Lowassa ni kama Jacob Zuma?

Time will tell. Hakuna lisilowezekana chini ya Jua! Nani mkamilifu? Hii ni hoja itakayotolewa baadaye na wahafidhina ndani ya CCM. Na hii hoja ndiyo itaondoa utando mwekundu kwa EL na kuwa mweupe kama theluji!!!! Lets wait and see!! Labda mwenyewe asema sasa siasa basi? Watanzania wanasahau mapema sana!!! na hata hivyo kwa waliosoma ripoti ya Mwakyembe EL hakutajwa kuchukua senti na hii ripoti ipo. Tatizo hapa ni media jinsi ilivyotumika. Sitta mwenyewe alikwenda Monduli na kumsifia ambayo ni ishara ya kumsafisha. Na kwa staili yake ya kutulia kimya atakuwa better off kuliko waropokaji wengi. Anything is possible!!!! Lakini kabla ya hapo tunahitaji katiba mpya itakayompunguzia rais madaraka!!!
 
Kamwe Lowassa hawezi kuwa kama Zuma kwa sababu nyingi tu na chache kati ya hizo ni hiziz:

1. Hana support yoyote toka kwa wafanyakazi wa nchi hii ambao kwa SA ndiy walikuwa instrumental katika kumnyanyua Zuma;

2. Zuma alikuwa na eloquence ya hali ya juu na alishuka mpaka kwa watu wa kawaida na vijana ambao ndiy walikuwa chachu ya ushindi wake. By the way huyu wa kwetu hapa amewahi hata kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, Sauti ya Ujerumani au hata VOA? kwa lugha gani?;

3. Mbeki alionekana kama mtu ambaye anajali maslahi ya matajiri na watu weupe na kuwaacha watu weusi na wala wa kima cha chini (kwa hapa kwetu sifa hizi za Mbeki ndizo za Lowassa);

4. Zuma alikuwa na constituency, kwa maana ya kwamba alikuwa ni 'undisputed king' wa wazulu na hao walimpa boost kubwa hasa kwa vile ndilo kabila kubwa kuliko yote. Huyu bwana hapa kwetu hata hao wamasai wenyewe wamem-disown wakidai ni mmeru na hata wangemuunga mkono, hawatoshi kumpa jeuri.

5. Kwa ujumla uungwaji mkono wa huyu bwana umebaki kwa wenye njaa wachache wanaoingia kwenye vikao vya chama na wengine sasa wameanza kumgundua na kuchoshwa na hila zake za hujuma na kiu yake ya kuutaka urais.

Mkuu Ndutu hapa umeongea yote nakuunga mkono sana hapa
 
usim underestimate lowassa. ana nguvu sana ndani ya ccm na nina hakika atateuliwa na chama. tatizo lake ana maadui wengi ndani ya chama hivyo watahakikisha hashindi. akiwa mjanja asigombee

huyu jamaa ni stratergist hatari sana...na ni mstahimilivu na ana ngozi ngumu sana kuhimili michubuko...nina imani kabisa huyu anapitishwa na CCM kuwania urais 2015....
 
Kamwe Lowassa hawezi kuwa kama Zuma kwa sababu nyingi tu na chache kati ya hizo ni hiziz:

1. Hana support yoyote toka kwa wafanyakazi wa nchi hii ambao kwa SA ndiy walikuwa instrumental katika kumnyanyua Zuma;

2. Zuma alikuwa na eloquence ya hali ya juu na alishuka mpaka kwa watu wa kawaida na vijana ambao ndiy walikuwa chachu ya ushindi wake. By the way huyu wa kwetu hapa amewahi hata kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, Sauti ya Ujerumani au hata VOA? kwa lugha gani?;

3. Mbeki alionekana kama mtu ambaye anajali maslahi ya matajiri na watu weupe na kuwaacha watu weusi na wala wa kima cha chini (kwa hapa kwetu sifa hizi za Mbeki ndizo za Lowassa);

4. Zuma alikuwa na constituency, kwa maana ya kwamba alikuwa ni 'undisputed king' wa wazulu na hao walimpa boost kubwa hasa kwa vile ndilo kabila kubwa kuliko yote. Huyu bwana hapa kwetu hata hao wamasai wenyewe wamem-disown wakidai ni mmeru na hata wangemuunga mkono, hawatoshi kumpa jeuri.

