio kwa msingi (by default), ipo siku mfumo utataka kujirekebisha ili kurudisha usawa, na mchakato huo mara nyingi huwa hauna mazungumzo wala huruma

Mwenye macho na asome na mwenye ubongo aelewe.
 
Na hasa Rais akiwa Form four failure,ngoma hapo ndiyo huwa mbaya zaidi .
 
Atakuja kujibu yeye mwenyewe kwa mafumbo kama ulivyo fanya wewe. Use kwenye mada hii au atakayo ianzisha yeye mwenyewe.

JF FOREVER
 
Back
Top Bottom