Lowassa ni kama Jacob Zuma?

kamwe lowassa hawezi kuwa kama zuma kwa sababu nyingi tu na chache kati ya hizo ni hiziz:

1. Hana support yoyote toka kwa wafanyakazi wa nchi hii ambao kwa sa ndiy walikuwa instrumental katika kumnyanyua zuma;

2. Zuma alikuwa na eloquence ya hali ya juu na alishuka mpaka kwa watu wa kawaida na vijana ambao ndiy walikuwa chachu ya ushindi wake. By the way huyu wa kwetu hapa amewahi hata kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa kama bbc, sauti ya ujerumani au hata voa? Kwa lugha gani?;

3. Mbeki alionekana kama mtu ambaye anajali maslahi ya matajiri na watu weupe na kuwaacha watu weusi na wala wa kima cha chini (kwa hapa kwetu sifa hizi za mbeki ndizo za lowassa);

4. Zuma alikuwa na constituency, kwa maana ya kwamba alikuwa ni 'undisputed king' wa wazulu na hao walimpa boost kubwa hasa kwa vile ndilo kabila kubwa kuliko yote. Huyu bwana hapa kwetu hata hao wamasai wenyewe wamem-disown wakidai ni mmeru na hata wangemuunga mkono, hawatoshi kumpa jeuri.

5. Kwa ujumla uungwaji mkono wa huyu bwana umebaki kwa wenye njaa wachache wanaoingia kwenye vikao vya chama na wengine sasa wameanza kumgundua na kuchoshwa na hila zake za hujuma na kiu yake ya kuutaka urais.

umefanya analysis nzuri sana ila umesahau sana kuwa enl alishaifanyia kazi hili tena vizuri sana kwani ukae ukijua anafahamu sana zengwe alofanyiwa malecela na pia jamii inatambua mchezo mzima alofanyiwa mpaka kuuondoa u pm, wewe na mimi na watz kibao bado tunakumbuka kauli ya naibu waziri wa ujenzi akiwa mbunge by then kuwa wali withheld some info for the sake of urt......, hajasema na sasa ni naibu waziri, je nin nani mwenye ujasiri wa ku expose hayo, mind u ile kamati wabunge wote wamerudi except mzee shelukindo......, angalizo langu kwako...ni mapema na makosa kumhukumu enl na pia si haki kumhukumu mtu unjustly kwa sababu tu fulani anasema huyu yuko hivi.....,

ccm ina namna zake za kujiendesha acha tusubiri kama watapitia mkondo wa anc au la...., pengine niseme tu uvccm ya sasa haina type ya mtu kama julius wa anc youth charter...., hawa wa kwetu hawasomeki, wakisomeka wana sura ya utumwa...which is more than danger...

Kidumu chama cha mapinduzi
 
Naona unachanganya mada kwa kutoelewa au unafanya makusudi kumbebesha Lowasa tuhuma zisizo mhusu: 1: Wakati Richmond inapokelewa na kupewa mikataba Lowasa hakuwa anahusika kwa aina yoyote ile: hakuwa waziri mkuu wala waziri wa nishati- nieleze anahusikaje na Richmond.2 wakati wa scandal ya bulyanhulu hakuwa muhusika pia. 3. Kumbuka kuwa kamati ya mwakyembe haikumuhoji na ilitoka na maamuzi bila kuzingatia ushauri alioutoa wakati akiwa madarakani. Kwa kifupi tuhuma za watu dhidi ya Lowasa ni za kutunga kwa malengo ya kisiasa.
Kama yote hayo alisingiziwa ilikuwaje akajiuzulu?
 