5. Kwa ujumla uungwaji mkono wa huyu bwana umebaki kwa wenye njaa wachache wanaoingia kwenye vikao vya chama na wengine sasa wameanza kumgundua na kuchoshwa na hila zake za hujuma na kiu yake ya kuutaka urais.

wewe humjui Lowassa kaa kimya..Atawaacha watu vinywa wazi...Muulize sitta aliambiwa nini na kikatokea nini..The guy is very powerful for you rinformation ZUma chamtoto tu...Wait utakuja kuniambia
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo
Kuna teja 1 pale mza, makoroboi. Bila shaka huyo ndo unayemfananisha na ndg. Lowassa eti.
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo

unamfundisha?
 
Wana JF, katika kipindi kifupi ambacho mh, Edward Lowasa aliongoza serikali maendeleo yaliweza kuonekana. Nitaje mambo machache ambayo ni miale ya maendeleo iliyooneshwa na huyu kiongozi shupavu: 1. Kila kata kujenga shule ya sekondari.2. Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kupata kozi ya muda mfupi ili kuongeza idadi ya walimu na kupunguza upungufu.3. Kila kata kuwa na kituo cha afya.4. Kuukataa mkataba usio na maslah wa mamlaka ya maji safi na maji taka DSM.5. Kufuta ada ya kudahiri watoto wanaoingia darasa la kwanza hivyo kuongeza idadi ya wanaoingia darasa la I.Ama kwa hakika tulikuwa bado tunamuhitaji na kama angeendelea kuwepo madarakani huenda sasa kila mkoa ungekuwa angalau na VETA kama siyo chuo kikuu.
 
....na kungekuwa na Richmond katika kila sekta.
 
bora kipindi cha Lowassa maofisa wa serikali waliogopa kufanya wizara/mashirika mali zao binafsi
Yes Lowassa ni FISADI ila PINDA ni mvivu wa kufikiri,ku act, hajui madaraka yake,analialia,anajipendekeza kwa kanisa, mwoga wakati dola yake, hafai kuwa hata mwenyekiti wa mtaa.
 
Lakini naye Lowasa Ni mwoga kujitetea. Toka abebeshwe zigo La ufisadi hajaeleza Watanganyika wenzake kuwa kinachesemwa kuhusu ufisadi nani muhusika mkuu. Yeye si Yesu kujitoa kafara kwa wenye dhambi. Asimame kama shujaa aseme anahusikaje katika kuihujumu Tanganyika Au La! Ndiyo tumjaji yeye Ni bora Au La.
 
Mchapa kazi, authoritative. Tumefanikiwa kufahamu kuwa ni mchafu kati ya wachafu wengi na wakuu aliowaacha serikalini. Namkubali kwa kazi na leadership authority. Thanks
 
Hapa unazungumzia watu wawili tofauti!.MWIZI ambaye ni lowassa na Mpenda vimada ambaye ni zuma in which lowasso can also be there ila mambo yake ya uhuni hayasikika.Lowassa angekuwa a good P aspirant ila ilo doa la TAMAA YA KUJILIMBIKIZIA MALI ZA WANANCHI KWA WIZI KAMA FISI MWENYE NJAA ALIYEONA NYAMA.Mungu tuepushe na Lowassa
 
Lakini naye Lowasa Ni mwoga kujitetea. Toka abebeshwe zigo La ufisadi hajaeleza Watanganyika wenzake kuwa kinachesemwa kuhusu ufisadi nani muhusika mkuu. Yeye si Yesu kujitoa kafara kwa wenye dhambi. Asimame kama shujaa aseme anahusikaje katika kuihujumu Tanganyika Au La! Ndiyo tumjaji yeye Ni bora Au La.
Umesahau kuwa alipotoka Dodoma alienda TBC ili auleze uma wa wa Tz namna bunge lilivyodanganywa na likafanya maamuzi oin favour of wenye uchu wa madaraka na si maendeleo ya nchi TV prog ikabadilishwa?. Nataka ujue kuwa anazibwamdomo kwa nguvu nyngi.
 
