Prisoner 46664,
Tafadhali sana JK kiingereza hajui vilevile, nitaupload link moja kesho uone alivyoharibu kwenye jukwaa la kukabiliana na anguko la uchumi duniani lililofanyika Arusha cha kushangaza alikuwa anaongelea mambo ya uchumi na ana shahada ya uchumi lakini alionekana hawezi kuchambua mambo katika knowledge ya kiuchumi pia kiingereza kilikuwa kibovu bila kueleweka.
Unajua lugha ina ubovu wa aina tatu wa kwanza ni ubovu wa fasihi yaani grammar lakini unaeleweka kama Idd Amini wa Uganda pamoja na kuwa alikuwa anakosea katika fasihi lakini alikuwa anaeleweka sana anachoongea huitaji kumtazama machoni ujue anaongea nini, ubovu wa pili ni ile hali ya kutokuwa na uwezo wa kuunganisha maneno pia kujua hili litumike wapi.
Pia kutokuwa na vocabulary za kutosha ili kuiongea lugha pia katika huo ubovu wa pili ni kutumia tafsri ya moja kwa moja kutoka katika lugha mama.
Na ubovu wa tatu ni kuwa lugha unaifahamu, unavocabulary za kutosha lakini katika kutamka hueleweki vizuri hilo huwa sio tatizo sana maana unaweza kuandika ukafahamika au ukasoma tahariri au vitabu vya maarifa ukaelewa lakini ubovu wa pili huwa mbaya sana maana watu wa namna ile hata kuandika paper hawaezi kwasababu wana maneno machache katika lugha. kwa maana nyingine walikuwa weupe darasani
Mtu kama Idd Amin akiongea utajua elimu yake haikuwa kubwa tokana na grammar yake lakini alikuwa anaongea vizuri sana hata kutamka alikuwa anatamka vizuri sana kuliko hata Julius Nyerere au Kenyatta wa Kenya. Ndio maana tunasema katika lugha ufundi wa kuitamka lugha ni kipaji lakini kujua kuongea kawaida kwa kutumia fasihi ni usomi ndio maana nchi zinazotumia kiingereza na Marekani pamoja na kwamba wanaongea kiigereza hata kule China, au Japan au Urabuni msomi atatofautishwa na mtu wa kawaida katika ile lugha kutokana na grammar yake.
Hata hapa kwetu anavyoongea Mkapa, Sitta, kikwete, pinda katika kiswahili wanaongea kisomi sio kama watu wengi wa kawaida watakavyokiongea kiswahili pale Tandale, Mwanjelwa Mbeya, Babati, Lindi, Mtwara au usukumani Shinyanga.
Tusichanganye wazaramo na watu wa pwani kuongea kiswaili cha kipwani tukazania ni fasihi uliwasikiliza kwa makini hawatumii fasihi wanaharibu badala ya kuoga wataseka kukoga, badala ya kuosha vyombo watasema kukosha vyombo maana kuna lugha ya darasani ya ya mtaani