King... naona ametumwa na Lowasa,
-kumfananisha Zuma na Lowasa ni sawa na kufananisha au kusema moto ni sawa na maji,vitu ambavyo havilingani.
-Kifupi ni kuwa sisi siyo wadanganyika,kama ana jeuri achukue fomu ya kugombea urais aone kitakachotokea.na ole wao CCM watakakaompitisha utakuwa ndiyo mwisho wa CCM duniani siyo TZ pekee.
-Soma alama za nyakati,au fikiri kidogo yaliyotokea Kenya,Zambia,Malawi na kwingineko ili ujue kuwa wananchi wakikuchoka wamechoka kabisa.
-Nchi hii haiwezi kuongozwa na mtu jeuri,mwenye kiburi,mwenye kutafuta sifa juu ya vichwa vya watu,kupanda ngazi kwa kuangamiza wengine,kuharibia watu maisha,mbinafsi,mkabila,fisadi,mwenye majivuno,anaetenganisha hadi ndugu zake,Mnazi mwenye kila aina ya uchafu haikubaliki.
-Namjulisha mwanzilishi wa hii thread kuwa Tanzania siyo Lowasa tu,au CCM siyo ya Lowasa kuna wengi wenye uwezo mkubwa kuongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa mara 100,000 zaidi ya Lowasa na hata aliyeko madarakani hivi sasa lakini hawataki kujitokeza kuogopa kuhujumiwa na hao kina wapenda uongozi.
-Hivi watu wakikuchoka na wewe ukaendelea kujipendekeza kwao kwa kutaka uwaongoze unategemea ni nini kitafuata,jibu sina ila angalia yanayotokea Libya utapata jibu zuri.
-Kwa ufupi mjulishe kuwa hana tena mvuto kwa wa TZ kama ni dawa ilishachuja kitambo,na mganga alishakufa zamani hamna wa kuweza kui renew,pasi na hilo ajivue gamba kwanza ili kidogo arudishe nyuma hasira zetu.
-LA KUVUNDA HALINA UBANI.
 
Mnapoteza muda wenu kumuongelea Lowassa na kumuhukumu pasipo ushahidi, kama ni mwizi mbona hakushitakiwa na kufungwa au kufilisiwa.
Hizo ni Kelele za kuku mwenye vifaranga, sizizomzuia mwewe kuchukua vifaranga. Mnapoteza muda wenu bure labda mumfufue Nyerere na Sokoine.
 
Wana JF, katika kipindi kifupi ambacho mh, Edward Lowasa aliongoza serikali maendeleo yaliweza kuonekana. Nitaje mambo machache ambayo ni miale ya maendeleo iliyooneshwa na huyu kiongozi shupavu: 1. Kila kata kujenga shule ya sekondari.2. Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kupata kozi ya muda mfupi ili kuongeza idadi ya walimu na kupunguza upungufu.3. Kila kata kuwa na kituo cha afya.4. Kuukataa mkataba usio na maslah wa mamlaka ya maji safi na maji taka DSM.5. Kufuta ada ya kudahiri watoto wanaoingia darasa la kwanza hivyo kuongeza idadi ya wanaoingia darasa la I.Ama kwa hakika tulikuwa bado tunamuhitaji na kama angeendelea kuwepo madarakani huenda sasa kila mkoa ungekuwa angalau na VETA kama siyo chuo kikuu.
Hayo uliandika juu mbona mengi hayakutokea kipondi akiwa waziri mkuu yeye, mf. No.1: shule za kata zilianza kujengwa wakati wa mkapa.
No.2: hiyo ilikuwa kipindi chake lakini ilprove failure maana watoto walikuwa hawaelewi.
No.3: Hiyo ya kila kata kuwa na kituo cha afya hapa dsm tu kata kibao hazina hata hiyo zahanati labda ungesema kila tarafa kuwa na kituo cha afya ningekuelewa.
No.4: aliifanya akiwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo hakuwa waziri mkuu.
No.5: ilifanyika mwaka wa kwanza tu wa uongozi wa Mkapa na sio kipindi cha Lowasa alivyokuwa waziri mkuu.
 
....na kungekuwa na Richmond katika kila sekta.
Wkt huohuo ukiri kwamba hakuhusika katika Richmond. Na uache kutumwa na watu kumchafua pasipo na ukweli(maana sababu za kilazimisha kuwa yeye anauhusiano na richmond unazowewe pekeee).
 
Hayo uliandika juu mbona mengi hayakutokea kipondi akiwa waziri mkuu yeye, mf. No.1: shule za kata zilianza kujengwa wakati wa mkapa. No.2: hiyo ilikuwa kipindi chake lakini ilprove failure maana watoto walikuwa hawaelewi.No.3: Hiyo ya kila kata kuwa na kituo cha afya hapa dsm tu kata kibao hazina hata hiyo zahanati labda ungesema kila tarafa kuwa na kituo cha afya ningekuelewa.No.4: aliifanya akiwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo hakuwa waziri mkuu.No.5: ilifanyika mwaka wa kwanza tu wa uongozi wa Mkapa na sio kipindi cha Lowasa alivyokuwa waziri mkuu.
Asant kwa kiniunga mkono japo unafikiri unanipinga, kwa hiyo umekubali kuwa Lowasa alifanya haya: 1: "Lowasa alihimiza kuwa kila kata ijenge shule na seko ili 80% ya watoto wanaomaliza drs la saba waende sekondari. 2: akiwa waziri wa maji alifuta mkataba wa Dawasco. Lakini bado hutaki kuukubali utendaji wake!?.
 
Back
Top Bottom