Lowassa awe Rais wa nchi ipi hiyo?Akipitishwa na CCM itabidi wapinzani waandae kabisa Wagombea kwa kushirikiana na mwanzo mpya utakuwa umefika Tanzania kwani watashinda kwa kishindo cha Tsunami
 
mkuu umesahau RICHMOND na Bulyankuru.
Naona unachanganya mada kwa kutoelewa au unafanya makusudi kumbebesha Lowasa tuhuma zisizo mhusu: 1: Wakati Richmond inapokelewa na kupewa mikataba Lowasa hakuwa anahusika kwa aina yoyote ile: hakuwa waziri mkuu wala waziri wa nishati- nieleze anahusikaje na Richmond.2 wakati wa scandal ya bulyanhulu hakuwa muhusika pia. 3. Kumbuka kuwa kamati ya mwakyembe haikumuhoji na ilitoka na maamuzi bila kuzingatia ushauri alioutoa wakati akiwa madarakani. Kwa kifupi tuhuma za watu dhidi ya Lowasa ni za kutunga kwa malengo ya kisiasa.
 
Lowasa na Zuma wanafanana kwa kuwa wote ni wahanga wa siasa za chuki na fitna. Wanafanana pia kwa kuwa naye atashinda kama zuma alivyoshinda kesi za kubambikiwa na kisha kushika hatamu upya ya kuongoza chama chake.
Hapa unazungumzia watu wawili tofauti!.MWIZI ambaye ni lowassa na Mpenda vimada ambaye ni zuma in which lowasso can also be there ila mambo yake ya uhuni hayasikika.Lowassa angekuwa a good P aspirant ila ilo doa la TAMAA YA KUJILIMBIKIZIA MALI ZA WANANCHI KWA WIZI KAMA FISI MWENYE NJAA ALIYEONA NYAMA.Mungu tuepushe na Lowassa
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo

Kaza buti sana - jamaa ana mhuri mgongoni ambao kuufuta inabidi usuguliwe hadi ngozi inyofoke. Pengine Symbion watakuwa wamesaidia kujaribu kuufuta - maana kelele za kukumbushia ya kale watakuwa wamesaidia kuzizima. Hongera Symbion!!!
 
Hapana Lowasa sio kama Zuma, Zuma baada ya kuondolewa umakamu wa rais kwa tuhuma za rushwa kesi ilienda mahakamani na akashinda kitu ambacho kwa Lowasa hakijafanyika bado, Zuma alikuwa ni m/kiti wa taifa wa ANC wakati Lowasa sio m/kiti hata wa mtaa wa CCM. Zuma alikuwa na nguvu ndani ya ANC kama m/kiti na mtu mwenye maono, Lowasa nguvu yake CCM ni kwa sababu ya Pesa.

Kwa hiyo kumfananisha Zuma na Lowasa ni kukosa hoja kama unampenda Lowasa usimlinganishe na wanamapinduzi kama kina Zuma, mlinganishe na watu kama kina Gordon Brown wa England ambaye alivyokuwa waziri wa fedha alifanya vizuri lakini alipopata uwaziri mkuu hadi chama chake kikapoteza mvuto, na Lowasa ni hivyo hivyo alivyokuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo ilikuwa nafuu lakini alipoukwaa uwaziri mkuu richmond ikampotea mvuto hadi akaona uwaziri mkuu ni mzigo akaamua kuutua.
 
Back
Top Bottom